Apr 2, 2017
Usipoteze Uwezo Na Mafanikio Yako Kwa Kuamini Hivi…
Fikiria kuhusu
sheria ulizojiwekea na kile unachokiamini katika maisha yako. Sheria au kile
unachokiamini msingi wake unatokana na nini? Je, msingi wake umetokana sana na
wewe au unaiga tu maisha ya wengine?
Kwa mfano,
unaamini sana ukiwa na pesa basi tena utakuwa na matatizo kidogo au changamoto
umeziondoa kabisa. Kitu cha kujiuliza huo ndio ukweli au unajidanganya bado?
Unaamini pia ili
furaha yako iwe timilifu ni lazima ufanye mapenzi au uwe na wapenzi wengi ambao
wanakufariji. Kwa sababu hiyo unajisahau kwamba kumbe upo uwezekano mkubwa pia
wa kupoteza afya yako.
Pia unaamini sana huna
mafanikio ya aina fulani au huna kazi ya aina fulani kwa sababu hukusoma na
unajiona hufai. Hivyo, umekuwa mnyonge sana na kujilaumu kwa nini hukusoma.
Hata hivyo
unaendelea kuamini sana kwamba wewe hauko bora kabisa na kuwapa ubora huo watu
wengine na matokeo unasahau kutumia hata uwezo mdogo ulionao ili ukusaidie kufanikiwa.
Hata wewe unao uwezo mkubwa wa kufanikiwa, acha kujilinganisha sana. |
Kwa kuamini hivyo
umekuwa ukijipoteza kwa sababu umekuwa ukifuata sheria za wengine za mafanikio
walizojiwekea bila hata wewe kujua na kushindwa kabisa kufuata sheria zako za
mafanikio.
Unaamini sana kuna
ubora wanao ambao wewe huna au kuna njia pengine hata za mkato wanapitia ambazo
zimewapa wao mafanikio. Kwa hali kama hiyo umekuwa hufanyi kitu na kujiruhusu kushindwa.
Kitendo cha
kufikiria hivyo tu umekuwa ni mtu wa kupoteza muda wako bure. Tambua kila mtu ana kitu
bora cha kujivunia ndani yake ambacho kwa mwingine kitu hicho hakipo.
Sasa kama iko
hivyo kwa nini umekuwa ukijiweka kwenye hali ya unyonge sana kujibebesha lawana
kwa kuamini wengine ni bora kuliko wewe. Fikra hizi zinakuangusha, unatakiwa
kuzifuta mara moja.
Kwa kuamini fikra
hizo, umekuwa ukijipunguzia nguvu na mafanikio yako na kujikuta unawapa wengine
mamlaka na nguvu ya kufanikiwa na kujisahau wewe mwenyewe.
Ni wakati wa wewe
kutambua kwamba unao uwezo ambao unatakiwa kuutumia hadi kufanikiwa. Uwezo huo
unao ila utakuja kwa kuundeleza na sio kukaa tu na kutegemea muujiza.
Ondokana na fikira
za kwamba wengine ni bora kuliko wewe. Hata wewe una kitu ambacho wengine
wanaweza kukitamani na kukifanyia kazi. Sasa kama iko hivyo kwa nini ujidharau?
Kazi kubwa
unayotakiwa kuifanya kama nilivyosema ni kuendeleza kitu hicho ambacho unacho
na kikupe mafanikio. Acha kutulia, tambua uwezo au kipaji ulichonacho na
kukiendeleza.
Kama ni kipaji
kidogo ulichonacho, kitumie kikusaidie kufanikiwa. Kagua uwezo ulionao hiyo ni
njia sahihi ya kukusaidia kufanikiwa. Usiruhusu uwezo huo uwape watu wengine.
Ukweli usiojua ni
kwamba watu unaowaona wako bora kuliko wewe, kwa ndani wako kama wewe tu,
hakuna tofauti kubwa sana iliyopitiliza, zaidi yako wewe unajidharau tu.
Watu hao hawana
kanuni ya ajabu ambayo wanaitumia ambayo wewe huna, kikubwa unachotakiwa ujue
wanauendeleza uwezo wao sana karibu kila siku hadi kufikia mafanikio yao.
Ukiamua leo
kukiendeleza chochote ulichonacho uwe una uhakika utafika mbali sana kimafanikio
na kufanikiwa vikubwa. Hakuna kitachokuzuia ni lazima utafika kwenye mafanikio
yako.
Acha kupoteza
uwezo wako na mafanikio yako kwa kuamini kwamba wengine ndio wanaweza,
utapotea.
Ansante kwa
kutufatilia, washirikishe wengine waweze kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Mshauri
wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 628 929 816, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 628 929 816, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.