Apr 6, 2017
Ukitaka Mafanikio Ya Kweli Acha Kulalamika Juu Ya Mambo Haya.
"Hivyo ulivyo inatokana na
mtazamo ulionao" usemi huu niliwahi kukutana nao siku moja
katika pekuapekua zangu, usemi huu una ukweli ndani yake kwa asilimia zote
uzijuazo wewe, kwa sababu maisha yako hivyo yalivyo yanataokana na mtazamo na
imani ulizonazo.
Watu
wengi ambao hawajafanikiwa wanaamini ya kwamba mafanikio yanapatina kwa baadhi
ya watu fulani, lakini dhana hii si kweli kwa sababu kila mmoja mwenye pumzi na
fikra ana wajibu wakuweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Hivyo
nikwambie ya kwamba mafanikio makubwa yatakuwa upande wako endapo utaacha mara
moja kulalamka juu ya mambo yautayo;
1. Acha kulalamika juu ya elimu
uliyonayo.
Mafanikio
yatakuja kwako endapo utaacha kulalamika juu ya elimu uliyonayo. Watu wengi wanalalamika eti kwa sababu
ya elimu walizonazo, wengi husema mimi sina mafanikio kwa sababu sina elimu ya
kotosha, au nimesoma kidogo na sina elimu ya chuo kikuu.
Kiuhalisia,
dhana hii haina mahusiano ya moja kwa moja na mafanikio yako, hii ni kwa sababu
sio kila mwenye elimu amefanikiwa hivyo kwa elimu hiyohiyo ambayo unayo ni
kigezo tosha juu ya mafanikio yako. Hebu tujiulize watu wengi ambao
wamefanikiwa elimu zao ni kiwango gani?
Wajibika, acha kulalamika juu ya kitu chochote. |
2. Acha kulalamika eti hujafanikiwa
kwa sababu huna bahati.
Kama
nilivyoanza kueleza hapo awali ya kwamba mtazamo ndio kila kitu, imani hii ya
kuendelea kuamini ya kwamba mafanikio ni bahati nakuomba uachane nayo mara
moja, imani hiyo inaweza kukupoteza na ukashindwa kupata mafanikio kama
utaishikilia sana.
Tambua
imani kubwa juu ya mafanikio ni kwamba kila mmoja amezaliwa kwa ajili ya
kufanikiwa na si vinginevyo jambo la msingi ni kwamba mara zote hakikisha
unakuwa na mtazamo chanya, ubunifu, pamoja kufanya kazi kwa bidii haijalishi ni
kazi ndogo au kubwa kiasi gani.
3. Acha kulalamika eti huna pesa za
kutosha.
Hili
ndilo kikwazo cha mafanikio ya wengi hii ni kwasababu watu wengi wamekuwa
wanalalamika ya kwamba hawana pesa za kutosha ili wafanye jambo fulani,
kuendelea na tabia hii ni kujiua mwenyewe kwani siku zote pesa huwa hazitoshi.
Jambo
la msingi ni kuhakikisha kwa kiwango hicho cha pesa ulichonacho ni njia pekee
ya kuanza kufanya jambo unalolitaka, kwani endapo utaendelea kusubiri ufikishe
kiwango fulani cha pesa ndio uanze kufanya jambo fulani nakuhakikishia huwezi
kufanya kamwe.
4. Acha kulalamika juu ya serikali
kama kweli unataka kufanikiwa.
Maisha
yako yapo mikononi mwako, hata hivyo kama kweli unaamini hili hakikisha unakuwa
bora sana katika kutafuta kusudio lako katika dunia hii, nasema hivi kwa sababu
watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wao kazi yao ni kuilaumu serikali
tu.
Na
watu hao wamekuwa wakifanya hivi huku siku sikizidi kwenda na wao maisha yao
yamekuwa hayabadiliki, jambo la msingi ambalo nataka kukuasa ni kwamba
kila mmoja asimame kidete katika kuyapigania maisha yake ambayo yatamtengezea
kesho yake bora.
Hivyo
nikuache kwa kukuambia ya kwamba endapo utaendelea na tabia yako ya kulalamika
ni kutengeneza maisha yako kuwa duni zaidi.
Nukuu
ya siku inasema "kulalamika ni adui
namba moja wa mafanikio yako"
Ndimi afisa mipango na mwanamafanikio,
Benson Chonya,
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.