Apr 17, 2017
Kuwa Makini Sana Na Mambo Haya Yanaweza Kukuzia Kufanikiwa Kwako.
Kuna wakati unaweza ukawa unashangaa kwa nini
ndoto zako hazitimii? Utakuta umejiwekea malengo yako vizuri, lakini
unashangaa ni malengo machache sana yanayotimia au wakati mwingine hakuna kabisa.
Sina shaka yoyote umeshawahi kukutana na hali
kama hii wakati fulani katika maisha yako. Kiuhalisia, yapo mambo mawili ambayo
kitaalamu hupelekea ndoto zako kushindwa kutimia ikiwa hutayajua vizuri.
Jambo la kwanza, ni kutokujua kile unachokitaka
vizuri. Hili ni jambo ambalo hupelekea wengi kushindwa kufanikisha ndoto zao
kabisa. Kama hujui kile unachokitaka vizuri, suala la kufanikisha ndoto zako
litakuwa gumu kidogo.
Katika akili yako ili uweze kufanikisha ndoto
yako au jambo unalolitaka kwa urahisi, ni lazima kile kitu unachokitaka uweze
kukijua vizuri. Tambua njia utakazotumia hadi kukipata kitu hicho pia tambua
kitu hicho changamoto zake ni zipi.
Acha kufanya kosa la kuuchanganya ubongo wako
kwa kuupa vitu vingi. Kuwa maalumu kwa kujua vizuri kile unachokitaka. Usipojua
kile unachokitaka kwa uhakika na kukifanyia kazi, ni wazi hutaweza kufanikiwa
na hilo halina ubishi.
Jambo la pili, ni kukosa hamasa ya kutosha kwa
kitu hicho unachokitaka. Hamasa ni kitu cha muhimu sana ili kufikia ndoto zako.
Ukishakijua kitu hicho vizuri, hamasa itakusaidia kufanya kila jitihada hata
kama umechoka.
Wengi ni watu wa kutaka kufikia lengo fulani
katika maisha yao, lakini kwa bahati mbaya hujikuta ni watu wa kukosa hamasa ya
kuwasukuma kuweza kukamilisha malengo yao.
Ili kufanikiwa, fanya kila ufanyalo kuhakikisha
una hamasa ya kufanya hicho unachotaka kukifanya katika maisha yako. Inapotokea
hamasa hiyo umeikosa acha kusimama eti kwa sababu ya kukosa hamasa.
Maisha hayasimami eti kwa sababu wewe hujisikii
kufanya kitu fulani au umekosa hamasa. Endelea kusonga mbele, huku ukitafuta
hamasa ya kufanikiwa kwako kila siku. Ukifanya hivyo utafika mbali kimafanikio.
Katika hali ya kawaida, kama kila wakati unakosa
mambo haya mawili suala la kufanikiwa kwako linakuwa ni gumu sana. Hivyo, ni
lazima sana kwako kujua vizuri kile unachokitaka na kuwa na hamasa kubwa yaani
‘burning desire’ ya kuhakikisha kitu hicho ni lazima unaweza
kukipata.
Ukichunguza watu wengi ambao hawajafanikiwa
wanashindwa kufanikiwa kwa sababu hizi mbili tu na si vinginevyo. Kama
unafikiri natania anza kufatilia, huku lakini ukianza na wewe.
Kama unajiona hujafanikiwa vya kutosha jiulize
binafsi je, unakijua vizuri kile unachokitaka na huna tamaa ya kutaka
hiki mara kile na mwisho wa siku kuwa na malengo mengi yasiyotekelezwa?
Usiishie hapo tu, tena kama unaona hujafanikiwa
vya kutosha jiulize, je, una hamasa kubwa ya kuona ndoto zako zinatumia? Je,
unakosa usingizi na kuamua kujituma usiku na mchana hadi kufanikiwa?
Ukipata majibu ya maswali hayo yatakusaidia sana
kuweza kufanikiwa na kuwa mtu mwingine tofauti na hatimaye kuweza kufanikisha
zoezi zima la kutimiza ndoto zako. Jitoe kikamilifu kuona ndoto zako zinatimia
kwa kuyajua mambo hayo mawili.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 628 929 816, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.