Apr 10, 2017
Mtazamo Chanya Bila Kuwa Na Kitu Hiki Ni Sawa Na Bure.
Inasemekana ya kwamba mtazamo chanya ni rasilimali tosha dhidi
ya kuuaga umaskini, aidha watalamu wa masuala haya ya elimu ya mafanikio
wanazidi kusisitiza ya kwamba ili mtu aweze kufanikiwa anakiwa kuibeba
mitazamo hiyo chanya kila wakati.
Lakini licha ya watu wengi kuibeba mitazamo hiyo chanya wamekuwa
wakisahau kitu kimoja, kitu hicho ni muhimu sana kwani huenda
sambamba na mitazamo hiyo chanya. Na leo nataka nikwambie kitu hicho, kwani
kuwa na mtazamo chanya bila ya kuwa na kitu hicho ni sawa na bure.
Kitu chenye ni hiki, mtazamo chanya huenda sambamba na "
kuwajibika" watu wengi kama ujuzi na maarifa wanayo ya kutosha, ila
tatizo ni kule kunakowafanya watu hao kuwa mtazamo chanya zaidi ila wamesahau
kuwajibika juu ya kitu walichonacho.
Tangu umeanza kujifunza mambo mbalimbali ya mafanikio naamini
mpaka sasa kwa sehemu fulani una mtazamo chanya juu ya jambo fulani, ila
kinachokosekana kutoka kwako ni kule kunakoitwa kuwajibika juu ya mtazamo huo.
Hivyo mimi naamini kutokufanikiwa kwako kimaisha umeamua mwenyewe,
nasema hivi kwa sababu hutaki kuchua hatua kwa ile hali uliyonayo, wengi huamini
mafanikio huja kesho, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda hujikuta maisha yao
yapo vilevile na hiyo kesho yao isiyokuwa na mipaka.
Kama wewe ni miongoni mwa watu wanaosema nitafanya kesho,
nakusihi ya kwamba achana na dhana hiyo kwani mafanikio ya kesho hutengenezwa
na leo, pia amini kwamba binadamu huishi siku moja, siku hiyo leo, kesho si
rafiki kwako.
Hivyo kwa kile kidogo ulichonacho mathalani mtazamo chanya ulionao
ni nguzo sahihi ya mafanikio yako endapo utaamua kuwajibika juu ya jambo hilo
unalolifahamu. Kuchukua hatua ni sehemu kubwa ambayo itakutoa hapo ulipo kwenda
sehemu nyingine ya mafanikio.
Ni wako Afisa Mipango Benson Chonya.
0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.