Feb 28, 2018
Wanaoficha Pete Za Ndoa Hawajui Kupenda.
Unapomkuta
mwanamke au mwanaume ambaye yuko kwenye ndoa, amevua au huwa anavua pete yake
ya ndoa mara kwa mara na kuiweka kwenye mkoba wake au mfukoni, utasemaje?
Ni
lazima kuna namna ambayo utamfikiria mtu huyo. Je, utamfikiria kwamba ni malaya,
haridhiswi na ndoa yake, au hampendi mumewe au mkewe?
Hapa
nitajaribu kutoa maelezo ambayo, yatakufanya usihisi vibaya kwa kile ambacho,
umekuwa ukikifikiria kuhusu mwanamke au mwanaume wa aina hiyo.
Imeelezwa
kwamba, wale wanawake au wanaume ambao, huficha pete zao za ndoa, ni watu ambao
hawana uwezo wa kulea watoto, yaani huwa wanawapuuza sana watoto wao.
Kwa
kulinganisha, inaelezwa kwamba, wale wanawake au wanaume wenye kuvua au kupenda
kuvua pete zao za ndoa na kuziweka mikobani, huwa wanawapuuza watoto wao kuliko
wale ambao, huvaa pete zao muda wote.
Weka wazi pete yako ni ishara ya upendo. |
Lakini
pia, inaelezwa kwamba wale wanawake au wanaume wenye sura za kuvutia au nzuri
sana wanapokuwa na tabia hii ya kuficha pete zao za ndoa, huwa ni wazazi
wasioweza hata chembe kulea watoto wao, yaani wanakuwa ni wazazi aambao, ni
watekelezaji sana, wasiojali kabisa kuhusu watoto wao.
Katika
moja ya tafiti zake mwanasaikokoljia Andrew Harell wa chuo kikuu cha Alberta nchini Canada, anasema kwamba, hili sio
suala la kubahatisha, kwani amelifanyia utafiti kwa wengi, kwa muda mrefu na
katika mazingira tofauti.
Mwanasaikolojia
huyo anazidi kudai kwamba, hata linapokuja suala la kuangalia na kutunza
wagonjwa, wale watu wanaoficha pete zao za ndoa, hawana uwezo wa kuwatunza
wagonjwa ukilinganisha na wale wenye kuvaa pete.
Inaelezwa
kwamba, kuvua pete ya harusi na kuificha ni ishara kwamba, mwenye pete hiyo
hana hisia au uwezo wa kujifunga na ndoa yake au familia yake. Kwa kukosa sifa
hizo, ni wazi mtu huyo hawawezi kujifunga na watu wengine wenye kuhitaji msaada
wake wa kihisia kama vile wagonjwa.
Kuvua
au kuficha pete ya ndoa, kunahesabiwa kama ni dalili ya mtu kutaka kuanzisha
uhusiano mpya nje ya ndoa yake. Haja hiyo inapotimizwa, uwezekano ni mkubwa kwa
mwanaume au mwanamke kupunguza upendo au kujali familia yake, akiwemo mke au
mume au watoto. Kwa hali hiyo, kuficha pete ni dalili ya kutokujali na
kushindwa kujifunga kwenye uhusiano.
Wakati
huo huo taarifa za kitafiti zinaonyesha kwamba, wazazi wenye kuvua pete huwa
hawatoi uangalifu mkubwa kwa watoto wao wenye sura mbaya, ukilinganisha na ule
wanaoutoa kwa watoto wao wenye sura za kuvutia au wazuri.
Katika
moja ya tafiti zilizowahi kufanywa, zilihusisha
wazazi na watunza watoto walioenda na watoto hao kwenye supermarkert. Ilionekana
kwamba, wale watoto wasiopendeza, waliachwa kwa umbali mkubwa bila wazazi wao
kujali, wakati wale watoto wenye kuvutia, wazazi au walezi walikuwa nao karibu
sana.
Tafiti
zote hizo zinajaribu kuonyesha upo uhusiano mkubwa sana kati ya kitendo cha kuvua pete
na suala zima la kujali. Je, hali hiyo kwako ikoje? Huu ni utafiti tu, wewe je,
unasemaje?
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku. Pia chukua jukumu la
kumshirikisha mwingine, ili aweze kujifunza na kunufaika na masomo yanayotolewa
humu.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA ESTHER ZACHARIAH,
DAR ES SALAAM.
MAWASILIANO; esterzacharia73@gmail.com
Feb 27, 2018
Fursa Za Kunufaika Nazo Katika Ufugaji Wa Kuku.
Rafiki, fursa zipo
nyingi ambazo zinatokana na ufugaji wa kuku leo naenda kukueleza fursa ambazo
zitakusaidia wewe kukua zaidi kiuchumi huku ukiwanufaisha jamii kubwa ya watu
ulionao katika maeneo yako na taifa kwa ujumla.
Rafiki tumejifunza
mambo mengi kuhusu ufugaji wa kuku kila kitu unachopasa kukijua kuhusu ufugaji
wa kuku tayari umekijua sasa ni wakati wa utekelezaji tu na siyo maneno tena
kwa sababu mafanikio yanatokana na hatua sahihi unazochukua.
Unapoweka mipango ya
kufuga kuku usiishie tu kupanga kufuga kuku mia au kuku elfu moja usiishie
kufuga tu fikiria kufuga na kuzalisha mayai yakutosha kwa ajiri ya kuboresha afya
kwa jamii kubwa ya watu wanaotuzunguka.
Kwa Tanzania bado upo
mkubwa wa mayai hasa mayai ya asili ni adimu sana hebu rafiki amka uikoe jamii
kubwa ya watanzania wanaokosa mayai kwa ajili ya chakula, kwani uhitaji bado
ni mkubwa.
Kunielewa vizuri ngoja
nikwambie kitu rafiki najua unafahamu kuwa mimi ni mfugaji na pia unafahamu
kuwa nilikuwa natangaza kuhusu watu wanaohitaji mayai, lakini kwa sasa hata
sitangazi tena kuhusu mayai kwa sababu mahitaji ya watu ni makubwa.
Watu wamekuwa wakiweka oda kwa zaidi ya wiki
tatu wote hao wanahitaji mayai nashindwa kuwafikia wateja wote kwa wakati
uhitaji umekuwa mkubwa kuliko uzalishaji nimekuwa nikiwasiliana na wazalishaji
mbalimbali ambao wanafuga kuku lakini hawajawa na uhakiki wa mayai.
Kwa wakati sahihi sasa
nimefikilia kuzalisha mayai kwa wingi ambayo yatakuwa yana uwezo wa kuwafikia
wengi zaidi kwa wakati, Rafiki panga na wewe kuwa sehemu ya watu watakao
nufaika na mradi huu wa kuku.
Nakupendekezea kwako rafiki
tumia njia ya sayansi katika kupunguza gharama ya chakula cha mifugo yako,
ongeza uzalishaji wako, lifikie soko kubwa zaidi, na hapo utakuwa na uhakika
mkubwa wa kipato chako.
Pia ngoja nikwambie jambo rafiki , iwapo utafanya
ufugaji wako kwa kutumia sayansi yakupunguza gharama ya chakula basi utafanya
ufugaji wako kwa gharama ya chini sana baada ya kuuza kwa bei kubwa wewe uza
kwa bei ya kawaida tu.
Kama sokoni mayai ya asili
yanauzwa mia tano wewe uza kwa mia tatu hadi mia nne kwa sababu gharama za
uendeshaji kwako zitakuwa chini sana ukilinganisha na wafugaji wengi ambao wanafuga
bila kutumia sayansi hii.
Unaweza ukajiuliza kwanini
mayai ya kisasa yanauzwa bei ya chini na mayai ya asili (kuku chotara) yanauzwa
bei ghari? je jibu nikiwa na mayai ya asili
ni adimu kupatikana ndio maana bei yake ni kubwa ukilinganisha na mayai ya
kisasa.
Naomba nikuulize rafiki
nani mkombozi wa jambo hili siyo mwingine ni mimi na wewe tunajukumu la
kuzalisha mayai kwa wingi yawe ya kisasa au ya asili bado yanahitajika sana kwa
jamii yetu mimi nimeanza wewe je?
Weka mipango yako sawa
wewe rafiki usifikirie kuishi kufuga kuku wachache fikiria kuwa na matawi kubwa
ya mayai, fikiria kusambaza mayai Tanzania nzima, mayai yanahitajika siyo
nasema uongo.
Jambo lingine utakalo
nufaika nalo ni kuwa na oda nyingi kutoka sehemu mbalimbali kama vile
mahotelini, kwenye mighahawa, kwenye vibanda yya chipsi, majumbani, maofisini
na maeneo mengine mbalimbali.
Kwa leo nimekupa
mwanga tu wa fursa za kunufaika nazo kutokana na ufugaji wa kuku. Na ukumbuke
tumeongelea fursa moja tu ambayo ni kufungua matawi ya uuzaji wa mayai kwa wingi
sana. Je, fursa ipi inafata itokanayo na ufugaji wa kuku? Tukutane wiki ijayo
katika somo linalofuata.
Ni mimi wako katika
ufugaji,
FRANK MAPUNDA,
0656 918 243.
Feb 26, 2018
Mbinu Za Kuongeza Mauzo Katika Biashara.
Yapo mambo ya msingi ambayo mfanyabiashara yeyote yule ili aweze
kukua katika biashara yake ni lazima ayafahamu, na mambo hayo si mengine bali
ni jinsi gani anatakiwa kuongeza kiwango chake cha mauzo.
Na si kuongeza kiwango cha mauzo pekee, bali kuhakikisha anapata
faida kubwa kwa kile anachokifanya. Wapo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa
hawalizingatii hili na kupelekea bidhaa au huduma wanazozitoa kutofanya vizuri
sokoni.
Kwa minajili hiyo nikaona ni vyema ili kuweza kuwasadia
wafanyabiashara hao ili wapone ni vyema niandike makala haya ili ikusaidie
kuweza kuongeza kiwango chako cha mauzo katika biashara unayoifanya.
Kwanza kabisa ili uweze kuongeza kiwango cha mauzo katika
biashara ambayo unaifanya unatakiwa kuachana na mfumo wa zamani ambao ulikuwa
unatumia katika kufanya biashara yako, kama inashindikana kuachana na mfumo huo
wa zamani basi unachotakiwa kufanya ni kuboresha mfumo huo wa zamani ili uweze
kufanikiwa kibiashara.
Jambo jingine ambalo ni muhimu kabisa ambalo unatakiwa
kulikumbatia katika biashara yako ni, kuelewa mbinu za kufanya
biashara ya yako kwa kutumia mitandao ya kijamii. Kwa wenzetu wazungu
mfumo huu huitwa affiliate marketing, ambapo kwa kibantu
tunaweza tukasema ifike mahala utengeneze mifumo thabiti, mfumo huu utakusadia
kutenggeza pesa ukiwa umekaa tu nyumbani.
Wakati mwingine unaweza ukasema labda njia hii haiwezekani
kuleta matokeo chanya, lakini ninachotaka kusema hakuna lisilo wezekana chini
ya jua hii ni kwa sababu dunia ya sasa imekuwa kiganjani mwa wadamu, kila kitu
ambacho unakitaka utakipata kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kifupi
dunia ya sasa inakwenda kasi sana tofauti na ilivyokuwa nyuma.
Na ili uweze kwenda sawa na kasi hiyo ni lazima jifunze mbinu
mbalimbali zitakazokusaidia kuuza bidhaa au huduma kwa kutumia mitandao ya
kijamii, kwani kwa sasa wanaitumia njia hiyo ndiyo ambao wanafaidi matunda ya
kutumia mbinu hizo.
Jambo jingine ambalo litaweza kukusaidia kuweza kuongeza mauzo
ya katika biashara unayoifanya ni kuhakikisha unakuwa mtalamu katika biashara
husika. Hii mbinu muhimu sana katika kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara
kwa sababu pindi utakapokuwa mtalamu au m-bobezi wa jambo hilo itakusaidia sana
kuweza kuizungumzia vizuri bidhaa au huduma unayoitoa kwa mteja wako,
kufanya hivyo kutamfanya mteja huyo ainunue bidhaa hiyo. Hivyo ili uweze
kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara yako jifunze kuwa mtalamu katika
eneo husika unalolifanya.
Jambo la mwisho ambalo ni muhimu sana litakalo kusaidia kuweza
kufanya biashara yenye tija ni kuhakikisha unaimarisha vizuri upande wa huduma
kwa mteja, kwa sababu ule usemi wa kwamba mfalme ni mteja hakuwepo tu, bali
msemo huo upo kumanisha kweli, mteja ni mfalme pindi awapo na asipokuwapo
katika eneo lako la kibiashara pia.
Ufike pahala neno mteja liwe lina maana kubwa sana
katika biashara yako, yaani mfanye mteja kuwa ni sehemu ya biashara ya yako.
Mfanye mteja ajisikie huru katika suala zima la kibiashara.
Mwisho nimalize kwa kusema biashara yenye tija hujengwa na vitu
vitatu vya msingi ambavyo ni bidhaa au huduma nzuri+ masoko mazuri= wateja
wengi.
0757-909942.
Feb 25, 2018
Kwa Chochote Unachokifanya Ili Ufanikiwe, Anza Hivi Na Maliza Hivi.
Iwe
wewe ni shabiki wa kuangalia mchezo wa kukimbia alimaarifu riadha au siyo,
lakini kwa vyovyote najua umeshawahi kuangalia mchezo huo hata mara moja na
kushuhudia wale washindi wanakuwa wanapatikanaje.
Kama
utakuwa umesahau kidogo naomba nitakukumbusha hapa, washindi katika riadha, hususani
zile riadha za mita mia moja, wanakuwa wanapatikana kutokana na kuanza kwao kwa
kasi na kumaliza kwa kasi.
Hayupo
mshindi katika riadha wa mita hasa mia moja kama nilivyosema anayeanza kukimbia
kidogo kidogo halafu akawa mshindi kwa madai ya kukazana mwishoni au hakuna ambaye
anaanza kwa kasi na mwishoni kukimbia kidogo kidogo na akawa mshindi.
Mchezo
huu wa riadha mara nyingi kama unataka ili uwe mshindi ni lazima uanze kwa
nguvu, uendelee kukimbia kwa nguvu ukiwa kwenye mbio na wakati huoho umalize
kwa kukimbia kwa nguvu sana kwani washindi wanapatikana pale mwishoni.
Hiyo
yote inatuonyesha mtu anayeshinda mbio, huwa hapunguzi kasi pale mwishoni bali
ndio huongeza kasi, bila kujali anakutana na changamoto za aina gani iwe
kuchoka au kuna hata wakati alidondoka, lakini ni lazima kuongeza kasi ili kushinda.
Halikadhalika
pia kwa upande wa mafanikio, yanategemea na watu wanaonza kitu chochote kwa
nguvu na kumaliza kwa nguvu pia. Kufanikiwa kwa kitu chochote kile ndio
kunakuja kwa namna hiyo na sio vinginevyo.
Tatizo
hapa la watu wengi wanapoanza jambo fulani wanakuwa wanaanza kwa kasi sana, lakini
inapofika katikati ile pumzi yao ambayo wanakuwa wameanza nayo kwa hakika
inakuwa inakata hali ambayo hupelekea kushindwa kabisa.
Na
kinachokuwa kikipelekea wao kuzidi kupunguza kasi na mwisho kuweza kupotea hapa
katika ni kutokana na changamoto, kutokijiamini na wasiwasi ambao wanakutana
nao hapa kati kati na mwisho wa siku hujikuta wako nje ya mstari wa mafanikio.
Unatakiwa
ujue mafanikio yanategemea sana wale wote wanaoweka juhudi kuanzia mwanzo na
kendeleza juhudi hizo mpaka mwisho wa mafanikio yao. Mafanikio ndivyo
yanavyotengenezwa na watu wa namna hiyo.
Kitu
pekee ambacho kitakufanya uanze jambo lolote kwa nguvu na umalize kwa nguvu ile
ile pasipo hapa wewe kati kati kuweza kupotea kwa namna yoyote ni kujitoa kwako
na kujenga mtazamo. Haya mambo yatakusaidia sana.
Unapokuwa
umeamua kujitoa na kujenga mtazamo chanya, hapa kati kati hata ukikutana na
changamoto nyingi, hutaweza kulalamika zaidi utaongeza mwendo kwa sababu unajua
vyema ni wapi unakoenda na unatakiwa umalize vipi ili uwe mshindi.
Nikukumbushe
tena washindi katika mafanikio wana anza kwa nguvu, wanaendelea kufanya kwa
nguvu na wanamaliza kwa nguvu pia kila wakati. Hii ndio kanuni wanaoyoitumia na
wewe unatakiwa uitumie vivyo hivyo pasipo kubabaishwa na kitu.
Kwa
chochote ambacho umechagua kukifanya, kianze kwa nguvu, endelea kukifanya kwa
nguvu na pia kimalizie kwa nguvu. Usije ukafanya kosa la kuanza kwa nguvu na
kumalizia kwa udhaifu, hutashinda ila utashindwa ukifanya hivyo.
Chochote
unachokifanya kitakupa ushindi ukiwa utakianza kwa nguvu na kukimalizia kwa
nguvu pia. Hakuna hali au mazingira ambayo yatakuzuia kufanikiwa kama moto ule
ule ulionanza nao na ndio huo utakaomaliza nao.
Amua
sasa kuwasha moto wa mafanikio yako kuanzia mwanzo hadi mwisho, pasiwepo kitu
chochote hapa kati ambacho kitaweza kujitokeza na kuzima moto huo. Wewe ni mshindi,
anza kwa nguvu, endelea kufanya kwa nguvu na maliza kwa nguvu.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Feb 24, 2018
Sehemu Sahihi Ya Kuanzia Mafanikio Yako Ni Hii Hapa.
Bila kujali upo mbali
kimafanikio kwa kiasi gani, lakini bado unayo nafasi ya kuchagua kuendelea
mbele kwenye safari ya mafanikio yako.
Si kitu cha ajabu sana kwako
na kwa wengine pia wanapoona wako mbali kimafanikio, hasa kwa kuwalinganisha na
wengine wanaanza kukata tamaa.
Kitu ambacho watu hawa wanakuwa
hawajui ni kwamba, mafanikio hayategemei sana au hayajali eti upo mbali sana,
bali kinachojalisha ni mwelekeo wako.
Mwelekeo ndio kitu cha
msingi sana katika safari yako ya mafanikio, hiyo ikiwa na maana pale ulipo kwa
sasa unaelekea wapi kimafanikio.
Kama mwelekeo wako ni
sahihi, basi hakuna shaka hata kama mwendo wako ni kidogo kama wa kinyonga
lakini wakati upo utafanikiwa.
Kikubwa ambacho hutakiwi
kukipoteza kwenye maisha yako ni ule mwelekeo wa kule unakoenda kwenye maisha
yako. Ukipoteza mwelekeo ndio basi huwezi kufanikiwa.
Watu wengi hawafanikiwi
katika maisha sio kwa sababu ya kwamba wapo mbali kwa hiyo ni ngumu kufanikiwa.
Hawafanikiwi kwa sababu hawana mwelekeo.
Hata katika mazingira ya kawaida
kitu chochote kikosa mwelekeo hakiwezi kufika kule kunakotakiwa kufika, lazima
kitapotea hapa katikati.
Kwa mfano, ukiangalia ndege
inaporuka hewani inakuwa na mwelekeo fulani unaoongozwa na rubani. Inapotokea
mwelekeo huo haupo, basi ndege haiwezi kufika.
Na maisha yako hayana
tofauti sana na hivyo. Maisha yako yanahitajji mwelekeo kwanza na sio wapi
ulipo kimaisha ndio iamue hatma yako.
Kama umekuwa bado
unasingizia kwamba eti uko mbali kimaisha na ndio maana hufanikiwi, huo sio
ukweli ni uongo.
Wewe sehemu ya kuanzia kwenye
safari yako ya mafanikio ni kutafuta mwelekeo. Ukiupata mwelekeo basi njia kuu
ya mafanikio umeiona.
Unatakiwa sasa kujiuliza
karibu kila siku, mwelekeo wa maisha yako uko wapi. Kitu gani utakachofanya
ambacho kitakupa mwelekeo sahihi wa maisha yako.
Hutakiwi kulaumu hata siku
moja pale ulipo, unatakiwa ushukuru kwanza, kwani sehemu ulipo hapo ndipo
unatakiwa kuanza kutafuta mwelekeo wa mafanikio yako.
Hutaweza kufanikiwa kama
hautaweza kuanza kutafauta mwelekeo
wako, sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio kama nilivyosema ni kujua mwelekeo
wako pale ulipo.
Hakuna kitu ambacho kitaweza
kushindikana kwako, kwa sababu utakuwa umeamua kutafuta kwa dhati sehemu ya
kuanza kutafuta mafanikio yako.
Amua leo iwe siku ya kuanza
kutafuta sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio yako kwa kutafuta mwelekeo wa wapi
uende.
Usiruhusu mtu akwambie
huwezi kufika, kule unakotaka kufika kimafanikio, wakati una uwezo wa kuanza
kutafuta mweleko wako na kusonga mbele unao.
Usiruhusu mtu akakukatisha
tamaa iwe kwa vitendo au kwa chochote kile kwamba wewe upo mbali sana na
hautaweza kufanikiwa.
Usiruhusu tena wewe mwenyewe
ndani yako ukajiambia kwamba, kwa maisha haya niliyonayo ndio basi tena siwezi
kufanikiwa.
Hutakiwi kuruhusu chochote
kile ndio kikawa chanzo cha wewe kushindwa kuwa na mwelekeo sahihi wa maisha
yako.
Kila wakati unatakiwa kujua
ule uwezo wa kufanikiwa na kufika ngazi ya juu kimafanikio unao, kwa sababu sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio
yako umeshaiona.
Kama kuna watu wanaoendelea
kukubeza, waache waendelea kukubeza na hiyo itakula kwao, wewe endelea kuchanja
mbuga kutafuta mwelekeo wako kimafanikio.
Hutakiwi tena kujiuliza
uliza au kumuuuliza mtu kwamba ni wapi mafanikio yanapoweza kuanzia au ni
sehemu gani.
Kitu cha kukumbuka
ulichojifunza hapa ni kwamba mafanikio yako, sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio
yako ni kwa wewe kuchukua hatua.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
\
Feb 23, 2018
Huu Ndio ‘Ugonjwa’ Mpya Hatari Usipothibitiwa Mapema, Utaangamiza Familia Nyingi.
Inafahamika yapo magonjwa mengi sana, ambayo yamekuwa tishio kwa familia na jamii inayotuzunguka kwa muda mrefu. Magonjwa hayo yapo ambayo yamekuwa yana dawa na yapo ambayo hayana dawa, lakini yapo.
Kwa
kuwa mimi si daktari hapa katika makala haya sitataja sehemu ya magonjwa hayo
ambayo yamekuwa ni hatari kwa familia, pengine na taifa kwa ujumla, bali hapa
mimi nitazungumzia ugonjwa mmoja tu ambao naufahamu ila ni hatari sana.
Ugonjwa
huu ambao nauzungumzia hapa na ambao ikiwa hauathibitiwa mapema, basi tujiandae
kupoteza familia nyingi na kuzipeleka kubaya zaidi, ni ugonjwa wa mmonyoko wa maadili,
ndio nimesema ni mmonyoko wa maadili.
Kwa
miaka ya hivi karibuni ukifatilia kwa makini, utagundua swala la kuporomoka kwa
maadili kadri siku zinavyokwenda mbele nalo limekuwa likiongezeka kwa kasi.
Watoto wa sasa, wamekuwa si watoto wa
miaka ile, mambo yamekuwa yametofautina sana.
Malezi bora kwa watoto yanatakiwa kusimamiwa vizuri. |
Hilo
unaweza ukaliona vizuri kwa watoto wa sasa, kama si wa kwako basi wa jirani na
kama si wajirani basi ni wa ndugu. Lakini kitu ambacho kipo na kinaendelea
kutokea katika jamii zetu tunamoishi kila siku.
Najua
walezi wa watoto kama wazazi, walimu pia ambao kwa sehemu wanajukumu la kukaa
na watoto kwa muda mrefu, hapa wanaweza wakawa wananielewa kwa uzuri sana kwamba
mmomonyoko wa maadili tayari limekuwa ni tatizo au ugonjwa ambao unakuja kimya
kimya.
Kwa
bahati mbaya sana kila mtu anakazana na kinga ya nyumbani kwake na wengine hata
hiyo kinga hawaijui, matokeo yake watoto wanakuwa wanalelewa tu kama kibahati, na
mwisho wa siku ni hatari kubwa ambayo inapelekea mmonyoko wa ukweli.
Kiuhalisia
ukiangalia yapo mengi yanayosababisha ‘ugongwa’ huu wa mmonyoko wa maadili kwa
sasa kutokea kwa kasi kuliko wakati mwingine. Moja ya msingi mbovu inaweza
ikawa ni malezi mabovu ya wazazi na walezi kwa watoto na hata pia mitandao ya
kijamii.
Hivi
ni vitu ambavyo vinaweza vikawa na mchango mkubwa sana kupelekea mmonyoko wa
maadili kwa watoto wetu. Na pasipo vitu hivi au swala hili la mmomonyoko wa
maadili kudhibitiwa basi taifa la kesho tutakalokuwa nalo litakuwa ni bovu sana.
Unaona
mpaka hapo ni jukumu la kila mmoja wetu kusimamia kwa umakini swala la mmonyoko
wa maadili kutokuendelea, vinginevyo tutakuwa na taifa ambalo litakuwa halina maadili
kwa siku za huko baadae.
Ni
imani na mategemeo yangu wazazi na walezi watajitahidi kuziba mianya yote inayopekeleka
mmonyoko wa maadili. Hayo yote hayawezi kufanikiwa pasipo kutoa ushirikiano kwa
wazazi wote.
Pia
walimu wetu inatakiwa washirikishwe na watiwe moyo na wazazi katika kuhakikisha
watoto wanalelewa katika maadili mazuri na bora. Kila mtu akisimama katika
nafasi yake mabadiliko yatawezea kutokea.
Lakini
ikiwa tukishindwa kuthibiti kwa sasa mmomonyoko wa maadili, basi tujiandae kuwa
na kizazi ambacho kitakuwa kipo kipo tu.
Mpaka hapo ieleweke hatujachalewa, uwezo wa kuthibiti ‘ugonjwa’ huu wa mmonyoko wa maadili inawezekana.
Inawezekana
unajiuliza tunaanzia wapi, anzia hapo ulipo, ‘mtoto wa mazazi mwezio ni mtoto wako pia.’ Kama unaona mtoto
amekosea kitu hata kama sio wako, chukua jukumu la kumuonya.
Pale
mtoto atakapogundua alaa kumbe anaweza kuonywa na mzazi ambaye si wake, najua
atajirekebisha na vivyo hivyo tutajikuta tuna kizazi chema, kizazi ambacho
tutakifurahia siku za usoni kwenye maisha yetu.
Watengenezaji
wa maisha ya watoto wetu ni sisi wenyewe, jukumu ni letu sote. Tuchuke hatua za
kuweza kubadili sisi kwa kuwa wazazi au wazazi wawajibikaji na kwa kufanya hivyo
tutaweza kuthibi ‘ugonjwa’ huu wa
mmonyoko wa maadili.
Fanyia
kazi ujumbe huu, linda kizazi cha kesho kwa kukipa maadili bora na ya manufaa
leo na si kesho.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Feb 22, 2018
Hizi Ndizo Biashara Ambazo Haziwezi Kufa.
Mara
nyingi inapotokea uchumi umeyumba au uchumi mbovu kunakuwa na idadi kubwa ya
biashara kuweza kuyumba na zingine kuweza kufa kabisa. Hali hii hupelekea watu hasa
wafanyabishara kuanza kupata tabu kwa kuyumba kiuchumi pia.
Ndio
maana kabla hujafanya biashara unashauriwa kufanya utafiti wa kutosha na
kuangalia ni biashara zipi ambazo zina mahitaji mengi au zinaweza zikadumu kwa
muda mrefu pasipo kuteteleka au kufa kabisa hata kitokee kitu gani.
Pegine
unajiuliza kweli kuna biashara ambazo haziwezi kufa? Katika mazingira ya kawaida
unaweza ukakataa ukasema kwamba, kila biashara inaweza kufa. Lakini hapa leo
nataka ni kukuonyesha biashara chache tu ambazo haziwezi kufa.
Katika
makala hii, biashara hizo sitazichambua kwa kina bali nitakuonyesha tu mwanga au
njia kisha utatafakari na kuangalia ukweli na uhalisia wa biashara hizo ambazo
zinafanywa kwa vizazi na vizazi, na zinaleta mafanikio kwa wengi
Kwa mtu
ambaye ameamua kufanya biashara hizi na akabobea kweli, ni ngumu sana kuweza
kumtoa kwa sababu zinalipa, labda wewe mwenyewe uamue kwamba sasa siwezi
kuifanya tena biashara hii, ukaamua kukaa kwa kubweteka.
Lakini
biashara ambazo nakwenda kukushirikisha hapo ni biashara ambazo zinafanyika
katika mazingira yoyote yale. Zinafanyika kijijini na zinafanyika mjini, lakini
ni biashara ambazo hazichagui kitu ilimradi tu wewe uamue kufanya kwa ufanisi
na utafanikiwa.
Biashara
ambazo haziwezi kufa au hata kama zikifa ndio zitakuwa za mwisho ni biashara
za vyakula kama vile unga wa sembe, unga
wa ngano, mchele, mafuta ya kula, sukari, maharage, dagaa, pamoja na chumvi. Hizi ni biashara ambazo
zinadumu sana.
Ukiangalia
hivi ni vitu ambavyo vinagusa matumizi ya watu ya kila siku. Hakuna siku ambayo
itapita pasipo watu kufanya matumizi ya hivi vitu. Kila siku kwa mfano, unga
eidha uwe wa sembe au wa dona unahitajika sana kila siku.
Watu
wenye mashine au wanaojihusisha na biashara hii kwa mfano ya uuzaji wa unga
wanajua ni biashara ambayo haiwezi kudorola sana, ni biashara ambayo ipo wakati
wote, iwe njaa au kusiwe na njaa lazima watu wale.
Ni jukumu
lako wewe kuangalia kwa mfano ni kipindi gani mahindi yanapatikana kwa urahisi
na kusaga ili kupata unga huo na kuusambaza mtaani. Kuuza ni lazima utauza hata
bila kujali kama utauza kwa faida ndogo au kwa faida kubwa.
Mbali
na unga wa sembe ukiangalia upande mwingine maharage nayo, yanatumika sana
kwenye familia zetu karibu kila siku na uzuri wake yapo maeneo mengi ambayo
maharage haya yanapatikana kwa bei nafuu hususani hasa kipindi cha mavuno.
Unaweza
ukanunua na kuyauza moja kwa moja au ukasubiri kipindi yakiadimika ukaanza kuyauza
moja kwa moja na ikakusaidia kupata pesa. Uzuri soko lake liko wazi ukizingatia
familia nyingi, zinatumia maharage kila siku.
Hali
hiyo hiyo ndio inayoenda mpaka kwenye sukari, dagaa, mafuta ya kula,
halikadhalika na ngano. Ni biashara ambazo zinawalaji wengi. Na watu wengi
wametoka kupitia biashara hizo na kuwa na pesa nyingi sana.
Ukiwauliza
watu wenye maduka ya reja reja ambayo yanauza vitu mchanganyiko, watakwambia
vitu vinavyoendesha duka la reja reja au roho ya duka la reja reja ipo kwenye
hivyo vitu na ndivyo vyenye faida.
Kama
utaamua kufanya, kwa sababu pia wengi wanafanya, ni jukumu lako wewe kuingia na
kufanya kwa akili, au kuongeza kitu cha ziada ili ufanye kwa ufanisi ikiwa ni
kuanzia kwenye vifungashio na hilo litakusaidia kupata wateja wengi.
Kumbuka
sijasema kwamba biashara hizi hazina changamoto. Kila biashara ina changamoto
zake, lakini hata hivyo ni biashara ambazo walaji wake ni wengi na wanapatikana
kila siku.
Mpaka
hapo angalau umepata mwanga wa kile ambacho nilikuwa nataka kukuonyesha
biashara ambazo haziwezi kufa au hata kama zikifa zitachukua muda mrefu sana
kudondoka. Usichelewe kuchukua hatua, ndoto zako zinawezekana.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
.DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Feb 21, 2018
Huu Ndio Ukweli Kuhusu Maisha Ya Mafanikio Unaotakiwa Kuufahamu Vizuri.
IIi
kufikia mafanikio, kuna wakati inatakiwa uujue ukweli wa aina fulani hivi na
kwa kuujua ukweli huo utakusaidia kufanikiwa. Lakini kuendelea kuishi kwa
kujidanganya na huku ukiwa hujui mbele wala nyuma juu mafaniko utajidangaya tu,
hutafanikiwa.
Najua
utaweka juhudi hii au ile kufikia mafanikio, lakini hutaweza kufikia kwa sababu
utakuwa bado unaishi kwenye dunia ya giza ambayo inakuwa imekufunika na
ushindwe kutafuta mafanikio yako kama inavyotakiwa iwe kwako.
Kupitia
makala hii ya leo, tunakuangazia kweli tano ambazo unatakiwa uzijue na ili zikusaidie
kufanikiwa. Ni matumaini yangu, utafaidika vya kutosha na kuweza kubadilisha
maisha yako kwa kufanyia kazi kweli hizi. Kweli hizi ni zipi, karibu ujifunze.
1. Ni kazi ngumu kufikia mafanikio.
Asije
akakudanganya mtu kwamba kufikia mafanikio ni kazi rahisi, huyo atakuwa ni mtu
mwongo kabisa. kufikia mafanikio inahitaji uweke juhudi na maarifa ya kutosha
ili kufikia mafanikio hayo. Kama huweki juhudi huwezi kufanikiwa.
Kwa
lugha nyepesi tu bila kukuficha kitu naomba nikwambie kufikia mafanikio ni kazi
ngumu na sio nyepesi kama wengine wanavyowezza wakawa labda wanakudanganya
kwamba ni kitu rahisi tu na cha mara moja.
Lakini
hata hivyo haimaanishi kwa kuwa ni kazi ngumu kufika mafanikio, basi
haiwezekeni kuyafikia. Kufikia mafanikio ni kweli ni kazi ngumu, lakini
inawezekana kuyafikia kwa asilimia zote na hilo halina ubishi. Huu ni ukweli
unaotakiwa uumeze kama ulivyo bila kutema.
2. Unahitaji msaada kufikia mafanikio.
Hakuna
mafanikio ambayo unaweza ukayapata ukiwa wewe kama wewe. Unahitai msaada ili kuweza
kufikia mafanikio yako. Pasipo kuweza kupata msaada huwezi kupata mafanikio
yoyote, kwani mafanikio yapo kwa watu.
Kwa
hiyo utaona unahitaji msaada kutoka kwa rafiki zako, utahitaji msaada kutoka
kwa ndugu zako wa karibu na hata pia utahitaji msaada kutoka kwa wale watu wanaokusaidia
kazi zako na ambao wanakuwa wana mchango fulani kwako.
Huhitaji
hapa kutunisha kifua kusema mimi ndio mimi, mafanikio ni muunganiko wa misaada
tofauti tofauti kutoka kwa watu wengine pia. Ukweli huu unatakiwa kuujua kwamba
mafaniko yanahitaji msaada wa wengine pia, hivyo heshimu watu.
3. Makosa ni ngazi ya kufikia mafanikio.
Imezoeleka
kati ya kitu kinachowaangusha wengi katika safari ya mafanikio ni yale makosa
ambayo wanakuwa wanayafanya wakati wanatafuta mafanikio yao. Watu hao wamekuwa
wakisahau kwamba makosa ni kama shule.
Unapokuwa
unatafuta mafanikio ya aina fulani, kukosea ni kitu cha kawaida sana. Kwa hiyo
hutakiwi kujilaumu kwa chochote kwamba kwa nini umekosea katika eneo la aina
fulani, badala yake unatakiwa ujifunze kusonga mbele.
Utakwama
sana kwenye maisha yako, kama makosa utakuwa unayachukulia kwa umakini sana na inakupelekea mpaka kushindwa
kufanya vitu vingine. Yafanye makosa yawe shule yako ya kukuwezesha wewe kuweza
kusonga mbele zaidi na si kukurudisha nyuma.
4. Kuwa king’ang’anizi.
Sifa
mojawapo kubwa ya watu ambao wamefanikiwa ni wabishi. Ni watu ambao hawakubali
kushindwa kirahisi, ni watu ambao wanaamua liwalo na liwe, lakini wanapigana
mpaka kuhakikisha ndoto zao zinaweza kutimia.
Hata
wewe ili uweze kufanikiwa unatakiwa uwe king’ang’anizi sana. Kwa kifupi
unatakiwa uwe na roho ngumu, roho ambayo haikubali kushindwa kirahisi, inayotaka
lazima mabadiliko yaweze kutokea kwenye maisha yako.
Ukiujua
vyema ukweli huu kwamba unatakiwa kuwa mbishi hilo litakusaidia sana kuweza
kuweza kung’ang’ana kufanya kila linalowezekana na kuongeza juhudi zote kwa
kufanya kila kilicho cha msingi, ilimradi tu ufanikiwe.
5. Jipe hamasa ya mafanikio kila siku.
Usifanye
kosa la kusubiri hali au kitu chochote kikupe hamasa ya kufanya kile unachotaka
kufanya. Jipe hamasa hiyo wewe mwenyewe kila siku. Kama huoni hamasa ikitokea
usitulie, wewe endelea kufanya, hamasa itakuja mbele ya safari wakati
unaendelea.
Washindi
katika mafanikio hawasubiri hamasa ili kuweza kusonga mbele. Ni watu wa kufanya
na mwisho wa siku hamasa inayofuata. Kwa hiyo hata wewe unaweza ukaanza kujihamasisha
wewe mwenyewe.
Hakikisha
unafanyia kazi kweli hizi muhimu kwako na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako
zinatumia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097
na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Feb 20, 2018
Usitegemee Kufanikiwa Kama Hautafanya Jambo Hili Mapema.
Kufanya
maandalizi ya kitu chochote kile ni jambo la muhimu sana kwako na pia ni moja
ya dalili nzuri kwamba unajiandaa kuwa mshindi kwa kitu hicho unachokifanya. Kama
haufanyi maandalizi ni rahisi tu kushindwa na hilo halina ubishi.
Ndio
maana unaona mwanafunzi ni lazima ajiandae mapema ili aweze kufaulu mtihani
wake, ndio maana unaona mkulima anaandaa shamba lake mapema pia ili wakati wa
kilimo ukifika ili aweze kufanikisha kilimo chake.
Hiyo
haitoshi unaona pia, mwana riadha anaanza kufanya mazoezi mapema ya kukimbia ili wakati ukifika aweze kushinda
mbio hizo, hiyo yote inaonyesha maandalizi ni kitu cha muhimu sana kwa ushindi
wowote ule.
Hakuna
mshindi anayetokea au kuibuka tu kiholela pasipo kuwa na maandalizi yale ya mwanzo
ya kuweza kujifua haswaa ili kutengeneza ushindi huo. Kila ushindi unaouona
umetokezea kwa nje, ujue kabisa ushindi huo umeandaliwa na haujaja kwa bahati.
Unapaswa
ukumbuke pia hata wakati ule wa Nuhu. haikuwa kipindi cha mvua au gharika
wakati Nuhu anajenga safina, bali Nuhu alifanya maandalizi ya mapema na gharika
inayokuja mbele yake na hilo kweli lilikuja kutokea.
Halikadhalika
na wewe unatakiwa kujenga maisha yako kwa ubora sana kipindi ambacho mambo yako
hayajaanza kuharibika au mambo hayajaanza kubanana na mpaka ukasombwa na
gharika ya changamoto.
Unatakiwa
kujua kwamba wakati wa kutengeneza maisha yako ni sasa wakati bado una nguvu za
kutosha ni si baadae. Huu ndio wakati wa kutengeneza safina ya maisha wakati
hali, nguvu na muda wako bado vinakuruhusu.
Kitafika
kipindi ambacho hautakuwa na uwezo huo yaani muda utakuwa huna, na wala nguvu
utakuwa huna. Angalia sana usije ukaanza kulia kama wale watu waliokuwa
wakimlilia Nuhu wafungulie kwenye safina, lakini akawaambia hakufunga yeye
mlango.
Hata
wewe angalia usije ukafika muda ambao utaanza kuwalilia watoto wako, ukaanza kuwalilia
wajukuu wako wakati utakapoanza kusombwa na maji na ukiangalia ulishindwa
kujenga safina yako mapema. Wakati wa kufanya na kukazana ni sasa na si kesho.
Kwa nini
usubiri mabaya ya kukute ili upambane nayo wakati una uwezo wa kujindaa sasa
mapema na kuyaepuka. Huhitaji kusubiri kitu, unahitaji kufanya kitu kwa ajili
ya maisha yako ya kesho bila kujali hli uliyonao kwa sasa ni ipi.
Hebu
nikuulize kitu, kama utashindwa kutengeneza maisha yako sasa na yakaonekana yana
maana, je, utaweza kweli ukishazeeka. Hapo ulipo ni kijana umeshindwa je,
ikifika uzeeni utaweza? najua hutaweza hata ufanyaje.
Ndio
maana unatakiwa kuweka juhudi sana za kuhakikisha unafanya kila kinachowezekana
wakati bado damu yako ina chemka, wakati bado una nguvu ili ufanikiwe. Nikwambie
tu ukisubiri, jiandae kusombwa na gharika ya changamoto za maisha.
Na ubaya
wa gharika inakuwa haina msamaha au hakuna kupona, ikikukuta ujue ndio tayari
umeshaenda. Kwa hiyo usikubali kupoteza maisha yako ya mafanikio kwa sababu ya
kushindwa kufanya maandalizi mapema.
Kuanzia
sasa fanya maandalizi mapema kwa kila kitu ambacho unachokifanya. Usipofanya maandalizi
mapema utaanguka na utajiangusha wewe mwenyewe na kutakuwa hakuna mtu ambaye
ataweza kukuamsha tena.
Ndiyo
maana, unatakiwa uweke akiba mapema kipindi ambacho kabla hujaishiwa. Unatakiwa
uzime moto mapema, kabla moto haujawaka vya kutosha. Ni muhimu kufanya
maandalizi mapema ya chochote kile ukifanyacho ili ikusaidie kuwa mashindi.
Kama
hautafanya maandalizi ya mapema kwa chochote unachokifanya kushindwa hautaweza
kukwepa hata kidogo. Kumbuka hata Nuhu alijenga safina mapema, kabla hata
gharika haijafika. Tafakari na chukua hatua.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)