google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 4, 2017

Falsafa Bora Ya Fedha Unayotakiwa Kuitumia Kila Wakati…Ili Kufanikiwa.

No comments :
Ili kufanikiwa kifedha,  ipo falsafa ya mafanikio ambayo inatumika kuwaongoza watu na hadi kufikia mafanikio hayo makubwa sana ya kifedha. Falsafa hiyo ndiyo inayopelekea wengine wakawa na pesa na wengine wakawa hawana, wengine wakawa matajiri na wengine wakawa maskini.
Kwa mfano, falsafa kubwa ya watu wenye mafanikio hasa linapokuja suala la pesa, ukilinganisha na wale ambao hawajafanikiwa iko hivi; watu wenye mafanikio falsafa yao ipo kwenye kuwekeza kila aina ya pesa wanayoipata hata iwe ndogo vipi.  Na kile kiasi kidogo kinachobakia hukitumia katika katika matumizi ya kawaida, lakini mara baada ya kuwekeza.
Wakati watu ambao hawajafanikiwa nao pia falsafa yao ya pesa ni kutumia kila pesa wanayoipata na kiasi kidogo kinachobakia hicho ndio huanza kujaribu kuwekeza. Watu wasio na mafanikio, matumizi ndio kipau mbele cha kwanza kabisa kabla ya uwekezaji wowote ule.

Bila kujali shida zetu tulizonazo, changamoto mbalimbali, Ili kufanikiwa unatakiwa kujiwekea falsafa ya pesa kama wanavyofanya matajiri, ni lazima uanze kuwekeza kwanza hata kwa pesa kidogo, halafu matumizi yatafuata, kinyume cha hapo utakwama sana na utashindwa kufikia uhuru wa kipesa.
 Je, unavyofikiri kwa falsafa hizo mbili, je, hali ya maisha inaweza ikawa sawa kwa watu hao wawili kutokana na matumizi ya hizo falsafa? Najua majibu mpaka hapo unayo kwamba falsafa ipi ni sahihi. Kama utatumia falsafa ya pesa ya watu wasiofanikiwa, tambua utakuwa hivyo na ukitumia falsafa ya pesa ya watu wenye mafanikio, utafanikiwa pia.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.

TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.

Ni wako rafiki,

IMANI NGWANGWALU,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.