Jun 29, 2015
Kama Unataka Kuishi Maisha Ya Furaha Na Mafanikio? Hakikisha Unafanya Uchaguzi Huu Katika Maisha Yako.
Maisha
uliyonayo yanaweza yakawa mazuri sana ama mabaya kutokana na aina ya uchaguzi
unaofanya juu ya maisha yako kila siku. Mara nyingi uchaguzi tunaofanya katika
maisha yetu ndiyo huwa unaamua zaidi maisha yetu yaweje. Kama uchaguzi
unaofanya ni mbaya, ni wazi maisha yako yatakuwa mabaya na kama uchaguzi wako
ni mzuri basi maisha yako yatakuwa mazuri hivyohivyo hakuna atakayezuia hilo.
Kwa
kuwa uchaguzi wowote tunaofanya katika maisha yetu unakuwa una athari ni vizuri
tukawa makini kidogo na uchaguzi wa mambo tunayofanya kila siku. Nikiwa na
maana kuwa inatakiwa tujue kama kuna jambo tunalifanya ni muhimu kutambua lina
athari zipi kwetu. Kama tumeamua kufanya kitu fulani tuanze kwa kutafakari
matokeo yake kwanza. Hivyo ndivo tunavyotakiwa kufanya ili kuwa na uchaguzi
sahihi katika maisha yetu.
Kwa
uchaguzi sahihi tutazidi kufanya maisha yetu kuwa bora siku hadi siku.
Ikumbukwe pia kila kunapokucha tunanya aina nyingi sana za chaguzi ambazo
zinaamua hatima ya maisha yetu. Mara nyingi huwa ni watu wa kuchagua mavazi,
nguo za kuvaa, njia na mambo mengineyo mengi. Sasa ikiwa tunachagua mambo haya,
kwanini tusiwe na uchaguzi juu ya maisha yetu? Je, unajua ni aina gani ya
uchaguzi sahihi tunaotakiwa kuufanya katika maisha yetu ili kufanikiwa zaidi?
1. Chagua kuishi sasa.
Hii
ndiyo siri ya wewe kuweza kufurahia maisha yako. Hautaweza kufurahia maisha
yako na kuyaona katika uzuri wake halisi ikiwa unaishi kwa fikra sana za siku ziliyopita
ama siku za nyuma zaidi. Kwa kuishi kwako sasa, kuishi kwa kutokuwa na hofu
sana juu ya kesho yako, hapo utakuwa unafanya uchaguzi sahihi utakao weza
kubadilisha maisha yako na kuwa ya furaha na yenye mafanikio kwako pia.
2. Chagua kuishi maisha yasiyokuumiza.
Acha
kuishi maisha ya kuumiza utaumia sana. Ili kufanikwa kwa hili, jifunze kutokuyachukulia
mambo kwa ujumla ili usiweze kuumia zaidi. Ikiwa mtu atakwambia wewe ni mbaya,
hufai hiyo yote inaweza ikawa sawa kulingana na mtazamo wake. Hapo lakini wewe
usije ukachukulia huo ndiyo ukweli na kuanza kuumia na kujiona kweli hufai.
Fuata ukweli ulio ndani yako kuhusu wewe na siyo vinginevyo.
3. Chagua kuishi maisha ya ukarimu.
Haijalishi
mtu amekufanyia nini katika maisha yako kitu kikubwa cha kujifunza nikuwa
mkarimu kwa wetu wengine. Unapokuwa mkarimu unakuwa unaishi maisha ya utulivu
ambayo mara nyingi yanakuwa hayana msuguano zaidina wengine katika maisha yako.
Kwa kuishi maisha hayo yatakusaidia kukupa furaha na nguvu ya kufanikiwa. Hivi
ndivyo unavyotakiwa kuishi na kuwa hivyo.
4. Chagua kuishi kwa kufanya mambo yako
kwa uchache.
Ikiwa
utajifunza kumudu tabia hii basi utaweza kuishi maisha safi ya furaha ambayo
wewe mwenyewe utakuwa ni wazi unayafurahia kwa vyovyote vile iwavyo. Jifunze katika
maisha yako kuongea kidogo na kuwa msikilizaji sana. Jifunze pia kula chakula
kiasi ili kukujengea afya bora zaidi. Mambo mengi jaribu kuyafanya kwa kiasi
hiyo itakuwa ni siri mojawapo ya kuweza kukupeleka kwenye mafanikio.
5. Chagua kufanya mambo mapya.
Hautaweza
kufanikiwa kama utakuwa unafanya mambo yaleyale siku zote. Ili kuweza
kufanikiwa unalazimika kuchagua kufanya mambo mapya ambayo hujayazoea. Katika
kufanya mambo mapya ni lazima kujitoa mhanga na kukabiliana na kila aina ya
changamoto ili kuweza kufanikiwa, vinginevyo itakuwa ni ngumu sana kuweza kumudu
kuleta mafanikio tunayoyataka katika maisha yetu.
Tunakutakia kila la
kheri katika safari yako ya mafanikio na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO
kwa kujifunza na kuhamasika zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA
MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Jun 27, 2015
Kilimo Bora Cha Bilinganya.
Bilinganya imo
katika jamii ya
mimea inayohusisha nyanya,
pilipili, viazi mviringo
na nyanya mshumaa.
Mboga hii ina
viini lishe muhimu kama
vile madini aina
ya chokaa na
chuma, Vitamini A,
B na C,
wanga, protini na
maji. Mboga hii
hutumika kutengeneza supu
au kama kiungo
katika vyakula mbalimbali.
Vilevile huweza
kuhifadhiwa kwa kukatakata
vipande na kuwekwa
kwenye makopo.
MAZINGIRA:
Zao hili huhitaji hali
ya joto la wastani,
udongo wenye kina
kirefu na rutuba
ya kutosha na
usiotuamisha maji. Kwa
kawaida bilinganya hulimwa
zaidi ya msimu
mmoja, lakini katika
nchi za Kitropiki
(joto) zao hili
hulimwa kwa msimu
mmoja.
AINA:
Aina za
bilinganya zinazolimwa kwa
wingi katika nchi
za ukanda wa
joto ni kama
zifuatazo;-
·
Black Beauty:
Aina hii
huzaa sana, matunda
yake meusi, makubwa,
na ya mviringo
·
Florida Market.
Matunda ya
Florida Market yana
umbo la yai.
Aina hii pia
huzaa sana, lakini
hushambuliwa kwa urahisi
na ugonjwa wa mnyauko bakiteria
(Bacterial wilt)
·
Florida High
Bush.
Matunda yake
ni makubwa yenye
umbo la yai
na rangi ya
kijani kibichi iliyochanganyika na
nyeusi.
·
Newyork
Spineless.
Matunda ya
Newyork Spineless ni
ya mviringo, makubwa
na yana rangi
ya ya zambarau.
·
Peredeniya.
Aina hii
huzaa sana, matunda
yake ni makubwa
kiasi na yana
umbo la yai.
Aina zingine
za bilinganya ni
matale, Kopek na
Rosita. Aina hizi huvumilia
sana mashambulizi ya
ugonjwa wa mnyauko
bacteria.
KUOTESHA MBEGU:
Mbegu huoteshwa kwanza
kwenye kitalu na
baadaye miche huhamishiwa shambani. Kabla
ya kusia mbegu,
tengeneza tuta lenye
upana wa mita moja
na urefu wowote. Weka mbolea
za asili kama
vile samadi au
takataka zilizooza vizuri,
kiasi cha ndoo
moja au mbili
katika eneo la
mita mraba moja.
Sia mbegu kiasi
cha gramu mbili
mpaka tatu (nusu kijiko
cha chai chenye
ujazo wa gramu
tano) katika eneo
hilo.
Gramu 500
za mbegu zinatosha
kupandikiza katika eneo
la hekta moja.
Nafasi kati ya
mstari na mstari
iwe sentimeta 10
hadi 15 na
kina kiwe sentimita
1.5. Baada ya
kusia mbegu fukia
na tandaza nyasi
kavu na kisha
mwagilia maji. Endelea kumwagilia
kitalu kila siku,
asubuhi na jioni,
hadi mbegu zitakapoota. Mbegu
huota baada ya
siku ya 10 hadi 12.
KUHAMISHA MICHE:
Miche huwa
tayari kwa kupandikizwa
shambani baada ya
wiki sita hadi
nane. Wakati huu
huwa na urefu wa
sentimita 15 mpaka
20 (sawa na
urefu wa kalamu
ya risasi).
Mwezi mmoja
kabla kupanda miche, rutubisha
udongo kwa kuweka
mbolea za asili
zilizooza vizuri. Mbolea
hizi ni kama
samadi, mbolea vunde
na mbolea ya
kuku.
Weka kiasi
cha tani 10
hadi 20 kwa
hekta. Kiasi hiki ni sawa
na kuweka ndoo
moja hadi mbili
zenye ujazo wa lita
20 katika eneo
la mita mraba
moja. Mbolea ya
mchanganyiko aina ya
N.P.K yenye uwiano
wa 20:10:10 huwekwa
kwenye shimo wakati
wa kupandikiza mche.
Kiasi kinachohitajika ni
gramu tatu hadi
tano (sawa na
nusu kijiko mpaka
kijiko kimoja kidogo
cha chai) kwa
kila shimo.
Nafasi ya
kupandikiza hutegemea aina
ya bilinganya. Aina ndogo
hupandikizwa katika nafasi
ya sentimita 80
mpaka 100 kutoka mstari hadi
mstari na sentimita
50 mpaka 60
kutoka mche hadi
mche. Aina kubwa
hupandikizwa katika nafasi
nafasi ya sentimita
80 mpaka 100
kutoka mstari hadi
mstari na sentimita 80
mpaka 90 kutoka mche
hadi mche. Kazi
ya kuhamisha miche
ifanyike kwa uangalifu
mkubwa ili kuepuka
kuikata mizizi.
KUTUNZA SHAMBA:
·
Kuweka
matandazo.
Mara baada
ya kupandikiza miche,
tandaza nyasi
kavu. Matandazo husaidia
kuhifadhi unyevu, huzuia
magugu yasiote na
huongeza rutuba ya
udongo.
·
Palizi.
Hakikisha shamba
ni safi wakati
wote ili kuzuia
ushindani wa chakula,
maji na mwanga
kati ya mimea
na magugu. Usafi
wa shamba pia
huondoa maficho ya
wadudu waharibifu na
huzuia kuenea kwa
magonjwa.
·
Mbolea.
Mbolea ya
kukuzia aina ya
S/A huwekwa wiki
tatu baada ya
mmea kuanza kutoa
maua. Kiasi cha
gramu tatu hadi
tano kuwekwa kuzungukia kila
mche. Mbolea iwekwe
katika umbali wa
sentimita tano mpaka
15 kutoka kwenye
shina, hutegemea ukubwa
wa mche. Hakikisha
mbolea haigusi mmea.
·
Kukata kilele.
Wiki mbili
baada ya kupandikiza miche,
kata sehemu ya
juu ya mmea (kilele)
kama umepanda aina
ndefu ya bilinganya.
Hii itasaidia kupata
matawi matatu hadi
manne na mmea
kutengeneza kupata matawi
matatu hadi manne
na mmmea kutengeneza
umbile la kichaka.
Matawi yakizidi manne
yaondolewe ili kupata mazao
mengi na bora.
·
Kumwagilia.
Zao la
bilinganya hustawi vizuri
likipata maji ya
kutosha. Umwagiliaji ufanyike
kila siku asubuhi
na jioni kutegemea
hali ya hewa.
Kuzuia Wadudu
Waharibifu na Magonjwa.
Wadudu Waharibifu:
·
Vivyatomvu wa
Bilinganya (Eggplant Lacebugs)
Wadudu hawa
hushambulia zaidi
sehemu ya chini
ya jani. Hufyonza
utomvu wa majani na
kusababisha majani kuwa
na mabaka meupe
au njano. Mashambulizi yakizidi
majani huanguka chini.
Vinyatomvu wanaweza kuzuiwa
kwa kunyunyizia moja
ya dawa zifuatazo;-
Deltamethrin (Decis), Dimethoate (Sapa
Dimethoate) Fenvalerate
(Sumicidin), Lambda -
Cyhalothrin (Karate).
·
Vidukari au
wadudu mafuta (Cotton
Aphids)
Hawa ni
wadudu wadogo wenye
rangi nyeusi. Hushambulia majani
machanga na kuyasababisha kudumaa
na kukunjamana. Zuia
wadudu hawa kwa
kutumia mojawapo ya
dawa zifuatazo;-
Dimocron 50%
E.C, Lambda - Cyhalothrin
(Karate) Dichlorvos (Nogos).
·
Utiriri wa
Mimea (Red Spider
Mites).
Ni vidudu
vidogo vyenye rangi
nyekundu iliyoiva.
Hushambulia majani kwa
kufyonza utomvu. Majani
yaliyoshambuliwa huonyesha utando
kama wa buibui.
Mashambulizi yakizidi mea
hudumaa, majani hukauka
na hatimaye hufa.
Utiriri unazuiwa
kwa kutumia dawa
zifuatazo;- Acrex, Karathane 25% W.P,
Dimethoate, Ekalux, Kelthane.
·
Minyoo Fundo
(Root knotnematodes).
Wadudu hawa
hushambulia mizizi. Hutoa
kinyesi ambacho ni
sumu kwa mmea.
Sumu hii husababisha
mizizi kuwa na
nundu kama ya
mizizi ya maharagwe.
Mashambulizi yakizidi mmea
hudumaa, hunyauka na
hatimaye hufa.
Njia ya
kuzuia wadudu hawa
ni kubadilisha mazao
kwa mfano baada
ya kuvuna zao
hili, zao linalofuata
lisiwe la jamii
moja na bilinganya
kama vile nyanya,
pilipili na viazi
mviringo. Pia dawa
aina ya Carbofuran
(Furadan) inaweza kutumika.
Magonjwa:
·
Mnyauko Bakteria
( Bacterial Wilt).
Ugonjwa huu
husababishwa na backteria.
Mmea ulioshambuliwa hunyauka
ghafla hasa wakati
wa jua kali.
Mnyauko bacteria
unaweza kuziuwa kwa
kubadilisha mazao shambani.
Endapo ardhi itashambuliwa na
ugonjwa huu zao
la bilinganya lisipandwe
katika eneo hilo
kwa muda wa
miaka mitatu hadi
mitano.
Njia nyingine
ni kupanda aina
za bilinganya kama
vile Matale, Kopek
na Rosita ambazo
huvumilia mashambulizi ya
ugonjwa huu.
·
Phomopsis Vexans:
Ugonjwa huu
husababishwa na bacteria
na kushambulia majani,
shina na matunda.
·
Verticillium Wilt.
Huenezwa na
maji na husababisha mmea
kudumaa, majani kukunjamana
na kuanguka.
Magonjwa ya
Phomopsis vexans na
Verticillium Wilt yanaweza
kuzuiwa kwa kung’oa
ma kuchoma moto
mimea iliyoshambuliwa, kubadilisha
mazao, na kuweka
shamba katika hali
ya usafi wakati
wote.
KUVUNA:
Bilinganya huanza
kutoa matunda yaliyokomaa
baada ya miezi
miwili hadi mitatu
tangu kupandikiza. Uvunaji
huendelea kwa muda
wa zaidi ya
miezi minne na
hauna budi ufanyike
mapema mara matunda
yanapokomaa. Matunda yaliyokomaa sana
hayafai kulimwa kwa
sababu huwa na
kambakamba na mbegu
zilizokomaa.
Vuna mara
mbili au tatu
kwa wiki, kwa
kutumia kisu kikali
ili usiumize matunda.
MAVUNO:
Kwa kawaida
zao hili huzaa
sana iwapo limetunzwa
vizuri. Shamba lililotunzwa vizuri
linaweza kutoa mavuno
tani 50 hadi
60 kwa hekta.
Hata hivyo mavuno
mengi hutegemea aina
ya bilinganya, umwagiliaji na
rutuba ya udongo.
§ MAKALA HII IMEANDALIWA NA SAID MALOGO,
MTAALAMU WA MASUALA YA KILIMO.
Jun 26, 2015
Hizi Ndizo Athari Za Kuwa Na Maumivu Makali Kihisia.
Nakumbuka ni hivi karibuni
ambapo ilikuwa ni majira ya jioni na
nilirudi nyumbani tofauti na kawaida yangu. Siku hiyo niliamua kupitia jikoni
kama kituo change cha kwanza. Nilipoingia jikoni nilimwona binti ambaye huwa
tunakaa naye akiwa ameinamia kwenye beseni la kuoshea vyombo
hapo jikoni.
Nilimsemesha na aligeuka
kuniangalia bila kunijibu chochote. Mikono yake alikuwa ameiweka ndani ya
beseni kama kuficha kitu lakini hata nilipomwangalia nilihisi kama alikuwa
analia hivi. Nilipomsogelea na kutazama mikono yake, nilipatwa na mshtuko sana.
Alikuwa ameshika kisu na mkono wake wa kushoto ulikuwa ukitoka damu. Ilionesha
alikuwa amejikata.
Nilipomuuliza ni kwa nini
anafanya vile huku nikiwa nimetundikiwa, alinitazama tu huku machozi yakimtoka.
Siyo siri niliogopa sana. Baada ya tukio lile niliamua kumuulizia daktari kwa
ufafanuzi zaidi alionipa ndipo nilipojua
hasa kuhusu jambo lile ambalo lilipelekea binti yule kuweza kujiumiza.
Ilinibidi kwa kweli,
nimpeleke hospitali na tatizo nililokuja kuambiwa na daktri ni tatizizo linalotokana hasa na mtu kukata tamaa, kuchangiwa
na kuamua kujiadhibu kwa kujiumiza. Bila shaka tunajua kwamba, kukata tamaa
kunapozidi na mtu anapohisi kuwa maisha hayana maana, anaweza kujiuwa.
Nilijifunza yote hayo kutokana na tatizo alilokuwa nalo binti
yangu huyu. Kujiumiza huku kunaweza kuwa ni kwa kujikata mikono, miguu au
sehemu nyingine ya mwili. Wakati mwingine inaweza kuwa kwa kuvuta nywele ,
ung’ata kucha kwa nguvu, kujipiga au kujichubua au kukwaruza hata kidond
ambacho hata kilikuwa karibu kupona.
Ingawa siyo tatizo kubwa ,
kwani inakadiriwa ni mtu mmoja tu kila
mia moja anakabiliwa nalo, bado hii ni idadi kubwa ya kutosha. Ina maana kwaba
kwa hapa nchini kiasi cha watu 440,000 wanakabiliwa na tatizo hilo.
Pamoja na ukubwa wa tatizo
hilo kwa bahati mbaya hakuna mtaalamu ambaye hadi sasa amewahi kusema kwa hakika tatizo hilo linatokana na nini
hasa. Lakini angalau inafahamika kwamba ni juhudi ya anayejiadhibu kutaka
kujihisi ahueni ya kimaisha angalau kwa muda fulani.
Bila shaka tumewahi
kushuhudia au kusikia kuhusu watu wanaojikwangua, wanaojiumiza, wanaojibamiza
ukutani, wanaopanda mitini na kujiangusha ili wavunjike kwa kuamini kuwa
wanapata ahueni kwa kufanya hivyo. Kama tumewahi kushudia au kusikia, hii yote
ni sehemu ya tatizo hili.
Mara nyingi kujiadhibu huku
hufanywa kwa siri sana na wahusika. Kwa hiyo wakati mwingine inakuwa vigumu
kuona kuwa anajiadhibu, bali tunaweza
kuona matokeo yake. Mtu anaweza kuona kidonda kipya kwenye mwili wa mtu au
kuona nywele zimevurugwavurugwa ghafla tu ama dalili nyinginezo.
Kwa bahati mbaya, hawa watu
wanaojiumiza wenyewe, ni mara nyingi huwa hawajui ni kwanini wanajiumiza,
hujiumiza kwa sababu huhisi wakifanya hivyo watapata nafuu. Lakini nafuu ya
nini, huwa ni swali gumu kupatiwa majibu.
Bado hata hivyo, ukweli
unabaki kwamba, wanafanya hivyo kwa sababu wana maumivi kihisia. Kwa hali hiyo,
kama inatokea mtu anagundua kwamba, jamaa yake ameingia mahali ambapo anajiumiza
mwenyewe kwa njia yoyote, inabidi ajaribu kumsaidia akijua ni tatizo la
kihisia.
Nimeshawahi kusikia kuhusu
watu amao wamepelekwa kwa waganga wa asili kwa sababu ya tatizo hili. Kufika
huko wakaambiwa wana wana jini anatafuta damu na kuanza kutibiwa kwa kutaka
kumtoa jini huyo, hali ambayo iliwazidishia maumivu kihisia hadi wakaamua
kujiua. Kumbe ambacho hawakujua kujiumiza huko siyo majini wala nini bali hizo
ndizo athari za kuwa na maumivu makali ya kihisia.
Tatizo la mtu kujiumiza
mwenyewe kwa lengo la kupata nafuu, halihusiani na kulongwa au nguvu nyingine
za giza. Ni tatizo ambalo kisaikolojia linaelezeka kabisa. Ingekuwa
halijanipata, ningeweza kusema, huenda lina nguvu za giza ndani yake kama wengi
wanavyofikiri. Lakini nimelishuhudia moja kwa moja na nalijua vizuri.
Tunakutakia kila la kheri,
endelea kujifunza kila siku bila kuchoka kwa kupitia mtandao huu wa DIRA YAMAFANIKIO lakini hakikisha unawashirikisha wengine ili kuweza kujifunza zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Jun 25, 2015
Sababu 10 Zinazofanya Biashara Nyingi Mpya Zishindwe Kuendelea.
Mara nyingi huwa inakadiriwa
kuwa biashara nyingi mpya zinazoanzishwa, huwa zinajikuta zinakufa kabla hazijafikia miaka mitano na
chache huwa ndio zinazoendelea baada ya hapo. Kufa huku kwa biashara hizi huwa
hakuji kwa bahati mbaya, bali huwa kunatokana na sababu kadhaa ambazo pengine
huwa zinatokana na wajasiriamali wenyewe au nje ya wajasiriamali. Ni muhimu
kujua sababu zinazopelekea biashara nyingi zife kabla hazijafikisha miaka
mitano, ili kama upo kwenye mchakato wa kuanzisha biashara ama upo kwenye
biashara usije ukafanya makosa hayo na kujikuta umeua biashara yako.
Hizi
Ndizo Sababu 10 Zinazofanya Biashara
Nyingi Mpya Zishindwe Kuendelea.
1.
Usimamizi mbovu.
Hili ndilo kosa kubwa huwa
linafanyika kwa biashara nyingi na matokeo yake ni kuwa ni biashara za kawaida
ambazo hazina mafanikio makubwa sana na mwisho wa siku kufa kabisa.
Kunapokosekana usimamizi mzuri na wa kutosha, mara nyingi biashara huanza
kujiendea kiholela ama kwa mazoea ya kawaida tu, kitu ambacho ni hatari sana
kwa biashara. Ni muhimu kwa biashara ikawa na usimamizi mzuri na mipango
iliyotulia ili iweze kuleta faida na mafanikio makubwa, vinginevyo itakufa.
2.
Kukosekana kwa ung’ang’anizi.
Mara nyingi huwa inachukua
muda mrefu kidogo kwa biashara mpya, kuweza kukuletea faida kama ulivyokuwa
umepanga. Katika kipindi hiki huwa ni kipindi kigumu kwa wajasiriamali wengi,
kwani ni kipindi ambacho biashara huwa inajiendesha kwa faida kidogo sana na
uvumilivu wa hali ya juu huwa unahitajika. Hapa ndipo, biashara nyingi mpya
huwa zinakufa ama kushindwa kuleta mafanikio makubwa, kutokana na kukosekana
kwa ung’ang’anizi ambacho huwa ni kitu muhimu sana.
3.
Kuweka biashara katika eneo lisilo
sahihi.
Hii ni moja ya sababu muhimu
sana ambayo mara nyingi huwa inapelekea biashara nyingi mpya kufa. Unapoweka
biashara yako katika eneo lisilo sahihi, mara nyingi kitakachotokea utaanza
kukosa wateja na utajikuta unabaki kulaumu kuwa biashara hiyo hailipi au haifai
kumbe eneo uliloweka ndilo sio sahihi. Ili kuepuka hili, ni muhimu sana kuiweka
biashara yako katika eneo lililosahihi ambapo una uhakika unaweza kupata wateja,
ambao watasaidia kuifanya biashara yako kuwa hai.
4.
Biashara inakuwa haitatui matatizo mengi ya watu.
Lengo kuu la biashara sio
kupata faida pekee, bali ni pamoja na kutatua matatizo ya watu. Kwa jinsi
biashara inavyozidi kutatua matatizo mengi ya watu ndivyo inavyozidi kupata
wateja wengi na faida kuwa kubwa zaidi. Hakuna biashara yoyote duniani ambayo
imeendelea bila kutatua matatizo muhimu ya watu. Kama unataka kufanikiwa na
kupiga hatua kwa biashara unayofanya, ni
lazima biashara yako itatue matatizo ya watu kwa sehemu kubwa.
5.
Kushindwa kujifunza kutokana na makosa.
Ni ukweli usifiochika
wajasiriamali walio wengi huwa ni watu wa kufanya makosa katika biashara zao.
Lakini, pamoja na makosa hayo kitu pekee ambacho huwa kinawafanya wananyanyuka
na kusonga mbele ni kile kitendo cha kuchukua hatua ya kujifunza na
kujirekebisha kutokana na makosa hayo. Tatizo walilionalo wajasiriamali wapya,
huwa ni wazito kujifunza kutokana na makosa na kujikuta ni watu wa kurudia
makosa yale yale yanayopelekea kuua biashara zao.
6.Kukabiliwa
na ushindani mkubwa.
Biashara nyingi mpya huwa
zinashindwa kufanya vizuri sokoni kutokana na kukutana na ushindani wa hali ya
juu. Kunapokuwa kuna ushindani wa kisoko, halafu wewe ukiwa kama mjasiriamali
ukashindwa kusoma nyakati za jinsi gani unaweza kukabiliana hali hiyo, uwe na
uhakika biashara yako haiwezi kufanikiwa sana, zaidi baada ya muda itaanza
kupotea polepole na mwisho ni kufa kabisa.
7.
Kutokuwa na mtaji wa kutosha.
Kutokuwa na mtaji wa kutosha
katika biashara, hii pia huwa ni sababu mojawapo inayopelekea biashara nyingi
mpya kufa mapema. Mtaji huwa unahusika sana hasa pale unapohitaji kuongeza
pengine bidhaa ili kuweza kukabiliana na soko na wakati huohuo unakuwa hauna
pesa ya kutosha. Inapotekea hali hii ya kukosa mtaji wa kutosha kwa biashara
unayoifanya, hapo ndipo huwa mwanzo wa kushindwa kwenye ushindani na biashara
huanzia kuyumbia hapo na baadae kupelekea kufa, kama jitahidi nyingine za ziada
zisipofanyika.
8.
Kunafanya biashara na watu ambao sio sahihi.
Ili biashara yako iweze
kuleta mafanikio makubwa unayotaka, ni muhimu kwako kuwa na timu sahihi
utakayoshirikiana nayo kukuletea mafanikio. Kwa kawaida huwa hakuna mafanikio
makubwa ya mtu mmoja, ni vizuri ukashirikina na timu uliyonayo katika biashara
yako ili kuleta mafanikio makubwa. Inapokosekana timu ya uhakika katika
biashara, hii ndiyo huwa sababu mojawapo inayosabbisha biashara nyingi mpya
kufa.
9.
Mipangilio mibaya ya bei.
Mara nyingi biashara nyingi
zinazoanza huwa zinamipangilio sio mizuri ya bei kitu ambacho husababisha
kuwachanganya wateja. Hili huwa linatokea pengine kutokana na kupanga bei ya
bidhaa, pasipo kujali ama kuangalia ubora wa bidhaa husika, hali ambayo
husababisha wateja kuingiwa na shaka na kuanza kuhama kidogo kidogo, kitu
ambacho ni hatari sana kwa biashara kuweza kuendelea.
10.
Kukosa ushauri mzuri wa Kibiashara.
Mjasiriamali unapokosa
ushauri mzuri ambao ungewezakukusaidia kuifanya biashara yako ikawa hai,
kinachotokea hapo ni kuua biashara. Biashara nyingi huwa zinakufa kwa sababu ya
kupokea ushauri wa kila aina na kuufanyia kazi hata kwa watu ambao sio wazoefu
sana wa biashara husika. Kama unataka biashara yako iweze kusonga mbele na
kuleta matunda acha kupokea ushauri wa kila aina, vinginevyo utaua biashara
yako.
Mwisho, zipo sababu nyingi
zinazopolekea biashara nyingi mpya kutoweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa na
kupelekea nyingi kuweza kufa hata kabla ya kufikisha miaka mitano. Kwa kuanzia,
hizo ndizo baadhi ya sababu zinazofanya biashara nyingi kuweza kufa na
kushindwa kusonga mbele kabisa. Ni muhimu kuweza kujifunza na kuchukua hatua
zitakazotusaidia kuepuka makosa hayo na kuweza kufanikiwa.
Nakutakia ushindi katika
biashara yako iwe ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa elimu
na maarifa zaidi, yatakayoboresha maisha yako kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
- 0713 048 035,
- dirayamafanikio@gmail.com
- dirayamafanikio.blogspot.com
Jun 24, 2015
Nguzo Tatu Muhimu Za Mafanikio Ambazo Ni Lazima Uwe Nazo.
Umefika sasa wakati wa kila
mmoja wetu kutambua kuwa ana uwezo mkubwa wa kutumia vipaji vilivyo ndani mwake
kuweza kumletea mafanikio makubwa
maishani. Hii nikiwa na maana
kuwa inakulazimu kuweza kujua kuwa hiki kipindi tulichonacho sasa ni kipindi
cha maarifa ambayo kwa sehemu kubwa yanahusisha vipaji na ubunifu mkubwa zaidi
ili kuweza kufanikiwa.
Katika kipindi hiki mtu anayefanya
chochote kwa sababu yoyote hawezi kufika popote. Watakaoweza kumudu mashindano
ya dunia hii ya sasa, ambayo imefanywa kuwa ndogo zaidi, ni wale tu walio na
maaarifa maaalum na kwa sababu maalum na siyo tu maarifa. Ninasema hivi sio kwa
kukutisha na pia si maanishi uwe na elimu ya chuo kikuu ndiyo uwe na maarifa
haya, unaweza kuyapata hata kama hukwenda shule.
Kwa kulijua hilo kuwa tupo
kwenye dunia ya ushindani ambayo inatulazimisha kuwa na maarifa, vipaji na
ubunifu ni muhimu kwetu kujipanga ili kuhakikisha mambo hayo yote matatu tunayo
ili kuweza kujihakikishia kufanikiwa, kwani mambo hayo ni nguzo muhimu sana
kwetu sisi na kizazi kijacho ili kujenga taifa imara lililofanikiwa.
Pamoja na umuhimu wa
maarifa, ubunifu na vipaji katika suala zima la mafanikio yetu, lakini kwa
bahati mbaya wazazi wengi hapa nchini hawajui au hawajali sana kuhusu vipaji.
Hii hupelekea wazazi wengi kuweza kukandamiza vipaji vingi vya watoto wao bila
kujua kuwa wanaua vipaji hivi vya watoto.
Kuna wazazi ambao huwakataza
watoto wao wasiimbe kwa maelezo kwamba, kuimba ni ibilisi. Kuna wazazi wengine
huweza kuwavunja nguvu watoto wanacheza
mpira, kuchora na shughuli nyingine za kisanii kwa maelezo kwamba mambo hayo
huwapotezea muda wa masomo. Wasichokifahamu wazazi hao ni kwamba, huenda hivyo wanavyofanya watoto ndivyo vipaji vyao,
yaani ndiyo makusudi ya wao kuletwa hapa duniani.
Kwa watu wengi ikiwemo
wazazi kama ambavyo nawaongelea hapa wanapenda au wanataka watoto wao wawe ama
wafanye yale ambayo wao wazazi ndiyo wanayoyapenda bila kujali upendeleo na
uwezo wa watoto. Hali hiyo ndiyo ambayo inawafanya wasomi wengi wa nchi hii kwa
wasomi wa sifa na pato, badala ya kuwa wasomi wa ubunifu kwa faida ya jamii.
Kuna wasomi ambao hawakujua
tangu awali kwa nini wanasoma kile walichokisoma, kwa sababu hata uchaguzi wa
wasome kitu gani, ulifanywa na wazi wao, wakati mwingine, kwa kuwalazimisha.
Kuna vijana wengi wenye vipaji vikubwa ambao wameshindwa kuvitumia kabisa au kuvitumia
vizuri, kwa sababu vilikandamizwa utotoni.
Kama tulivyosema, umefika
muda sasa ambapo wazi wanapaswa kama siyo kulazimishwa na mazingira, kujua kwa
makusudi vipaji vya watoto wao ili waweze kuwasaidia kujenga kesho yenye
mkabala thabiti zaidi wa kimafanikio.
Mtoto anapoonesha kipaji fulani,
sisi wazazi tusikikandamize kwa sababu, hatukitaki. Anapoonyesha kipaji tumpe
moyo ili aweze kukiendeleza kwa faida
yake na ya kwa wengine. Kukandamiza vipaji vya watoto na kujaribu kuwaingizia
kile ambacho hakiko ndani mwao kwa hakika ni kuwaumiza bure tu.
Ifike
mahali na sisi tukubali kwamba, hata sisi huenda vipaji vyetu huenda vilikandamizwa au hatukuoneshwa
kwa namna nzuri ya kuvibaini na ndiyo maana pengine wengi wetu hatufurahii
shughuli tunazizifanya maishani mwetu. Kwa nini nasi tulee watoto ambao
watakuwa na utapiamulo wa ufahamu na matumizi ya vipaji.
Pia tutambue kuwa, tupo
kwenye kipindi cha zama za maarifa ni jukumu lako kutumia nguzo tatu hizo
muhimu kuweza kutufanikisha nikiwa na maana Maarifa, ubunifu na vipaji tulivyo navyo ili kufikia mafanikio
makubwa. Vitu hivi vikikaa pamoja na kufanyiwa kazi vinaleta matokeo makubwa na
ya kushangaza. Kwani hizo ndizo nguzo tatu muhimu za mafanikio kwako na kizazi
kijacho unazotakiwa kuzijua.
Tunakutakia kila la kheri,
endelea kujifunza kila siku bila kuchoka kwa kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO lakini hakikisha unawashirikisha wengine ili kuweza kujifunza zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Jun 23, 2015
Hii Ndiyo Siri Ya Mafanikio Iliyojificha Kwenye Kushindwa Kwako.
Kama kushindwa ingekuwa
ndiyo mwisho wa safari ya mafanikio basi leo hii kusingekuwa na mtu ambaye
angekuwa amefanikiwa. Kwa bahati nzuri sana dunia imejaa watu wengi ambao kabla
ya kufanikiwa kwao walishashindwa sana. Watu hawa hawakuweza kukata tama pale
waliposhindwa ila walichukulia kushindwa kwao kama fundisho na kuzidi kusonga
mbele.
Ukifatilia hili utagundua
kuwa watu wote wenye mafanikio makubwa hao ndio walikuwa washindwaji sana katika kile walichokuwa wakikifanya. Kwa
maana hiyo hakuna mtu ambaye amefanikiwa sana hakuwahi kushindwa kwa namna
yoyote ile. Unaweza kuthibitisha juu ya hili kwa kuangalia maisha ya Thomas
Edson. Katika maisha yake alikosea karibu mara 999 kabla hajaja na ugunduzi
rasmi wa balbu(glopu).
Kwa makosa aliyokuwa
akiyafanya Thomas Edson aliyachukulia kama fundisho na kuamua kusonga mbele.
Pengine leo hii dunia ingekuwa giza kama sio ubishi wa Edson kung’ang’ania
ugunduzi wake huo wa taa mpaka ukafanikiwa. Ipo siri kubwa sana katika kukosea
kwetu ambayo wengi wetu hawajui. Wengi hujikuta wanakatishwa tamaa sana na
makosa yao na kurudishwa nyuma.
Kwa vyovyote vile iwavyo
pale inapotokea umekosea usitoke mikono mitupu, jifunze kitu. Kwa kujifunza
itakusaidia kuweza kuendelea zaidi kwa ujasiri na mafanikio makubwa. Ni mara
ngapi umekuwa ukikosea na kukata tamaa, bila shaka ni mara nyingi. Kukosea
kwako mara mbili, tatu, au nne kusikukatishe tamaa, wapo waliokosea zaidi ya
mara elfu moja lakini walijirekebisha na kusonga mbele.
Nimekuandikia makala hii
kukutia moyo kuwa mafanikio katika maisha yako yapo na yanakusubiri hata kama
umeshindwa mara ngapi. Unachotakiwa kufanya ni kuwa mvumilivu kwa muda ili
kuyafikia. Kama nilivyoanza katika makala hii, watu wengi wenye mafanikio
walianza kwa kushindwa kwanza kisha wakafanikiwa. Hicho ndicho kitu
unachotakiwa kukifanya kwa sasa badala ya kujilaumu.
Ni muhimu kujua kuwa
kushindwa ama kukosea ni hatua nayo mojawapo katika safari ya mafanikio ingawa
hatua hiyo huja kwa kuumiza. Tukubali kujifunza pale tunapokosea kisha baada ya
hapo tusonge mbele na kuachana na tabia ya kulalamika. Kama unafikiri makosa na
kushindwa kumekurudisha nyuma sana, angalia maisha ya watu hawa na kisha
jifunze kitu na kuwasha moto wa mafanikio ndani yako.
1. Soichiro Honda, huyu
ndiye mwanzilishi wa kampunni kubwa ya
kutengeneza pikipiki aina ya Honda. Maisha yake kimafanikio yalianzia pale
ambapo alienda kuomba kazi katika kampuni ya utengenezaji wa magari aina ya
Toyota na kukataliwa sana kuwa alikuwa hafai na hawezi kitu chochote akatafute
kazi nyingine na sehemu nyingine.
Kwa Honda hilo
halikumkatisha tamaa, aliamini anaweza na anao uwezo mkubwa ndani yake
utakaomsaidia, ndipo akaamua kuanzisha kampuni yake ya Honda ambayo baadaye
ikaja kuwa kampuni kubwa ya magari duniani inayoshindana na kampuni ile ya
Toyota ambayo walimkataa mwanzo. Ikiwa kuna kitu cha kujifunza hapa kupitia
maisha ya Honda kamwe USIKATE TAMAA
kwa kile unachoamini kuwa kitakufanikisha.
2. Stephen king's, huyu
ni mwandishi maarufu wa vitabu lakini wengi hawajui alikotokea zaidi ya kuishia
kusoma vitabu vyake tu. Stephen King’s ni mwandishi pekee ambaye kitabu chake cha
kwanza kilikataliwa sana na kampuni nyingi za uchapishaji alikotaka kwenda kuchapisha
kwa kuambiwa kuwa hakifai. Hata hivyo
hakukata tamaa mpaka alipotimiza lengo lake.Kwa hiyo unakuja kuona kwa
vyovyote hata ukataliwevipi, unao uwezo wa kubadili matokeo na kufanikiwa ikiwa
unajiamini.
3. Oprah Winfrey's, katika maisha yake ya sasa huyu ni moja kati ya wanawake wenye pesa
nyingi sana duniani, mhamasishaji wa mafanikio na mwendeshaji wa vipindi vya
TV. Kwa kazi hiyo ya utangazaji imempa pesa nyingi sana kiasi kwamba naweza
kusema ni moja kati ya wanawake matajiri duniani na mwenye umaarufu mkubwa sana.
Hata hivyo pamoja na mafanikio hayo, Oprah Winfrey kabla hajafika hapo kituo
kimojawapo cha kwanza walichomwajiri walimfukuza kazi kwa madai kuwa hafai.
Hilo yeye halikuwa pigo alikaa chini na kuongeza juhudi hatimaye kufika juu
kwenye kilele cha mafanikio makubwa.
4. Bill gates, huyu ni mwanzilishi wa kampuni inajulikana sana duniani ya Microsoft ni
mmoja kati ya wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa sana dunia. Pamoja na hayo,
lakini je? unajua kwamba wazo lake la kutengeneza kompyuta ambayo ingekuwa inatumia
‘mouse’ lilikataliwa kabisa katika
kampuni alikolipeleka wazo hilo kwa mara ya kwanza?. Lakini yeye hakujikatia
tamaa na wazo lake aliweza kuliendeleza na kumpa mafanikio makubwa. Sasa ndiyo huyu Bill Gates unayemjua sasa
alikotoka na kwa sasa ndiye tajiri wa kwanza duniani.
Nini cha kujifunza kupitia maisha ya watu hawa.
1. Kukataliwa au
kuambiwa huwezi kitu isiwe sababu ya wewe kushindwa na kuamua kuachana na ndoto
zako. Jiamini na kisha songa mbele, utafanikiwa sana tena sana.
2. Kushindwa katika
kile unachokifanya sio tatizo hata kidogo, kikubwa jifunze kupitia kushindwa
kwako huko. Jiulize ni wapi ulipokosea, jirekebishe na zidi kuendelea mbele
kukamilisha ndoto zako.
3. Kujiamini wewe
kwanza, kuwa unaweza na hakuna kitu cha kukuzuia, huo ndiyo ufunguo halisi wa
kukufikisha kwenye njia ya mafanikio.
4. Watu wanaokukatalia
wewe kuwa huwezi, ni wazi hawajui kitu kukuhusu wewe kwamba ni mtu mafanikio.
5. Kama ukishindwa
kitu leo, haimanishi umeshindwa milele. Unaweza ukajipanga upya na kufikia
mafanikio makubwa zaidi ya mwanzo.
Kumbuka, unaweza
kufanikisha malengo yako yote unayotaka ikiwa utaamua na kuishi kwa vitendo na
hakuna wa kukuzuia. Suala la kufanikiwa katika maisha yako siyo la bahati kama
unavyofikiri. Inapotokea umeshindwa jipe moyo na kusonga mbele kwani katikati
ya kushindwa ipo siri kubwa ya mafanikio yako ambayo unatakiwa kitumia na
kufanikiwa zaidi na zaidi.
Tunakutakia kila la
kheri katika safari yako ya mafanikio iwe ya ushindi. Na endelea kutembelea
DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuhamasika zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA
MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)