Oct 30, 2015
Kama Kila Unachokifanya Kimeshindwa Kukupa Mafanikio, Fanya Kitu Hiki.
Inawezekana
umefanya mambo mengi ya kukupa
mafanikio, lakini kila ukiangalia umekuwa ukiona kama juhudi zako zimekwenda
bure. Karibu kila kitu unachojaribu kukifanya unaona kimeshindikana. Kila ukiangalia
hakuna mafanikio makubwa uliyoyapata.
Ninajua
unaweza ukawa unapitia katika hali hii ambayo kwako inakuwa ni ngumu na
inakutesa. Kama ni hivyo huna haja ya kukata tamaa sana. Kila kitu kinaweza
kubadilika. Ikiwa kama kila unachokifanya kimeshindwa kukupa mafanikio, kitu
pekee cha kufanya hapo siyo kukata tamaa kama unavyofikiri, bali ni KUFANYA
KAZI KWA BIDII TENA. Hiki ndicho kitu unachotakiwa kukifanya.
Unaweza
ukasema ‘ooh mbona mimi najituma sana na
nimekuwa nikifanya hivyo siku zote.’ Hilo linaweza kuwa ni sawa kwako,
lakini ongeza juhudi zaidi na zaidi kwa namna tofauti mpaka ‘kieleweke’. Hakuna mbadala mwinginwe wa
kitu cha kufanya zaidi ya kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii kuliko mwanzo. Kama
ulikuwa ukifanya kazi kwa saa 8, unaweza ukaongeza masaa mengine tena ya ziada,
hata kama ni mawili.
Hiyo
ndiyo siri kubwa inyoweza kukutoa hapo ulipo na kukupa maisha mengine ya
kimafanikio. Acha kujihurumia, acha kufikiria kwamba unajitesa. Wewe fanya kazi
kwa bidii. Zipo faida na mambo mengi unayoweza kuyapata ikiwa utaongeza juhudi
za makusudi tena kwa kila unachofanya.
FANYA KAZI KWA BIDII ZOTE. |
Kwanza,
itakusaidia sana kukuondolea wasiwasi kwenye maisha yako. Kwa nini hiyo iko
hivyo ni kwa sababu. Kila juhudi na uwezo wako wote utakuwa umeweka sehemu
moja. Hivyo, hutajilaumu sana kwa matokeo utakayoyapata hata kama siyo ya
kuridhisha.
Pili,
kufanya kazi kwa bidii kutakusaidia kutatua matatizo mengi. Kama kulikuwa kuna
matatizo fulani madogo yalikuwa yanakusumbua itakuwa ni rahisi kwako kuweza
kuyapatia majibu yanayotakiwa.
Tatu,
kufanya kazi kwa bdii kutakupunguzia msongo wa mawazo. Hiyo yote ni kwa sababu
akili yako haitaweza kupata muda wa kufikiria mambo ya ajabu ajabu kwa sabau ya
kuchoka. Baada ya kazi kwako itakuwa ni kupumzisha mwili kwa kulala.
Kama
nilivyoanza makala haya, kama kila kitu unachokifanya kimeshindikana ongeza
juhudi ya kufanya kazi kwa bidii zote kama mtumwa, matokeo mazuri utayapata na mafanikio
yatakuwa kwa upande wako.
Nakutakia
siku njema na mafanikio makubwa yawe kwako siku zote na kumbuka endelea kujifunza
kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
E-mail;dirayamafanikio@gmail.com
Oct 27, 2015
Usiruhusu Mambo Haya Matatu Yakakuzuia Kufanikiwa.
Yapo
mambo mengi ambayo mara nyingi yanakuwa yanamzuia binadamu kufikia mfanikio
yake. Mambo hayo yapo ambayo tunakuwa tunayajua na tunaweza kuyatawala, lakini
mengine tunakuwa hatuyajui, hivyo inakuwa ngumu kuyatawala. Hivyo kwa vyovyote
vile kila mtu hukutana na vizuizi fulani katika safari yake ya kufikia mafanikio.
Kwa
kuwepo kwa vizuizi hivi, hapa ndipo utofauti wa maisha huanza kujitokeza. Wapo
ambao huwa ni rahisi kushindwa kutokana na vizuizi. Wapo pia ambao huwa ni
ving’ang’anizi mpaka kufikia mafanikio yao. Wale ambao hushindwa , kuna wakati
hushindwa kwa vizuizi ambavyo naweza kusema wangeweza kuvishinda kama wangekuwa
makini kidogo.
Hapa
ndipo kipo kiini cha makala haya kilipo. Jaribu kukumbuka kidogo hivi, ni mara
ngapi umekuwa umekuwa ukizuiliwa na mambo madogo madogo kufanikiwa? Bila shaka
ni mara nyingi. Kuna wakati ulishindwa kutimiza ndoto zako kwa sababu pengine
ya visingizio tena visivyo na maana. Utakuta ni sababu ndogo ndogo ambazo umekuwa
ukijitengenezea.
Lakini
leo ninachotaka kukwambiani hiki, kama unataka kufanikiwa usiruhusu kabisa
mambo haya madogo matatu yakakuzuia kufanikiwa:-
1. Kukosolewa.
Acha
kushindwa kufikia mafanikio yako kwa sababu ya kugopa kukosolewa. Makosa unayoyafanya
yachukulie yawe fundisho kwako la kuweza kukusogeza mbele kufikia mafanikio
unayoyahitaji. Acha kusikiliza maneno ya watu wanaozidi kukukwambia kuwa eti
huwezi kufanikiwa tena. Hilo sio kweli kwani hakuna mtu anayejua uwezo wako
halisi.
Wapo
wengi ambao hushindwa kutimiza malengo yao kwa sababu ya kuogopa kukosolewa.
Kama kuna jambo unataka kulifanya wewe lifanye. Kama kuna mtu anayekukosoa mwache
aendelee kukosoa lakini safari yako izidi kusonga mbele. Hakikisha usizuiliwe
na kosa hili dogo na kukufanya ukashindwa kufikia mafanikio yako.
ONDOA HOFU ILI KUFIKIA MAFANIKIO YAKO |
2. Wasiwasi/woga.
Wengi
ni watu wa wasiwasi ama woga sana na hata wao kuna wakati wanashindwa kuelewa
wasiwasi huo hutokea wapi hasa. Utakuta ni watu wa wasiwasi kwa mambo madodogo
madogo na ya kawaida kabisa. Kwa mfano akitaka kufanya jambo hili au lile
anakuwa na wasiwasi mwingi sana nafsini mwake. Hili ni jambo ambalo kiukweli
huwakwamisha wengi kufanikiwa.
Sasa
kwa kuwa na wasiwasi huo ambao unakuwa unaujenga kila siku, inasababisha
mipango na malengo yako mengi kushindwa kutumia. Wasiwasi ni kitu ambacho
kinawafanya watu wengi kushindwa sana kutimiza malengo yao. Hiyo yote ni kwa sababu
unapokuwa una woga unasababisha kushindwa kujaribu mambo mengi ya
kukufanikisha.
3. Maumivu.
Inawezekana
unashindwa kuendeea mbele zaidi ya hapo ulipo kwa sababu ya maumivu uliyonayo
moyoni mwako. Maumivu hayo inawezekana uliumizwa baada ya jambo ulilokuwa
ukilifanya kushindwa kukuletea mafanikio makubwa au kukupa hasara ya kutosha.
Na ikafika mahali ukashindwa kujuani nini cha kufanya.
Haya
ni maumivu ambayo kwa namna moja nyingine tunakutana nayo katika maisha. Ni maumivu
ambayo hutufanya tushindwe kusonga mbele kila tukikumbuka makosa hayo. Kama upo
au ulishapitia hali hii, najua unaelewa ni kitu gani ninacho kiongea hapa. Ili
kufanikiwa, usiruhusu maumivu haya yakakufanya ukashindwa kufikia mafanikio
yako hata siku moja.
Kumbuka,
kwa kuwa na wasiwasi sana juu ya maisha yako, kuogopa kukosolewa na kushikilia
sana na maumivu ni mambo madogo ambayo yanaweza kukuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa. Acha kuruhusu
hali hii ijitokeze kwako. Kuwa shujaa wa maisha yako.
Dira
ya mafanikio inakutakia siku njema na mafanikio makubwa yawe kwako siku zote.
Na kumbuka endelea kujifunza kila siku bila kuchoka.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
E-mail;
dirayamafanikio@gmail.com
Oct 26, 2015
Jinsi Unavyoweza Kufanya Jambo Ambalo Hujisikii Kulifanya.
Maisha
yanakuwa na maana na mazuri kwetu kama tunafanya yale mambo ambayo tunayapenda
na kuyatamani. Inapotokea unakuwa unafanya jambo ambalo hulipendi au hujisikii mara
nyingi mambo yanakuwa magumu sana. Ni kitu ambacho huwa kinatokea, unakuta tu,
hujisikii kufanya jambo fulani ambalo pengine ni muhimu kwako.
Je,
inapokutokea unataka kufanya kitu halafu ukawa hujisikii hapo unakuwa
unafanyaje? Je, unakuwa unaacha na kuendelea na mambo mengine au kuna hatua
unakuwa unachukua? Yapo mambo mengi unayoweza ukawa unajifikiria, lakini ukweli
wa mambo ni kwamba, zipo njia unazoweza kuzitumia kufanya jambo ambalo
hujisikii kulifanya.
Zifuatazo
Ni Njia Ambazo Unaweza Kuzitumia Kufanya Jambo Ambalo Hujisikii Kulifanya.
1. Anza kwa kidogo.
Kama
ni jambo ambalo hujisikii kulifanya anza nalo kwa kidogo. Kama wewe ni
mwandishi unataka kuandika kitu na unahisi hujisikii, anza na sentensi moja
kwanza, hiyo itakupa nguvu ya kuendelea zaidi. Na katika maeneo mengine ya
maisha yako unaweza ukatumia mbinu hiyohiyo, kwa kuanza na hatua ndogo katika
kila jambo.
ACHA KUKATA TAMAA, ANZA KUFANYA MARA MOJA. |
2. Usiruhusu akili yako kuogopa sana.
Kuna
wakati ni rahisi kujisikia huwezi kufanya jambo fulani kwa sababu ya woga ambao
unakuwa umeujenga kwenye akili yako. Mara nyingi akili inapokuwa na woga wa
aina fulani inakuwa siyo rahisi kufanya jambo lolote hata iweje. Ili kufanikiwa
katika hili, kwa vyovyote vile usiruhusu akili yako ikawa na woga wa
kupitiliza, kwa mfano woga wa kuweza pengine hutaweza kufanikiwa.
3. Jipe muda wa kujifunza.
Inawezekana
unashindwa jambo hilo kwa sababu hujalijua vizuri zaidi. Kama ni hivyo jipe
muda wa kujifunza na kulielewa jambo hilo kwa undani. Hii itakusaidia kuanza
kulifanya huku ukiwa na hamasa kubwa ambayo itakusaidia wewe binafsi kuweza
kulifanya jambo lako na kuweza kusonga mbele kimafanikio.
4. Acha kuahirisha.
Pamoja
na kuwa upo ugumu fulani wa kutokujisikia kulifanya jambo hilo, dawa pekee ya
kuweza kulifanya ni jifunze kutoweza kuliahirisha jambo hilo. Lianze hivyohivyo
hata kama ni kwa kidogo, hata kama huku ukiwa unahisi kama mwili hautaki, lakini kikubwa usiahirishe. Kwa kadri
utakavyozidi kufanya bila kuahirisha utajikuta unazidi kuongeza hamasa ya
kulifanya zaidi na zaidi.
Kwa
kifupi, hizo ndizo njia ambo unaweza ukazitumia kufanya lile jambo ambalo kwako
hujisikii kulifanya.
Tunakutakia
siku njema na mafanikio makubwa yawe kwako siku zote. Na kumbuka endelea
kujifunza kila siku bila kuchoka.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,
E-mail;
dirayamafanikio@gmail.com
Oct 22, 2015
Kama Hujui, Hawa Ndiyo Watoto Wenye Akili Nyingi zaidi.
Hivi
karibuni kumekuwa na maneno hata mijadala kuhusu watoto wanaozaliwa kwa njia ya
upasuaji. Kuna madai na maneno kwamba, watoto wanaozaliwa kwa upasuaji wanakuwa
na akili kubwa sana ukilinganisha na wenzao wanaozaliwa kwa njia ya kawaida.
Wataalamu
wa sayansi ya utabibu hivi sasa wanakiri kwamba, watoto wanaozaliwa kwa njia ya
upasuaji, wanakuwa salama kiakili kuliko wale wanaozaliwa kupitia njia ya
kawaida.
Karibu
watoto watatu kati ya kila kumi, wanaozaliwa kwa njia ya kawaida, huwa wanapata
tatizo la kuvuja damu ubongoni, ambalo husababishwa na mchakato mzima wa
kujifungua kwa mama.
Hivi
sasa bila shaka, unaweza ukajua ni kwa nini watu wanaamini kwamba, watoto
wanaozaliwa kwa upasuaji wanakuwa na akili kuliko wale wanaozaliwa kwa njia ya
kawaida. Kama ulikuwa hujasikia, inabidi ujue kwamba, imani hiyo imeingia na
inakua haraka.
Kuna
kipindi ambapo wataalamu wa chuo cha utabibu cha North Carolina, waliwahi
kusema kwamba, watoto wanaozaliwa kwa upasuaji, wanakuwa na akili salama zaidi.
Waliweza
kukiri pia kwamba, kuna uwezekano kuwa, uzaliwaji kwa njia ya kawaida, huathiri
kwa kiasi fulani ubongo wa mtoto. Kwa wale watatu katika kumi athari huwa kubwa
zaidi.
Kwa
wanaozaliwa kwa njia upasuaji, hakuna hata mmoja anayeweza kupata athari ya
kwenye ubongo. Ndiyo maana wale wanaozaliwa kwa njia hii, inatabiriwa kwamba,
wanaweza kuwa na akili kubwa au salama.
Hata
hivyo, watafiti hawa wanasema, ugunduzi huu hauna maana ya kuwataka akina mama
kung’ang’ania kujifungua kwa njia ya upasuajii ili kuwafanya watoto wao kuwa na
akili nzuri na salama.
Mtoto
anapozaliwa kupitia kwa njia ya kawaida, huwa anatoka damu kidogo ubongoni,
lakini wataalamu wanajipa moyo kwamba, huenda hiyo ni njia ya maumbile katika
suala zima la kujifungua.
Hivi
karibuni ndipo ambapo imebainika kwamba, katika harakati za kujifungua kwa njia
ya kawaida, kichwa cha mtoto huwa kinabanwa na ubongo kupata msukomsuko.
Jambo
kama hili halitokei kwenye kujifungua kwa njia ya upasuaji, kwani hapo hakibanwi
na chochote.
Dk.
Honor Wolfe, wa chuo hicho anakiri kwamba, watoto wanazaliwa kwa njia ya
upasuaji wana uhakika wa kuwa na ubongo usio na kasoro, ukilinganisha na wale
wanaozaliwa kwa njia ya kawaida.
Maana
yake ni kwamba, kujifungua kwa njia ya upasuaji inaweza ikaanza kuwa ‘fasheni’ kwa siku za karibuni.
Ni
wazi akina mama wengi wangependa kuona wanazaa watoto ambao wako salama kiakili
kadri inavyowezekana.
Kuna
watu wanaosema kwamba, utafiti huo hauna jipya , kwani binadamu amekuwa
akizaliwa kwa njia ya kwaida kwa miaka nenda rudi.
Kama
ni hatari, basi ilitakiwa iwepo, kwani upasuaji ni njia inayotumika kama kuzaa
kwa kawaida kumeshindikana.
Lakini,
bado ukweli upo kwamba, huenda wengi watu tumeathirika kiakili wakati wa
kuzaliwa. Kama tumeathirika kiakili wakati wa kuzaliwa haina maana kwamba, ni
lazima liwe jambo la awaida.
Kama
kila watu kumi unaokutana nao, watatu walivuja damu ubongoni wakati wa kuzaliwa
, hatuwezi kusema ni jambo la lazima au kimaumbile.
Jarida
la Radiology linaonesha kwamba,
watoto wanaozaliwa Marekani kila mwaka, kwa mfano kati ya milioni 4, milioni 1.1
huzaliwa kwa upasuaji.
Idadi
hiyo imeongezeka hivi karibuni kwa kadri wazai wanavyoamini kuhusu utafiti huu.
kwa afrika kujifungua kwa upasuaji hakuko kwa kiwango kikubwa.
Nilichotaka
kusema hapa ni kwamba ni kweli wale watoto wanaozaliwa kwa upasuaji wanakuwa na
akili kubwa au iliyo na usalama zaidi.
Tunakutakia
mafanikio mema, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713
048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com
Oct 21, 2015
Mbinu Tano Za Kukuza Biashara Yako.
Kwa
mapenzi yake Mungu naamini umzima wa afya na unaendelea kujifunza kupitia
mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO. Nami bila hiana nakukaribisha tena katika
siku nyingine ili uchote maarifa sahihi ya kuweza kukusaidia kubadili maisha
yako. Ni maarifa hayahaya yatakayokusaidia kuboresha maisha yako kila siku na
kwa nyakati tofauti.
Katika
makala yetu ya leo tutaangalia namna unavyoweza kukuza biashara yako na kufikia
viwango vya juu. Ikumbukwe kukuza biashara ni hitaji ambalo karibu kila
mjasiriamali analitamani kulitimiza. Kama ni hivyo basi, unawezaje kukuza
biashara yako? Hapa nimekuwekea mbinu muhimu za kukusaidia kukuza biashara yako
hadi kufikia mafanikio makubwa.
1.
Toa thamani.
Ili
biashara yako iweze kuwa kubwa sana na inayokupa faida, haihitaji mtaji mkubwa
sana kama unavyofikiri, inachohitaji ni thamani unayoitoa. Je, thamani
unayoitoa inaendana na ile ambayo wateja wako wanaitaka? Kama kweli unatoa
thamani halisi, kwa vyovyote vile lazima biashara yako ikue. Haijalishi mtaji
ulionao, toa thamani bora utapata matokeo mazuri.
SOMA;
Sababu Tano Kwanini Unatakiwa Kumiliki Biashara Yako Sasa?
2. Kuwa na mahusiano mazuri na wateja
wako.
THAMANI UNAYOTOA ITAKUPA MAFANIKIO MAKUBWA. |
Unaweza
ukawa unatoa thamani inayotakiwa, lakini kama huna mahusiano mazuri na wateja
biashara yako haitaweza kukua kwa kiwango kikubwa. Wateja ndio kila kitu kwenye
biashara yako. Jitahidi hata kama kuna mteja amekukera mwonyeshe kumjali. Kwani
hiyo itakujengea jina na kupelekea kuwa na wateja wengi wanaohitaji huduma yako.
3. Kuwa na usimamizi mzuri.
Wapo
watu ambao huamua kuanzisha biashara na kuwaachia wengine wasimamie. Linaweza
likawa jambo zuri, lakini linahitaji umakini kwa wasimamizi utakaowaweka. Kama
watasimamia vibaya uwe na uhakika tayari umeua biashara yako. Hivyo, iwe unasimamia
wewe au wengine, inabidi utambue usimamizi mzuri ni kitu ambacho kinahitajika
sana ili kukuza biashara.
4. Tengeneza timu sahihi yakukusaidia.
Haiwezekani
kila kitu ukafanya wewe kwenye biashara yako. Inabidi ifike mahali ambapo unatakiwa
utengeneze timu bora itakayokusaidia kufikia malengo yako. Kipo kipindi ambacho
unaweza ukawa unaumwa, au una dharura fulani. Je, katika hiki kipindi
unafanyaje? Hapa ndipo unatakiwa uwe na timu au watu wa kukusaidia kukuza
biashara yako pale ambapo dharua zinaweza zikajitokeza kwako, ili mambo yaende
mbele bila kusimama.
5. Ongeza ukubwa soko lako.
Kama
ulikuwa ni mtu wa kuuza bidhaa zako ndani ya mtaa mmoja, ni vyema ukaongeza
ukubwa wa soko lako kwa kadri siku zinavyokwenda. Tafuta soko lingine, nje ya
eneo ulipo. Utamudu hili lakini ikiwa utawaridhisha wateja wako wa kwanza ambao
watakusaidia kukutangazia biashara yako, hali itakayopelekea biashara yako
kuzidi kukua siku hadi siku.
Hizo
ni baadhi ya mbinu ambazo unaweza ukazitumia ili kuboresha biashara yako na
kufikia mafanikio makubwa. Je, una mbinu nyingine ambazo unafikiri zinaweza
kutusaidia kukuza biashara na kufikia mafanikio makubwa? Unaweza
ukatushirikisha hapo chini kwenye maoni, tukajifunza pamoja.
Dira
ya mafanikio inakutakia siku njema na mafanikio makubwa yawe kwako siku zote.
Na kumbuka endelea kujifunza kila siku bila kuchoka.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,
E-mail;
dirayamafanikio@gmail.com
Oct 20, 2015
Kama Unataka Kutimiza Ndoto Zako, Acha Kufanya Makosa Haya.
Kila mmoja ana ndoto zake katika maisha, kila mmoja ana njia
yake ambayo anaiamini inaweza kumsaidia katika kutimiza ndoto zake za maisha.
Ndoto ni kama malengo ambayo kila mmoja anakuwa amejiwekea katika safari yake
ya maisha. Mafanikio ni pale unapokuwa umeweza kutimiza ndoto zako. Kuna
ambao walishindwa kutimiza ndoto zao labda kutokana na kutoelewa mambo machache
ambayo walioweza kutimiza mipango yao waliweza kuyaelewa.
Je unaweza kuiweka ndoto yako kuwa hai? Kuweka ndoto hako hai na
kuiishi ni kuepuka kufanya makosa ambayo wengi waliokata tamaa walishindwa. Je
ni makosa gani ambayo wengine hushindwa na kupelekea ndoto zao kuzimika?
1.Wasiwasi.
Wapo ambao ndoto zao zimezimika kwani wamekuwa na wasiwasi sana.
Unaweza ukawa unajiuliza "Je nitafanikisha kweli?". Wasiwasi hauna
nguvu yoyote katika kupelekea mambo yaende sawa bali huaribu mambo kwenda sawa.
Wasiwasi hukatisha tamaa, na kupelekea mtu kuona kuwa hawezi kutimiza malengo
yake. Una wasiwasi wa nini? Unapoona una wasiwasi chekelea na uuambie wasiwasi
wako kuwa "Nitazidi kuwa imara".
Woga ni kitu ambacho kinatenganisha watu waliofanikiwa na
waliofeli kufanikiwa. Kumbuka maana ya kufanikiwa simaanishi pesa na umaarufu
bali hali ya kuweza kutimiza malengo yako uliyopanga ni mafanikio pia.
Hivyo badala ya kuruhusu wasiwasi ukutawale, endelea kuweka
msimamo na kushikilia malengo yako.
MIPANGO MIZURI YA MALENGO NI MUHIMU KUJIWEKEA. |
2. Usikubali
vikwazo vikutawale.
Kwa kifupi ni kuwa lazima utakutana na vikwazo, vikwazo ni jambo
la kawaida katika maisha, vikwazo vipo kwa lengo la kutuimarisha. Na kama
kungekuwa hamna vikwazo tusingeimarika kwani kujisahau kungeongezeka. Vikwazo
vinatakiwa uvitazame kama vile ni ngazi, vinakusaidia kupanda hali fulani na
tunapaswa kujifunza na kuwa imara zaidi katika hali za vikwazo.
Ukifuatilia watu walioweza kuishi katika ndoto zao kila mmoja
atakuambia ni lini alipopata kikwazo kikuu ambacho hatasahau, wengine
walikataliwa kuwa hawawezi, wengine walikosa hata uwezo wa kutimiza ndoto zao,
lakini wote hao ambao wamefanikiwa japokuwa walikutana na vikwazo hivyo,
watakuambia kuwa HAWAKUKATA TAMAA.
Hawakuruhusu vikwazo viwatawale na kuwarudisha nyuma. Walizidi
kuimarika na kusonga mbele na kuzidi kushikilia nia yao.
3. Kubaliana na hali
uliyonayo.
Hali uliyonayo hivi sasa inabadilika. Maisha hubadilika na
hayabaki sawa milele. Hali zinapita, utazidi kukutana na watu mbalimbali,
utazidi kujifunza vitu mbalimbali na maisha hayataacha kukundisha. Wapo ambao
wamekata tamaa kutokana na hali waliyonao hivi sasa haiwezi kuwafikisha pale
wanapodhamiria lakini wanasahau kuwa mambo hubadilika. Jambo dogo linaweza
kubadilisha maisha yako yote na hukutegemea. Maisha ni maajabu.
Kubali hali ya sasa na maisha yako ya wakati huu, shukuru kwa
uhai ulio nao, marafiki wanaokuelewa, na tafuta kitu cha kushukuru nacho badala
ya kujiumiza kwa mawazo na lawama.
Kubali wakati huu wa sasa, shukuru kwa kila jambo, huku ukifanya
juhudi kuhakikisha unaendeleza malengo yako. Hata kwa madogo shukuru.
4. Kushikilia
yaliyopita.
Kosa lingine ambalo wengi hukosea na mwishowe kushindwa kutimiza
malengo yao ni kushikilia wakati uliopita. Bado wanaishi kwa kuwaza makosa
waliyoyafanya, mazuri waliyopoteza n.k. Wakati uliopita ulishapita, wakati
uliopo ndio wakati ambao unakupa nafasi wewe kujirekebisha na kuishi vyema.
Wakati ujao nao unategemea wakati huu wa sasa kutabirika. Kama wakati huu wa
sasa unautumia vyema na kuweka malengo utasonga mbele.
Kumbuka hakuna kiasi cha majuto ya wakati uliopita kinachoweza
kubadili yaliyopita na hakuna kiasi cha wasiwasi kuhusu wakati ujao ambacho
kinaweza kuubadili wakati ujao bali wakati huu wa sasa ndio pekee kwetu sisi. Jifunze
kwa yaliyopita na zidi kusonga mbele.
5. Kusahau
kujitunza.
Wengine husahau hata kutunza miili yao, kula kwa afya, mazoezi,
na kuhakikisha wana afya ya mwili, akili na roho.
Huwezi kufurahia matimizo ya ndoto zako kama una afya mbaya, kama
umezungukwa na tatizo. Usikubali kupoteza uhai, kuharibu afya yako, au kufanya
ambacho kinaashiria huwezi kujitunza na kujithamini. Unapaswa kujijali na
kutambua kuwa nawe unastahidi kujijali badala ya kujali ndoto/malengo yako tu.
Wapo ambao wanaamini bila kusaidiwa hawawezi kutimiza ndoto
zako.
Labda nitoe mfano mzuri, unaweza siku moja ukakutana na mtu na
kutokana na kujitambua kwako ukaweza kuweka urafiki mzuri na mtu yule. Kumbe
mtu yule anafahamiana na fulani ambaye naye kuna kitu ulichokuwa unahitaji sana
kusaidiwa na anakuunganisha na mwishowe unajikuta umepata mtu wa kukusaidia
kutimiza ndoto zako.
Sio kwamba hali ya kusaidiwa haitokei bali hutokea, kumbuka Mungu hana mikono kwamba itashuka mikono mawinguni na kukupa unachotaka bali ulimwengu ukitaka kukupa kitu fulani au huduma fulani hutumia wanadamu wenzio kukufunza na kukusaidia. Badala ya kutegemea msaada bali endelea kuishi vyema, heshimu kila mmoja awe wa chini yako au wa juu yako. Ishi na watu vyema na ishi katika haki. Haimaanishi ukifanya hivi itakusaidia moja kwa moja bali itasaidia njia yako ya kutimiza ndoto zako kwa kukuweka katika amani na watu.
Sio kwamba hali ya kusaidiwa haitokei bali hutokea, kumbuka Mungu hana mikono kwamba itashuka mikono mawinguni na kukupa unachotaka bali ulimwengu ukitaka kukupa kitu fulani au huduma fulani hutumia wanadamu wenzio kukufunza na kukusaidia. Badala ya kutegemea msaada bali endelea kuishi vyema, heshimu kila mmoja awe wa chini yako au wa juu yako. Ishi na watu vyema na ishi katika haki. Haimaanishi ukifanya hivi itakusaidia moja kwa moja bali itasaidia njia yako ya kutimiza ndoto zako kwa kukuweka katika amani na watu.
Wengine husubiria mpaka wawe na pesa kutimiza malengo yao,
wakati wakiwa hawana uwezo wa kutimiza malengo yao wanaacha ndoto zao. Kiukweli
unaweza pia kila siku ukafanya jambo moja ambalo linahusiana na ndoto zako,
hata kama ni dogo lakini siku yako imepita vyema kwa kuiishi katika ndoto yako.
7. Kujisikia vibaya watu
wakikusema vibaya.
Fahamu kuwa watakuhukumu (watahukumu kwa mabaya au kwa mema),
kwani wanadamu wengine hupenda kuhukumu watu na kuwazungumzia watu, lakini
ukipoteza raha yako kuwaza watakuhukumu vipi utakuwa mtumwa. Sio vibaya
kusikiliza watu wanavyokuhukumu, lakini ni vibaya pale mtu anapokuhukumu vibaya
na wewe kumchukia, mpende na jifunze uimara kupitia yeye, kwani changamoto hiyo
ipo kwa ajili ya kukuweka imara na kuzidi kuongeza upendo kwa wanaokusema
vibaya.
Shukuru kwa kila jambo na jiamini.
8. Kushikilia mambo
hasi.
Ni vigumu kuwaza mambo chanya au hasi kwa pamoja, bali unaweza
kuwaza au kushikilia moja. Kumbuka mawazo na fikra zako huumba. Pale unapoona
unawaza mambo katika upande chanya basi badili mtazamo wako na jaribu kuwaza
katika upande wa hasi.
Wengi wanawaza kuwa "ni vigumu kufanya hivi",
"Ukifanya hivi utashindwa", "Wewe huwezi",
"Unajidanganya" n.k. Mawazo haya hayajengi bali huzidi kukupa hofu.
Unapowaza mambo chanya hupelekea mambo chanya kutokea na unapowaza mambo hasi
hupelekea hasi kutokea. Kila njia moja ina umuhimu na kila njia inakupeleka
katika upande tofauti.
Badala kuwaza mabaya na kushikilia imani duni weka msimamo wako
katika njia sahihi. Usikubali kuwaza mabaya wakati wote. Usikubali hofu,
wasiwasi, hukumu, maneno, mawazo mabaya yakutawale.
Unapoweka akili katika mawazo hasi unaipa nafasi ya kukuonyesha
njia.
9. Kujilinganisha na
wengine.
Kujilinganisha hupelekea "wivu" na "tamaa".
Usikubali kujilinganisha na watu wengine, usikubali kuweka tamaa ya kutamani
maisha au hali ya mwingine. Sheherekea mafanikio ya mwenzio lakini sio utamani
na kutaka kuwa kama yeye, bali jifunze kupitia kwake na wewe uwe kama wewe.
Kila mmoja ana safari yake ya maisha, ndio maana uhai ukajigawanya katika
personality mbalimbali.
Hata wewe ukijiangalia kuna anayetamani kuwa kama wewe, kuna
ambaye hajafika ulipofika wewe, kuwa wewe kama wewe huku ukifurahia mafanikio
ya wenzio na sio ushindani, wivu, tamaa n.k.
10. Kutaka Watu Wakukubali
Kwa Ndoto Zako.
Usifanye kitu ili watu wakuone mjanja au watu wakusifie bali
weka malengo yako kwa nia ya kujiendeleza wewe na kuendeleza wanaokuzunguka.
Ukitaka watu wakukubali ukitimiza ndoto zako utakuwa unaishi kama mfungwa.
Jikubali kwanza wewe na hakikisha unaishi katika ndoto yako wewe kama
wew
Fahamu unataka nini, weka nia kwa
unacholenga, na tumia ulichonacho na kila nafasi uliyonayo kufika unapopanga.
Makala hii imeandikwa na Apolinary Protas wa JITAMBUE
SASA . Unaweza kujifunza zaidi kuhusu maisha na mafanikio, kwa kutembelea
blog yake www.jitambuesasa.blogspot.com. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana naye
kwa email jitambuesasa@gmail.com
|
Oct 19, 2015
Mambo 6 Ambayo Watu Wasio Na Mafanikio Wanayafanya Kila Wakati.
Kitu
kikubwa kinachotofautisha watu wenye mafanikio na wale wasio na mafanikio ni
fikra, tabia na yale mambo ambayo wanayafanya kila siku. Watu wenye mafanikio
yapo mambo ambayo wanayafanya kila wakati na ambayo huwapelekea kufanikiwa
kwao. Na watu wasio na mafanikio yapo mambo pia ambayo wanayang’ang’ania
kuyafanya na yanapelekea kushindwa kwao.
Kwa
hiyo kama katika maisha yako hujafikia viwango fulani vya mafanikio
unayoyahitaji, tambua kabisa kuna mambo ambayo umekuwa ukiyang’ang’ania sana na
yamekufikisha hapo ulipo. Hivyo, kama unataka kufanikiwa na kutoka hapo ulipo
huna haja ya kujilaumu sana, ni kitendo cha kuamua na kuchukua hatua ya
kuachana na mambo yanakurudisha nyuma.
Kwa
haraka haraka naomba nikutajie mambo ambayo wasio na mafanikio wanayafanya kila wakati.
1. Kulalamika.
Watu
wasio na mafanikio mara nyingi ni watu wa kulalamika sana. Utakuta
wanalalamikia hiki mara kile na mwisho hujikuta wakishindwa kuchukua hatua na
kubaki kama walivyo. Hili jambo ambalo hulifanya karibu kila siku kwa
kulalamikia hata mambo madogo ambayo wanauwezo wa kuyabadili. Na kwa
kulalamikia huko sana, hujikuta wakishindwa kufanikiwa.
ACHA KUWAZA HASI KILA WAKATI
2. Kuwaza hasi.
|
Fikra
na mitazamo ya watu wasio na mafanikio mara nyingi zipo hasi sana. Karibia kila
kitu wanakiona kwa mtazamo hasi. Hata suala la mafanikio kwao wanakuwa wanaona
ni suala la wengine sio lao. Kwa mitazamo hiyo huwafanya wazidi kuona kila kitu
hakiwezekani ikiwa pamoja na mafanikio yao. Kwa kuendelea kujenga fikra hasi,
hivyo ndivyo ambavyo hujikuta maisha yao wakiyabomoa bila kujijua.
3.
Kupoteza muda.
Kati
ya kitu ambacho hakina thamani sana kwa watu wasio na mafanikio ni muda.
Matumizi yao ya muda ni mabovu utafikiri wao wana saa 48 kwa siku. Na kutokana
na sababu hii ya kupoteza muda hovyo, maisha yao hubaki kuwa ya hovyo. Kwa
sababu hakuna wanachokuwa wanakizalisha katika muda mwafaka. Muda mwingi
wanakuwa wanapoteza katika mambo ya kipuuzi na yasiyo na maana.
4. Kupuuza.
Siku
zote watu wasio na mafanikio maisha yao ni ya kupuuza mambo mengi ambayo kama
wangeyafatilia yangewaletea mafanikio makubwa. Ni watu ambao wanapuuza kwa
kudharau sana biashara ndogo ingawa hawana. Hiyo haitoshi wanapoteza pesa kwa
matumizi yasiyo ya msingi kwa kuona si kitu. Utakuta haya ndiyo maisha yao kwa
sehemu kubwa wanaishi kwa kupuuza mambo madogomadogo ambayo baadae
yanawarudisha nyuma kimafanikio.
5. Kujenga uadui.
Pia
hiki ni kitu ambacho watu wasio na mafanikio wanacho. Mara nyingi ni watu wa
kujenga uadui na watu waliofanikiwa. Maisha yao yanakuwa yamejaa roho mbaya
ambazo hazitaki kuona wengine wakifanikiwa. Kwa ubinafsi huo wanaoutengeneza
mara kwa mara, huwafanya washindwe kujifunza kutoka kwa watu walio na
mafanikio. Na matokeo yake hujikuta maisha yao yakizidi kuwa magumu.
6. Kuficha ukweli wa mambo.
Siyo
rahisi kwa watu wasio na mafanikio kuweka wazi ukweli wa maisha yao, hata inapotokea
pale wanapohitaji msaada wa kweli. Hawa ni watu ambao ni wasiri sana na
hujifanya wana mafanikio kumbe hawana. Na Hili ndilo kosa kubwa wanalolifanya
ambalo linawatesa na kuwafanya wakose msaada wa kile wanachokitaka katika
maisha yao ya kila siku.
Kwa
vyovyote vile, maisha uliyonayo sasa, yanatupa picha nzima ya kile
unachokifanya mara kwa mara. Ikiwa maisha yako ni ya mafanikio, endelea
kung’ang’ania mambo yaliyokupa hayo mafanikio. Lakini, ikiwa maisha yako ni ya
kushindwa inabidi ubadili mwelekeo haraka sana na kuacha kushikilia mambo
yanayokurudisha nyuma. Kwa kifupi, hayo ndiyo mambo ambayo watu wasio na
mafanikio huyafanya sana katika maisha yao.
Tunakutakia
mafanikio mema, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
Kumbuka TUPO PAMOJA.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com
Oct 16, 2015
Hizi Ndizo Athari Mbovu Za Malezi Kwa Watoto Wetu.
Tumekuwa
tukishangaa au kama siyo kushangaa, kukerwa na kuachiwa maswali na tabia hii. Inasemekana
wasichana wa mijini wanadanganyika kirahisi sana zaidi kwa magari. Utakuta msichana
anakubali kuwa na uhusiano na mwanamume kwa sababu amegundua kwamba, ana gari.
Lakini,
wengine wanajua kabisa kwamba, gari siyo la huyo mwanamume, lakini hujikuta
wakikubali kuwa na uhusiano naye kwa sababu ya gari tu. Ndiyo maana madereva
wengi, hasa wale wa teksi wanajisifu kwamba, wanawake wanawapapatikia sana. Kuna
ukweli wa aina fulani.
Lakini,
je wasichana ni wote ambao
wanawapaptikia madereva au watu wenye magari? Ndilo swali gumu sana kwenye
suala hili. Kila kitu kinachohusu uhusiano wa kimapenzi, tunajifunza kutoka kwa
wazazi au walezi wetu, labda asilimia 10 tu ndiyo tunajifunza nje ya nyumbani.
Siyo
suala la gari peke yake, bali ni suala la karibu kila kitu. Je watoto wetu
tunawajengea dhana gani kuhusu kila kitu kwenye maisha? Halafu tunawaambia kitu
gani kuhusu kupenda? Siku zote na tulio wengi, tunawaambia watoto wetu uongo
mwingi sana.
Uongo
huo unatokana na sababu nyingi. Kwanza, nasi tulidanganywa na wazazi wetu. Pili
hatujiamini. Tatu, hatuna uhakika sisi ni akina nani na nne, tunadhani uongo
huo utawasaidia watoto kuwapa moyo.
Hebu
chunguza kwa makini, utagundua kwamba, wasichana wanaobabaikia magari ni wale ambao
wamelelewa kwenye malezi ya uongo mtupu.
Unaweza
kudhani wale waliotoka kwenye familia maskini ndiyo ambao wanababaikia magari,
hapana. Msichana anaweza kutoka kwenye familia maskini na asibabaikie utajiri
wala mali ya mtu. Wako wengi wa aina hiyo.
Kama
nyumbani, wazazi wanasifu wenye magari, wanaonesha kwamba, ukiwa na gari ndiyo
unakuwa na maana, kwamba, gari ni kiwango cha juu cha mafanikio, unatarajia
kitu gani kutoka kwa watoto? Kuna wakati wazazi wanasema, ‘ameshafika mbali siyo mwenzio, yule ana akili bwana. Ana magari mawili
na nyumba tatu’
Wakati
mwingine inatosha mara moja tu jambo kusemwa na mzazi na mtoto kuamini, kwamba,
mwenye gari au magari na nyumba, ndiye aliyekamilika, ndiye mwenye akili.
Kumbuka,
mtoto anaingiza akilini mwake maarifa kutoka kwa watu anaowaamini na anaokutana
nao maishani. Kwenye suala la uhusiano, wazazi ndiyo wanaoaminika zaidi.
Kwa
sababu ya umaskini wetu tulio wengi, gari na nyumba ndiyo tunayoyachukulia kuwa
ni malengo ya juu kabisa kuyapata. Kwa hiyo mtoto anakuwa ana akili ya aina
hiyo , kigezo chake kuhusiana na mtu kitakuwa ni gari na nyumba au mali kwa
ujumla.
Kwake,
binadamu, mwenye maana na anayefaa ni yule anayemudu kumiliki vitu hivyo, hii
siyo kwa wasichana peke yake, bali hata wanaume, kama mtoto wa kiume alioneshwa
thamani ya mtu inatoka kwenye gari, nyumba, na mali, naye bila shaka atakuwa
anababaikia vitu hivyo.
Linapokuja
suala la uhusiano, anajitahidi kumwonesha msichana kwamba, anavyo vitu hivyo
au anao uwezo wa kuvimiliki. Anafanya hivyo, kwa sababu, aliambiwa thamani yake
inakuwepo pale anapokuwa na vitu hivyo.
Wazazi
wengi wameegemeza thamani zao kwenye vitu, badala ya wao wenyewe. Bila hiari
yao wanawafundisha watoto watoto wao kujali na kuthamini vitu, badala ya utu
wao. Kwa kadri mfumo wa maisha ulivyokuwa ukiendelea, ukilinganisha na zamani,
utagundua binadamu alijitoa thamani na kuiweka kwenye vitu, hasa mali.
Bahati
mbaya, wale watoto wa wazazi ambao wana maisha ya kati, ndiyo ambao
wanasumbuliwa sana na mali. Kwa nini? Wazazi hao hawajui kama wako juu au chini
kimapato.
Katika
kujitafuta hufanya mambo na kutoa kauli zenye kuonesha kwamba, maisha ni mali,
basi. Wazazi walio chini kabisa, wanaweza nao kuwaathiri vibaya watoto kwa
kuzungumza na kutenda kwa njia ambayo watoto wataamini kwamba, umaskini huondoa
kabisa thamani ya mtu.
Wale
wa juu kabisa, wanaweza wasifikirie kuwa gari au nyumba ni mambo ya maana sana,
hata kama wamefundishwa kuhusu mali. Wao watafikiria mali kwa mkabala mkubwa
zaidi.
Labda
watafikiria kuhusu ndege ya kutembelea, boti ya kifahari na mengine. Lakini, yote
ni ileile, kuamini mali ni kubwa kuliko thamani ya binadamu. Mali ambayo
unaitengeneza na kuitafuta mwenyewe iwe kubwa kuliko wewe.
Wazazi
ambao wanakuchukulia mali kwa ujumla, kama kitu cha kawaida sana, ambacho uwe
nacho au usiwe nacho, maana ya maisha haibadiliki, na thamani yako haiondoki,
hawa ndiyo ambao watoto wao tunawapenda.
Nikisema
tunawapenda, nina maana kwamba, ni watu ambao kwao, kila binadamu ana thamani
bila kujali anamiliki au hamiliki kitu gani. Wazazi ni wepesi sana kusema, ‘hawa watoto wetu nao, wakiona mwanamume ana
gari, basi wanamkubali tu, bila hata kuchunguza’
Lakini,
nyumbani akina mama kauli zao ni hizi; ‘ukiwa
na gari na wewe mbele ya watu unasimama ati’ halafu wanatarajia mtoto
anayesikia kauli hizo aje ajue kuwa ana thamani kuliko gari. Hizo ni ndoto za
mchana.
Ni
wazazi hawahawa ambao hawaishi kusema, ‘umefanya
kazi miaka yote, hata nyumba wala gari huna, una akili kweli wewe?’ watoto
wanasikia, wanaamini kwamba, asiyemiliki nyumba au gari hana akili. Halafu leo
watoto wetu wakiyumbishwa na vitu hivi hadi wanakuwa kama vichaa, tunashangaa.
Nakutakia
siku njema iwe ya ushindi kwako na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na
kuhamasika.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia
mafanikio yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035
kwa ushauri na msaada wa haraka.
Oct 15, 2015
Kama Na Wewe Utazidi Kung’ang’ania Fikra Hizi, Umaskini Ni Halali Yako.
Katika
hali ya kawaida, fikra ulizonazo ndizo zinazoamua maisha yako yaweje. Kama
unafikiria chanya ni wazi maisha yako yatakuwa ya mafanikio, lakini kama pia
utakuwa na fikra hasi nalo hilo halina ubishi ni lazima utaishia kwenye
umaskini tena wa kutupwa. Je, wewe binafsi huwa una mawazo gani? Yakukufanikisha
au kukwamisha?
Wengi
wanakwamishwa sana na mawazo yao badala
ya kuwasaidia. Utakuta ni watu wa kulalamikia sana watu wengine lakini ukija
kuchunguza kinachowatesa ni mawazo yao na si kingine. Mara nyingi huwa nashangaa
sana hasa pale ninapokutana na watu wengi wakiwa na fikra kama za kutaka kusaidiwa sana katika maisha yao. Bila shaka umeshawi
kuliona hili, tena nina uhakika sana tu.
Hizi
ni moja kati ya fikra au mawazo mabovu yanayowarudisha watu wengi nyuma sana
kimafanikio. Wengi wanafikra hizi sana za kutaka kusaidiwa badala ya kusaidia.
Kila mmoja anakuwa anajitahidi sana kufikiria namna atakavyoweza kusaidiwa na
ndugu yake, serikali, mfadhili au tajiri fulani. Ni jambo la ajabu sana kuona
watanzania wengi wanafikra kama hizi.
Tangu
tukiwa wadogo tumefundishwa kwamba, maana ya ndugu ni kusaidiwa naye, siyo
kumsaidia. Tunakuja kujua kuhusu kumsaidia ndugu, pale tunapokuwa watu wazima
na kuwa na uwezo ambao unawafanya hao ndugu kutujia kutuomba msaada. Lakini
muda wote huwa tunajua kwamba, wajibu wetu ni kusaidiwa.
Kwa
hali hiyo, tumejengewa dhana kwamba, serikali inawajibu wa kutusaidia na ndugu
na jamaa zetu wapo kwa ajili ya kutusaidia. Hivyo tunasahau kwamba, ni wajibu
wetu kusaidia kuliko kusaidiwa.
Kuna
msemo maarufu sana duniani ambao uliwahi tolewa na Rais wa zamani wa marekani
kwamba, kabla hujauliza nchi yako imekufanyia nini, jiulize wewe umeifanyia
kitu gani nchi yako. Msemo huu una mantiki kubwa sana ndani. Lakini pia kabla
hujadai ndugu yako akusaidie, jiulize wewe umewahi kumsaidia nani maishani mwako?
Kwa kawaida, wasiosaidia wala kujisaidia, ndiyo wanaodai sana kusaidiwa.
Ni
jambo la kusikitisha kwamba, kwa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, ndivyo
watu wengi wanazidi kuamini kwamba, wajibu wao ni kusaidiwa na kamwe kusaidia
hakuwahusu. Kwa hali hiyo, mtu anakwepa kulipa kodi, halafu analaumu barabara
haihudumiwi, hakuna dawa hospitalini au hakuna huduma za jamii kwa ujumla.
Kuna
watu ambao kazi yao kubwa ni kuwalaumu ndugu zao kwamba, hawataki kuwasaidia,
kuilaumu serikali kwamba, haiwajali, bila kujiuliza ni nani aliwaambia kuna
kudai haki bila wajibu.
Inabidi
kila mmoja atimize wajibu wake, ili kuomba haki kwake liwe ni suala lenye
mashiko. Kuomba haki bila kutimiza wajibu ni aina ya ukichaa. Wajibu wa kila
mmoja wetu ni kuuliza yeye amesaidia wapi, amemsaidia nani, na amesaidia nini,
na siyo amesaidiwa na nani, lini na wapi.
Siyo
suala la mzaha kwamba, wengi wanazidi kuwa wataalamu wa kuomba, wataalamu wa
kusubiri kusaidiwa wafanyiwe, bila wao kujiuliza mchango wao kwenye kutenda
ambayo yatawasaidia wengine hata serikali pia. Kuna haja ya kubadilika kwani
tunaelekea kuchelewa. Na ndio maana kama unandelea kung’ang’ania fikra hizi,
mafanikio kwako yatakuwa ni ndoto za mchana.
Tuanze
kujifunza na kuwafundisha watoto wetu kwamba, wajibu wao ni kusaidia na siyo
kusaidiwa. Ni lazima tuwafundishe kwamba, wasione aibu kusaidiwa, lakini
wasiishi kwamba, kusaidiwa ndiyo wajibu wao.
Ni
lazima tuanze kujifunza kuwajibika badala ya kudai haki kwanza. Kwa kujifunza
kuwajibika, tunajikuta tukisaidia badala kuishi kwa kusubiri kusaidiwa.
Nakutakia
mafanikio mema
na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia
mafanikio yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035
kwa ushauri na msaada wa haraka.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)