Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, February 5, 2016

Njia Rahisi Za Kukupa Hamasa Ya Mafanikio Wakati Mipango Yako Inapokwenda Vibaya.

No comments :
Kuna wakati ambapo katika safari yetu ya mafanikio, mambo huwa hayaendi sawa kama tulivyopanga. Ni kipindi ambacho kinakuwa kigumu kwa wengi na kupelekea hata hali ya kukata tamaa kuingia ndani mwetu. Natambua umeshawi kukutana na hali kama hii wakati fulani kwenye maisha yako.
Je, mipango na malengo yako ilipokwenda hovyo ni kipi ulichokuwa ukikiwaza? Ilifika mahali ulikata tamaa au ulifanyaje? Kitu kikubwa cha kuelewa hapa, mambo yako yanapokwenda hovyo isiwe sababu ya kukata tamaa, dawa ni kusonga mbele. Na utaweza kusonga mbele ikiwa utakuwa na hamasa kubwa ya kufanikiwa. Na hamasa hiyo utaipataje?
Zifuatazo Ni Njia Rahisi Za Kukupa Hamasa Ya Mafanikio Wakati Mipango Yako Inapokwenda Vibaya.
1. Tambua upo kwenye kipindi ambacho utakipita.
Pamoja na kwamba unaweza ukawa unaona mipango yako imeenda vibaya kuliko kawaida, lakini tambua upo kwenye kipindi cha mpito. Hautaweza kukaa katika hali mbaya uliyopo siku zote. Ni lazima utavuka, hivyo kama ulikuwa umeanza kukata tamaa nyanyuka ulipo kwani ushindi upo mbele yako unakusubiri.

USHINDI NI LAZIMA.
2. Kuwa na watu chanya.
Mipango yako unapojikuta imeenda hovyo kinyume na ulivyotarajia, njia bora nyingine ya wewe kuweza kujihamasisha na kusonga mbele ni kuwa karibu na watu chanya. Hawa ni watu watakaokusaidia kukupa hamasa na hamu ya kuendelea mbele. Pia watakusaidia kukufariji na kukunyanyua zaidi pale ulipo kwama.
3. Panga malengo yako tena upya.
Najua kama umekwama sehemu, ni rahisi sana ‘kupaniki’ na kuona kila kitu basi hakiwezekani tena. Lakini ukweli wa mambo ulivyo inapotokea mambo yako yanapokwama, tuliza akili na weka mipango yako upya. Kushindwa kwako mara moja kusikufanye ukashindwa kupanga malengo mengine. Panga mambo upya ya kukufanikisha tena.
4. Ondoa hofu zote ulizonazo.
Haina haja ya kubeba wasiwasi mwingi ndani yako eti kwa sababu umeshindwa mara moja.  Vaa moyo wa ujasiri na kuamua kwamba ni lazima usonge mbele hata iweje. Kama kupanga malengo yako yapange tena. Kushindwa kwako mara moja haimaanishi kwamba huo ndio mwisho wa mafanikio yako tena. Unayo nafasi ya kujaribu na kufanikiwa. Usiruhsu kabisa hofu ikawa kikwazo kwako.
Ukiamua unaweza kufikia mafanikio yako makubwa bila ubishi.
Nikutakie siku njema na mafanikio mema. Kumbuka endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kila wakati, kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika.
Kama makala hii imekusaidia kwa namna moja au nyingine, fanya tendo la upendo kwa kumshirikisha na mwingine aweze kujifunza kupitia mtandao huu.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048035,

No comments :

Post a Comment