Aug 8, 2016
Sumu Inayoathiri Mafanikio Ya Wengi.
Uliwahi kukaa chini na kujiuliza hivi
ni kwanini baadhi ya mambo mengi hufeli zaidi kuliko kuwa katika ubora ambao
mtu ametarajia? Kama hujawahi kujihoji ipo haja zaidi ya kuushirikisha ubongo
wako muda huu katika kuyafakari hayo ili kujua kwa undani zaidi.
Watalamu wa saikolojia wanazidi
kututabainisha ya kwamba uwezekano mkubwa wa jambo lolote ambalo unalitaka
kulifanya au unalifanya upo uwezekano wa matokeo yake yasiwe kama vile ambavyo
ulitarajia awali.
Hata hivyo watalaamu hao hao wanazidi
kutukumbusha ya kwamba mambo mengi huwa yanafeli zaidi kuliko kuwa bora hii ni
kutokana kutokuwepo kwa hamasa ya kutosha aliyo nayo mtu katika kulitenda jambo
fulani.
Hamasa hii imsukumayo mtu katika
kulitenda jambo fulani, ndiyo sumu ambayo inayaathiri mafanikio ya wengi wetu
kwa kiwango kikubwa sana. Ukichunguza kwa makini katika safari yeyote ya
kuyasaka mafanikio mwanzoni huwa ni safari yenye utamu mwingi kuliko uchachu.
Utamu huo ambao nauzungumzia ni
kwamba kila mtu wakati anaanza kulitenda jambo fulani huwa yupo katika hali ya
kulipenda sana jambo hilo, hata hivyo ndipo tunapoona ya kwamba hamasa
isukumayo mtu katika kulitenda jambo hilo huwa kubwa sana.
Lakini pamoja na hamasa hiyo kuwa
kubwa huanza kupungua siku hadi siku, hii hutegemea na kiwango cha
changamoto ambazo zitajitokeza. Hebu tujikite kidogo kwa kuona baadhi ya mifano
itakayotusaidia kutafakari hili kwa undani zaidi.
a) Hebu tujiulize ni mahusiano
mangapi leo hii yamekufa? Huku mitazamo ya watu wengi hawakutegemea kama
mahusiano hayo yatakufa?
b) Ni biashara ngapi ambazo zilianza
vizuri lakini kadri siku zinavyozidi kusonga nazo zinalegalega?
c) Ni wanafunzi wangapi ambao leo
wameacha kuendelea na masomo yako lakini mwanzoni wakati wanaanza masomo
walikuwa wanafanya vizuri? Achilia mbali sababu za kutokuwapo na fedha
kwa masomo bali jikite zaidi katika kutafakari sababu zile za kawaida
kabisa.
c) Jiulize tena kwanini mara nyingi
vipaji vingi vya watu hufa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele?
Kwa hayo machache kati ya mengi
ambayo umeyatafakari au unatakiwa kuyatafakari utagundua sababu za kufeli
kwake ni Kutokana na muhusika huyo kukosa hamasa ya kupenda jambo hilo.
Lakini vilevile zipo changamoto kubwa
na nyingi ambazo hujitokeza katika jambo hilo. Na kutokea kwa changamoto hizo
ndizo ambazo zikekuwa sumu kubwa sana ambazo zinawafanya watu wengi kukakata
tamaa mapema.
Nini kifanyike ile kuongeza hamasa za
kiutendaji ili kufanikiwa?
1. Lifanye jambo lolote kwa upendo na sio kwa hofu au kwa
kujaribu.
Upendo wa jambo lolote ambalo
unalifanya linakufanya wewe kuweza kuwa katika hali ya ushindi wa mafanikio
yako. Kupenda kitu kunakufanya kujua mbinu ambazo zitakusaidia kukabiliana na
changamoto ambazo zitajitokeza.
Kwa mfano kama unataka kukua
kibiashara lazima ipende kwa dhati biashara yako lakini ukiweka chuki kati yako
na biashara yako biashara nayo itaweka chuki nawe, na kufanya hivi ni
kutengeneza mazingira ya kufa kwa biashara yenyewe.
2. Zifanye changamoto kama njia za kukifikisha kwenye lengo
lako.
Kila jambo lolote lina changamoto
zake hivyo huna budi kuziogopa changamoto hasa chamgamoto zitakazokufanya
ushindwe kufika kwenye Ndoto zako kubwa.
Jambo la msingi zifanye changamoto
kama njia ya kufika kule utakako, Huna haja ya kuacha kufanya jambo lolote
lenye kukuletea mafanikio ambalo unalitaka kulifanya kwa sababu ambazo
sio msingi katika kukamilisha Ndoto zako.
3. Fanya kitu ambacho unakiogopa.
Ili uweze kufanikiwa huna budi
kutokugopa kufanya jambo lolote. Kuacha au kugopa kufanya jambo lako ni dalili
tosha kwamba huna hamasa za kiutendaji pia kufanya hivi kunakufanya kwa
asilimia kubwa kuweza kufa na ndoto zako.
Lakini nikukumbushe ya kwamba idadi
kubwa ya watu ambao wamefanikiwa katika sayari ni kwamba walifanya vitu ambavyo
walikuwa wanaviogopa na mambo hayo ndiyo yaliyosaidia kugeuza maisha yao kwa
asilimia kubwa. Na watu hao wenye mafanikio huwa hawasimamishi masikio yao
kusikiliza nani kasema nini, hususani wale wakatishaji tamaa. Tabia hii ya watu
walifanikiwa ukiitumia leo itakusaidia sana.
Hivyo nikutie moyo kwa kukwambia ya
kwamba ndoto zako zinakwenda kuwa kweli endapo utakwenda kuijenga misingi imara
ya hamasa za kiutendaji kwa jambo lolote lile ambalo unalifanya au unataka
kulifanya.
"Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi" kwa kuendelea
kutembelea mtandao huu wa Dira ya mafanikio.
Ndimi; afisa mipango Benson Chonya.
E-mail; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.