Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, March 7, 2017

Kinachokupa Mafanikio Ni Hiki…

No comments :
Si kile unachokifanya ndio kina uhakika wa kukupa mafanikio kwa asilimia zote. Kama ulikuwa unafikiri hivi unajidanganya.
Hunielewi vizuri hapa ngoja nikwambie kwa namna hii, kama unafikiri kwa sababu huna kazi fulani ndio maana huna mafanikio sio kweli.
Unaweza ukafanya kazi unayoiona nzuri na usiweze kupata mafanikio unayotaka. Mafanikio si matokeo ya kazi ya aina fulani.
Bali kinachoweza kukupa mafanikio ni namna unavyofanya hicho unachokifanya sasa, kitu hicho unachokifanya unakifanya kwa mbinu zipi.
Kile unachokifanya sasa, kinakukupa ‘tiketi’ ya wewe kwamba sasa unawezaje kupata mafanikio yako unayoyahitaji.

Namna unavyofanya, ndipo hapo mafanikio yako yalipo.
Acha kubweteka au kujiona eti hufai kwa sababu umesikia hicho unachokifanya hakina mafanikio makubwa.
Jiulize ni nani aliyekudanganya hadi ukaamua kujenga imani kama hiyo ambayo unaendeleza kuijenga sasa?
Watu wengi wanakwama kwa sababu ya kujiona wanyonge wa kazi wanazozifanya kwa kuamini kwamba eti hawawezi kufika mbali.
Kila wakati kumbuka mafanikio yote yanapatikana kulingana na mbinu unazotumia kwa hicho unachokifanya na sio unafanya kitu gani.
Hivyo, acha kujiuliza kila wakati unakosa nini, badala yake tambua namna ya kuboresha hicho unachokifanya mpaka kikupe mafanikio makubwa.
Unaweza kufikia mafanikio makubwa ikiwa utajua namna ya kufanya hicho unachokifanya kwa utofauti na ubora wa hali ya juu.
Unaweza kuongeza kipato chako na kuwa kikubwa kabisa ikiwa kama utajua kukifanya hicho unachokifanya kwa ufasaha zaidi.
Chochote kile unaweza, ila mahala pa kuanzia ni kutambua kwamba kinachokupa mafanikio ni jinsi unavyokifanya hicho unachokifanya sasa na si vinginevyo.
Tunakutakia siku njema na kila kheri,
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,

No comments :

Post a Comment