Oct 31, 2017
Kama Unafikiri Mafanikio Utayapata Kwa Njia Hii, Sahau.
Kujenga
nidhamu binafsi na kuishi maisha unayoyataka wewe sio kitu rahisi kinachotokea
tu mara moja.
Kujitoa
na kufanya yale yanayotakiwa kufanyika ili kuweza kutimiza ndoto zako,
halikadhalika hicho nacho si kitu rahisi.
Kuweza
kutimiza ahadi zako na kuwa na mawazo zingativu juu ya ndoto zako pia nacho
hicho si kitu rahisi kuweza kukufanikisha kama unavyofikiri.
Kupanga
mipango yako na kufanyia kazi ili iweze kutoa mafanikio pia hicho sio kitu
rahisi, kuna ugumu fulani unaojitokeza.
Ukiangalia
katika maisha karibu kila kitu ambacho unataka kukifanya na kweli kikatoa
mafanikio, kina ugumu wa aina fulani hivi.
Ukiona
kuna jambo ukilifanya ni mteremko sana kwako na halihitaji wewe kujibidiisha sana, ujue hapo kufanikiwa si
rahisi sana pia.
Utaona
mpaka hapo mafanikio yanahitaji nguvu na kujitoa sana kila wakati na kila siku ili uweze kuyafikia.
Lakini
ikiwa utaamua kuyaendea mafanikio kwa mkono wako mlegevu au kwa jinsi
unavyotaka wewe kufanikiwa kwako itakuwa ni shida.
Hapa
sina shaka unapata picha kamili kwamba hakuna kitu rahisi katika hii dunia. Kila
kitu kina ugumu wake katika kukipata.
Ukiona
mtu anakwambia mafanikio ni rahisi au wewe mwenyewe unaona mafanikio ya mwingine
yamepatikana kama kwa urahisi vile, sio kweli.
Ipo
namna yule mtu ambaye labda unamuona kafanikiwa kiurahisi kapigana na kuweza
kufanikiwa kwa mafanikio yale.
Lakini
ukiwa na ndoto za kufanikiwa huku umelala, na bila kijibiidisha vya kutosha andika
utaumia hutaweza kufanikiwa popote.
Amua
kwenye maisha yako kutenga muda wa kutafuta mafanikio yako, kubali kupigika
kiakili, kimwili lakini usikubali ukashindwa kufanikiwa.
Unajua
dunia tunayoishi ina kila kitu cha kukupa mafanikio. Kinachosababisha ukose
mafanikio ni juhudi na nguvu zako tu na sio kitu kingine.
Kama
unataka mali na pesa hizo zipo, lakini sio rahisi kuzipata, unatakiwa uweke
juhudi na kufanya kazi kwa nguvu zote na kuachana na mchezo mchezo.
Kama
utacheza na huku unasema unatafuta mafanikio makubwa, nikwambie tu ukweli huo ni
uongo, ambao tena labda unajidanganya wewe na kuwadanganya na wengine pia.
Elewa
hauna kitu ambacho cha kimafanikio ni rajisi katika maisha yako, ipo nguvu ambayo
unatakiwa kuitumia ili kupata kitu chochote kile.
Chochote
kile ambacho kinakupa mafanikio au chochote kile ambacho kinabadili tabia au
hali yako na kuwa bora si rahisi sana kukipata.
Kama
unafikiri mafanikio utayapata kwa njia ya urahisi, sahau. Unatakiwa kuweka
juhudi kwa nguvu zako zote.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com.
Oct 30, 2017
Kama Utazingatia Hatua Na Mawazo Haya, Tayari Umefanikiwa.
Siku zote ieleweke hivi,
kama unarudia mawazo yako, kama unarudia hatua fulani hivi mara kwa mara ni
wazi utakuwa bora sana kwa hicho unachokirudia kila wakati.
Haijalishi kitu gani
unachokirudia sana kwenye mawazo yako yaani unakifikiria sana ila kitu hicho
kitakuwa sehemu ya maisha yako kama utafanya hivyo sana.
Haijalishi ni hatua zipi
utakuwa unazirudia sana kwenye maisha yako ila hatua hizo zitakua matokeo ya
kitu fulani hivi kwenye maisha yako.
Ikiwa utatenga muda na masaa
kadhaa kwa wiki kufikiria na kutenda jambo lolote lile katika maisha yako, uwe
na uhakika jambo hilo utalivuna.
Kwa mfano, ukiona una maisha
mabovu au una maisha mazuri ujue ni mwendelezo wa mawazo fulani ambayo ulikuwa
nayo kwa siku za nyuma.
Mawazo yapi uliyonayo kwa
muda mrefu, ni hatua zipi ulizonazo kwa muda mrefu hizo ndio hatua zinazokupa
matokeo ya kitu fulani kwenye maisha yako.
Hauhitaji sana kumtafuta mtu
pengine anayefanya maisha yako mabaya, kama iko hivyo kweli, ila unachotakiwa
kufanya ni kukagua hatua na mfumo wa mawazo yako ukoje.
Wakimbiaji wote duniani wanaelewa vyema kabla hujawa mshindi katika
mbio lazima ufanye mazoezi mengi sana yatakayokufanya uwe mshindi.
Kuna wakati itakutaka
ukimbie mbio za muda mrefu zaidi ya mashindano unayochukua na tena mara kwa mara
hadi uweze kushinda.
Kuwa mshindi katika mbio kwa
wakiambiaji wanajua kabisa sio swala la mara moja bali ni swala linalochukua
mazoezi karibu ya kila siku.
Halikadhalika, hata washindi
katika maisha ni watu ambao wanajuhudi endelevu
za kila siku kwenye maisha yao. Kitu hiki leo kikikataa kuna kingine
kitafanyika hadi kieleweke.
Hivyo hata kwako inatakiwa
ieleweke mawazo yanayojirudia mara kwa mara akili mwako, hatua zinazojirudia
hizo ndizo zinazokupa mafanikio yako.
Mafanikio yako yanajengwa
hatua kwa hatua, unatakiwa kujua hata kama hatua unazo chukua ni kidogo lakini
hatua hizo zipo na ipo siku zitakufanikisha.
Una uwezo wa kufanya maisha
yako kuwa bora zaidi ikiwa utakuwa na mawazo na hatua bora zinajirudia akilini
mwako kila wakati.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com.
Oct 29, 2017
Acha Kuendelea Kufanya Kosa Hili Tena Na Tena Unapotafuta Mafanikio Yako.
Kati ya kosa ambalo hutakiwi
kuendelea kulifanya kwenye maisha ni kufanya vitu au mambo yako kwa kuingia na
mawazo ya kujaribu.
Hili ni kosa kubwa ambalo
linawangusha wengi wanaposema wanataka kufanya kitu fulani halafu wanasema hebu
ngoja ni jaribu.
Unajua unaposema najaribu
maanake nini? hiyo ina maana hicho kitu ambacho
unakifanya kwanza huna uhakika nacho kama utakiweza.
Kwa hiyo unapojaribu,
usitegemee kama kuna ushindi wowote unaweza ukatokea, maana wewe si unajaribu.
Wale wote wanaojaribu sio
rahisi kuweza kufanikiwa kupata ushindi, kwa sababu akili na kila kitu kinakuwa
kimekaa kwa kujaribu jaribu.
Unapotaka kufanya jambo
halafu ukaingia na mawazo ya kujaribu, kwanza hata ukishindwa unakuwa hauna
uchungu sana, kwa sababu utasema ulikuwa unajaribu.
Pia hata hivyo, utakuwa ni
mtu ambaye una sababu hata kama
ukishindwa, lazima utasema tu si nilikuwa najribu tu sio nilikuwa nafanya
kabisa.
Kwenye maisha hakuna uwanja
wa majaribio hata siku moja. Kama unafanya kitu au vitu vyako kwa kujaribu unajipotezea
muda wako bure na unajidanganya.
Ikiwa kama kuna vitu umeamua
kuvifanya, jitoe kufanya vitu hivyo kwa ukamilifu wako wote lakini sio kufanya
majaribio.
Wakati wewe utaendeleakuendeleza
wimbo wa kujaribu, wapo watu ambao wamejitoa kufanya kweli kwenye maisha yao na
hawajaribu.
Najua hili ni kosa ambao
umekuwa ukilifanya sana na limekuwa likagharimu maisha yako lakini si wakati wa
kuweza kurudia tena.
Kimefika kipindi cha kusimamia
ndoto zako, kimefika kipindi cha kuhakikisha ndoto zako zinaweza kutimia na
kuwa kweli.
Jaribu kujiuliza utaendelea
kujaribu mpaka lini? Jipe muda wa kufanya mambo yako, achana na habari ya
kujaribu maisha hayakusubiri hata kidogo.
Washindi katika maisha ni
watu wa kufanya na si watu wa majaribio. Chagua kufanya kitu hata kama ni kidogo
sana lakini kifanye na usijaribu hata kidogo.
Kujaribu mara nyingi
kunakuandalia mazingira ya wewe kuweza kushindwa moja kwa moja. Hakuna
mafanikio utakayoweza kuyapata kwa kuishi maisha ya kujaribu.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Oct 28, 2017
Huu Ndiyo Ujasiri Unaotakiwa Kuwa Nao Ili Kuzishinda Changamoto Zako Mara Moja.
Haijalishi
maisha yako uliyonayo yakoje, yaani ya mafanikio sana au ya kushindwa
sana, lakini jambo ambalo ni lazima utakutana nalo kila wakati ni changamoto.
Changamoto
katika maisha zipo kwa kila mtu, haziangalia hali ya kipato au kitu chochote, changamoto
zipo na zinatofautiana.
Ujasiri
unaotakiwa kuwa nao ni kuzishinda changamoto hizo na kuamua kuweza kusonga
mbele bila kujali ukubwa wa changamoto hizo.
Lakini
ikiwa kila wakati utaamua kutulia na kuchelewa kutatua changamoto zako mapema,
ujue unaongeza changamoto zingine tena.
Kivipi,
sikiliza, kila ukiona unachangamoto ya aina fulani, ujue kabisa nyuma yake ipo
changamoto nyingine ambayo unatakiwa uivuke na kuifanikisha.
Ukiona
unakutana na changamoto halafu unajipa muda kwamba utaitatua baadae, ujue basi
kabisa unakaribisha changamoto zingine nyuma yako.
Kila
unapokutana na changamoto, unatakiwa ujue nyuma yake ipo changamoto nyingine,
hivyo unatakiwa kuitatua changamoto uliyonayo haraka maana nyingine zitakuja
tu iwe unataka au hutaki.
Uwezo
wako wa kutatua changamoto haraka ndiyo utakao kufanya uzidi kuwa mshindi. Hakuna
anayeomba kukutana na chagamoto, lakini changamoto zipo na zinataka majibu.
Zipo
changamoto katika fursa tunazokutana nazo na pia zipo changamoto tofauti tofauti
tunazokutana nazo kwenye maisha, hizi zote tunatakiwa kuzitatua.
Ikiwa
unakutana na changamoto, kisha unasema utakuja kuzitatua kwa wakati fulani, wewe
elewa kabisa utakuwa unakaribisha changamoto zingine zaidi.
Kitu
ninachotaka uelewe hapa ni kwamba kila unapokutana na changamoto, itatue haraka
changamoto hiyo kabla changomoto nyingine haijakufikia.
Ujasiri
unaotakiwa kuwa nao katika changamoto ni kuamua kuzikabili changamoto zako na
si kuzipa nafasi ya baadae kwamba utazitatua kesho au siku nyingine.
Kujipa
muda kwamba changamoto zako utazitatua wakati mwingine huko ni sawa kuamua sasa
kwamba changamoto zako zikumalize.
Na kwa
bahati mbaya sana unaweza ukaona ni kitu cha kawaida tu kwako kuahirisha changamoto,
lakini changamoto hizo zikizidi ndio utajua umuhimu wa kutatua changamoto
haraka sana.
Ukumbuke
hata mafanikio yanakuja si kwa sababu hakuna changamoto, bali mafanikio
yanapatikana kwa kutatua changamoto zako mapema sana.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Oct 27, 2017
Kipe Kipaumbele Kitu Hichi Kikupe Mafanikio.
Hivi
umeshawahi kujiuliza au unajua ni kitu gani ambacho ni cha muhimu sana kwenye
maisha yako? je, ni afya, familia, imani yako au ni kitu gani?
Iwe kwa
kujua au kutokujua kwa kawaida kipo kitu cha muhimu sana karibu kwa kila mtu
kwenye maisha yake. Kitu hicho ndicho kinacho ongoza maisha ya mtu huyo.
Hata
hivyo pia, kila siku maisha yanatuuliza kitu cha muhimu kwetu, na kwa bahati
nzuri tunajibu kupitia vitendo vyetu na si midomo.
Kwa mantiki
hiyo, hata nikikuuliza kitu kipi cha muhimu kwako hata usiponijibu najua
vitendo vyako vitanijibu vizuri sana kuliko maneno yako.
Zipo
namna nyingi amabazo zinaweza kukusaidia kujua kipi ni cha muhimu kwako au
kwenye maisha yako na kipi si cha muhimu.
Unaweza
kujua kitu cha muhimu kwako kwa kuangalia jinsi unavyotumia muda wako kufanya
jambo fulani hivi.
Ikiwa
muda wako umeutenga kufanya jambo fulani na kila siku na jambo hilo unalifanya na huachi basi hicho ni
kitu cha muhimu sana kwako na kina matokeo.
Chochote
kile unachokipa muda wako mwingi hicho ndicho kitu cha muhimu bila kujali kitu
hicho kina faida au hakina.
Inawezekana
kabisa kitu cha muhimu kwako ikawa ni maongezi au kufatilia habari na
inawezekana pia kitu cha muhimu kwako ikawa ni kufatilia ndoto zako.
Kitu
kipi kitakachotufanya tujue kitu kipi cha muhimu kwako ni kwa jinsi wewe unavyotenga
muda wako kwenye kitu hicho kila wakati.
Ukumbuke
kitu cha muhimu kwako inaweza ikawa hata kuimba, kuangalia mpira ila kama kina
kula muda wako basi hicho ndicho kitu cha muhimu kwako.
Maisha
yako yako hivyo kutokana na kuna vitu ambavyo ulivipa umuhimu hivyo vitu ndivyo
vimefanya uwe na maisha hayo.
Sasa
ikiwa ulikuwa unatumia muda wako mwingi kwa vitu vya hovyo hovyo itakugharimu
na kwa sababu havijakusaidia kitu.
Kuanzia
leo, anza kufanya vitu vya muhimu kwako ili vikusaidie kukupa mafanikio bora
leo na kesho kwenye maisha yako yote.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Oct 26, 2017
Hatua Muhimu Za Matunzo Kwa Kuku Wanaokua.
Katika matunzo ya kuku wanaokua, hapa tunaangalia mitemba au
kuku wenye umri wa kuanzia miezi miwili hadi minne. Kuku hawa wenye umri huu
wanatakiwa watunzwe vizuri ili wakusaidie kukupa mfugaji faida, vinginevyo
ukishindwa hapa kutunza kuku wako vizuri basi usitegemee kupata faida kubwa.
1. Hatua ya 1, waweke
kwenye banda kubwa.
Hatua hii inakuja kama walikua bado kwenye eneo la kulea
vifaranga, wahamishe na uwapeleke kwenye banda kubwa. Kama banda ni hilo
hilo moja, waondolee ‘hardboards’
ulizokuwa umetengea vifaranga, na waachie kwenye banda zima.
2. Hatua ya 2, wawekee
bembea kwenye banda.
Ukumbuke kwamba kuku ni ndege, hivyo kuna wakati wanapenda kuwa
juu. Hivyo ni muhimu kuwawekea bembea ili iwasaidie kufurahia maisha yao na
kuwa huru zaidi. Hiyo itakuwa ni sehemu mojawapo ya kufanya zoezi.
3. Hatua ya 3, weka matandazo safi.
Hakikisha matandazo yasiwe na harufu kali au vumbi. Hakikisha
pia maji hayamwagiki bandani. Na
Mara tu yakimwagika ondoa matandazo yaliyolowa na weka mapya. Pia ukumbuke
kubadilisha matandazo mapema ili yasiweze kutoa halafu na kuleta magonjwa
mengine yatakanayo na matandazo kurundikana.
4. Hatua ya 4, weka
ratiba ya usafi.
Unaweza ukaweka ratiba ya usafi bandani na kwenye eneo la
kuzunguka banda, angalau mara mbili kwa wiki. Tumia dawa ya V-RID kufanyia
usafi na kupulizia dawa hewani. Hii itasaidia banda lako kubaki safi wakti wote
na afya kwa kuku wako pia.
5. Hatua ya 5, wape
kuku maji safi muda wote.
Pia unaweza kuwaongezea vitamin kwenye maji yao hasa kama
wanafugwa ndani muda wote. unapowapa maji safi muda wote si rahisi sana kuweza
kupata magonjwa yatokanayo na bakteria.
6. Hatua ya 6, wape
chakula chenye virutubisho.
Usiwape kuku wako ilimradi tu chakula, wape kuku wako chakula
chenye virutubisho vya kutosha. Unaweza ukaanza kuwapa ‘growers’ au aina nyingine
ya chakula kizuri. Ukiwalisha kuku wako chakula duni, wanadumaa.
7. Hatua ya 7, rudia
chanjo ya newcastle kwa wakati.
Hii unaweza kufanya yaani kila baada ya wiki 10 tangu
walipochanjwa mara ya mwisho. Unaporudia chanjo inasaidia sana kuwafanya kuku
wako wawe imara wakati wote na inakuwa ngumu kukutana na magonjwa.
8. Hatua ya 8, wape
dawa ya minyoo.
Dawa ya minyoo unawapa kuku wakiwa na miezi miwili na rudia kila
baada ya wiki 10. Ukishindwa kuwapa dawa hii basi tegemea kuokota kuku wengi
ambao watakufa kutokana na kushambuliwa na minyoo.
9. Hatua ya 9, walishe
majani na mboga mboga kwa wingi.
Unapowalisha kuku majani ya mboga mboga hiyo itawairishia miili yao
kwa kuiongezea kinga dhidi ya magonjwa. Hata hivyo kama kuku wakilishwa majani
ni rahisi pia kuweza kutaga vizuri inapofikia kipindi hicho.
10. Hatua ya 10, kama
una eneo kubwa, wafungulie nje ili wazunguke zunguke.
Waache kuku wako wazunguke na waoge kwenye mchanga. Kuzunguka
zunguka na kuparua parua kunawafanya bize na kudonoana na kulana manyoya. Kuoga
kwenye mchanga kunawafanya wawe safi na kama wana wadudu, wanaweza kuwaondoka.
11. Hatua ya 11, kuwa
na mawasiliano ya karibu na daktari wa mifugo.
Mara tu uonapo dalili za ugonjwa, wasiliana na daktari wa mifugo
kwa ushauri zaidi. Pia tafuta chanzo cha ugonjwa ili ukiondoe.
Mwisho wa somo letu la leo na tunaamini umejifunza kitu cha
kukusaidia kuboresha ufugaji wako.
Pia kama wewe ni mfugaji wa
kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO na KIENYEJI ASILIA. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote mnakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika
mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Oct 25, 2017
Mbinu Bora Ya Kuishi Ndani Ya Bajeti Yako.
Hivi
falsafa juu ya matumizi ya bajeti ambayo
ipo ndani ya uwezo wako ikoje? Hili ni
swali la muhimu sana ambalo kila mmoja wetu anatakiwa kujiuliza kataka maisha
yake ya kila siku. Nasema hivi kwa sababu moja kati ya tabia ya watu wengi huwa
wanaishi nje ya bajeti ambayo wanakuwa wamepanga.
Yote
hii hutoka na sababu kubwa moja, sababu hiyo ni pale mtu ambapo amepata fedha
nyingi kwa wakati mmoja. Kitendo hicho ndicho ambacho humfanya mtu kuweza
kuishi nje ya bajeti yake ya kila siku.
Kwa
mfano mtu akipokea mshahara hawezi kuishi maisha ambayo alikuwa ameyazoea
ukifananisha na alipokuwa hana pesa, unakuta matumizi yanakuwa mengi kuliko
pesa aliyonayo. Wapo wengine mara baada ya kutumia pesa yote hujikuta wanaingia
kwenye madeni yasiyo ya msingi.
Achilia
mbali madeni, wapo baadhi ya watu pindi wapatapo pesa utakuta wananua vitu
vingi hata ambavyo hawakupanga kununua, tatizo hili lipo kwa watu wengi sana,
siwezi ita tu ni tatizo bali ni ugonjwa wa matumizi ya pesa.
Niliwahi
soma kitabu kimoja cha kanuni ya pesa, ndani ya kitabu hicho mwandishi anasema
ya kwamba ukimpa mtu maskini pesa basi ndani ya sekunde kadhaa basi jiandae
kujua tabia za mtu huyo, hii ni kwasababu ni mtu ambaye mara zote huongozwa na
pesa, basi kila kilichopo mbele yake anataka kukimiliki yeye.
Lakini
pesa hiyo ukimpa mtu ambaye anaelewa ni nini maana ya pesa, basi pesa
hiyo huweza kufanya kitendo cha uwekezaji, ili pesa hiyo iweze kujizalisha
yenyewe hapo baadae. Kwa nukta hiyo jaribu kutafakari hivi pesa ambayo huwa unaipata mikononi mwako unajiona upo kundi gani kati ya hayo
niliyoyaeleza?
Kama
utaona ya kwamba upo kundi ambalo umekuwa ni mtumiaji mzuri kuliko kuwa mwekezaji
basi tambua lipo tatizo kubwa ndani yako, ambalo linakufanya uishi nje ya
mstari wa bajeti yako, Hivyo unatakiwa kujua ni kwa namna gani unatakiwa kuishi
ndani mstari bajeti yako kwa kuzingatia jambo hili.
Jambo
Kwanza kabisa hakikisha pesa isikupelekeshe hasa pale unapoipata ila wewe ndiyo
unatakiwa kuipelekesha pesa, kwa kuzingatia ya kwamba pindi utakapo ipa nafasi
pesa ikuendeshe basi tambua fika lolote
linaweza kutokea ndani yako.
Lakini
pia kwa kuwa wanasema pesa ina makelele
sana hasa pale unapoipata hivyo hakikisha pale unapoipata pesa unaishi kwenye
pajeti yako ambayo umeizoa, kwani pindi utapopandisha bajeti yako eti kwa
sababu umeipata pesa basi tambua ya kwamba
utaunganaa na wale wanaosema vyuma vimekaza.
Hivyo
pesa isiongeze matumizi yako ya kila
siku eti kwa sababu umepata pesa, hivyo kila wakati jifunze kuishi ndani ya
bajeti yako.
Ndimi; Benson Chonya
Oct 24, 2017
Kitu Hiki Ndicho Kitakachokufanya Ukue Sana Kimafanikio.
Kitu
chochote kinachokupa changamoto wewe, ni kitu hicho hicho ndicho kinachokufanya
ukue na ujenge ukomavu kutokana na changamto unazopitia.
Unapokuwa
unakutana na changamoto hizo, uwezo wako wa kutenda unaongezeka na unakuwa ni
mtu mwingine hata mara baada ya kuvuka changamoto hizo.
Mara
nyingi changamoto zinapoanza na kutokea kwenye maisha ya mtu ni mbaya sana,
lakini kwa kiasi kikubwa zinasaidia kumpa mtu ukomavu.
Kwa
mfano, kama unatembea kawaida huwezi kuwa sawa na yule anayepanda milima. Kwa
vyovyote mpanda mlima ni rahisi kujenga misuli mikubwa ya mwili kuliko
asiyepanda.
Changamoto
ipi inayokukabili wewe? Changamoto hiyo kumbuka ndiyo inayokupa uzoefu na
ukomavu mkubwa utakao kupa mafanikio yakutosha.
Watu
wote wenye mafanikio makubwa, watu ambao ukiwaangalia wamefika mbali sana kimafanikio
ni watu ambao wanapambana sana na changamoto kwenye maisha yao.
Huwezi
kufanikiwa na kufika juu sana kwenye mafanikio yako kama wewe ni mtu wa
kutoroka au kukimbia changamoto kila wakati.
Unatakiwa
ufike wakati ujue ni kwa jinsi gani utakavyoweza kukabiliana na changamoto ili
ziweze kukupa ushindi wa kimafanikio.
Changamoto
kwenye mafanikio ni silaha au njia nzuri sana ya kuweza kukusaidia wewe kuweza
kufanikiwa au kufika mbali kimafanikio.
Ulimwengu
una changamoto sana, ni changamoto hizo ndizo ambazo ukijua namna ya kukabiliana
nazo zitakupa mafanikio makubwa sana.
Hakuna
namna au hakuna mtu ambaye ana uwezo wa kuzikimbia changamoto. Uwe una pesa au
huna, changamoto katika maisha zipo palepale.
Acha
kuwaona watu wengine ni kama watu ambao maisha yao mazuri sana hayapitii kwenye
changamoto zozote, changamoto kila mtu anazipitia na ndizo ziletazo mafanikio.
Kuwa
miongoni miongoni mwa watu ambao wataamua kukua kutokana na changamoto wanazo kabiliana
nazo kila siku.
Lakini
ikiwa kila unapokutana na changamoto unalalamika sana au unaamua kukimbia
kufanikiwa kwako itakuwa ni vigumu.
Washindi
katika maisha wanakumbana na changamoto nyingi sana ambazo mwisho wa siku
huwaacha wakiwa washindi kutokana na kuzishinda changamoto hizo.
Kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa
kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote manakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Oct 23, 2017
Jiandae Kwa Hiki Ili Kufanikiwa Katika Kila Jambo.
Ili
kuweza kufanikiwa katika jambo lolote kwenye maisha yako unahitaji kuwa na UJASIRI. Unahitaji kuwa na ujasiri wa
kushinda hofu zako na pia unahitaji kuwa na ujasiri wa kushinda changamoto
zozote zile zinazozojitokeza mbele yako.
Na
ujasiri tunaouzungumza hapa hauji kwa bahati mbaya, ujasiri huo unakuja
kutokana na maandalizi muhimu ambayo unatakiwa uyafanye. Hautaweza kuwa jasiri
kama huna maandalizi ya muhimu kwako.
Inawezekana
unaanza kujiuliza ujasiri huo utaujenga kwa vipi? Sikiliza, na twende kwa
mfano. Mwanafunzi ambaye amejiandaa vizuri kwa kusoma kabla ya mtihani, huyu
anakuwa hana wasiwasi sana tofauti na
yule mwanafunzi ambaye hakusoma kabisa.
Halikadhalika
wale wanaoongea mbele za watu alimaarufu ‘public
speaker’ ambaye kabla ya kwenda kuongea usiku alifanya mazoezi, atakuwa ana
ujasiri tofauti na yule ambaye hakuweza kufanya mazoezi na kuamua kwenda tu
kuongea.
Hata
katika maisha na mafanikio yako, unahitaji kuweka maandalizi ya nguvu ili kuwa
na ujasiri na kufanikiwa. Maandalizi haya utayapata tu kwa wewe kuamua kufanya
kazi kwa bidii na nguvu zote.
Kufanya
kazi kwa juhudi na nguvu zote ndio kutakapokupa ujasiri wa kuweza kushinda hofu
na kila aina ya woga ambao unakukabili.
Watu wote ambao hawana hofu sana katika maisha ukiwatazama vizuri ni wachapakazi.
Ni
wazi tu, hofu hiyo wanakuwa hawana na badala yake wanakuwa ni majasiri, unajua
ni kwa sababu gani, ni kwa sababu wanakuwa wanajua hata mambo yagome vipi kwao
hakuna kitu kitakachoweza kuharibika kwao.
Si
jambo la kujiuliza sana unapokuwa unashindwa kuwajibika au kuchapa kazi kwa
juhudi sana elewa tu kwa namna yoyote utaanza kukosa ujasiri na mwisho wa siku
woga mwingi wa maisha yako utaanza kukuvaa.
Fanya
wajibu wako. Fanya kazi kwa bidii sana bila kujali kazi unayoifanya ni ya aina
gani na kwa kufanya kazi kwako huko utajikuta ukiwa ni mtu ambaye unavuta
mafanikio kwa kiasi kikubwa sana kama sumaku.
Ujasiri
ni kitu cha muhimu sana katika mafanikio yoyote yale. Kumbuka kama nilivyoanza
kwa kusema bila kuwa na ujasiri huwezi kufanikiwa hata ufanyaje, zaidi
utaendelea kubakia na maisha yako hayo.
Kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa
kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO na KIENYEJI ASILIA. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote mnakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Oct 22, 2017
TANGAZO MAALUM; Mashine Za Kutotoleshea Mayai(Incubators) Zinazotumia Solar power au Betri, Zinapatikana Hapa.
Mashine itumiayo betri/solar power kwa ajili ya kutotoleshea mayai. |
DM POULTRY FARM PROJECT kwa sasa mbali na mashine tulizonazo za kutotoleshea vifaranga,
kwa sasa tunauza pia mashine za kutotoleshea mayai (incubator) zinazotumia SOLAR POWER AU BETRI YA GARI.
Mashine zetu hizi zina
ubora wa kiwango cha hali ya juu na zinaweza kutumia umeme, solar power au
betri ya gari. Kama umeamua kutumia umeme ni uamuzi wako ila umeme ukikatika
unatumia betri yake maalum.
Vile vile mashine zetu
hizi mpya ni 'full automatic,' yaani
zinafanya kazi kwa kujitegemea. Kwa maana hiyo zinafanya kazi katika mazingira
yoyote yale iwe kijijini ambako hakuna umeme au mjini, kote ni sawa.
Karibu sana ujionee mashine zenye ubora na zenye
viwango tofauti na ukubwa tofauti kutegemea na matumizi yako. Mashine hizi tunazo za mayai 45, 90, 180, 240, 300 na 500.
Huhitaji kulalamika kwamba sina
umeme, jibu la changamoto yako sasa limepatikana ikiwa utanunua mashine zetu.
Kwa maelezo zaidi au mawasiliano kuhusu oda yako, piga
simu kwa namba 0767 04 80 35 na wote mnakaribishwa.Mashine ikiwa ofisini kwetu tayari kwa kuuzwa. |
Oct 21, 2017
Siri Ya Kupata Zaidi Kile Ukitakacho.
Ni tabia au asili ya
binadamu kila anachokipata kutaka kukipata zaidi na zaidi. Hapa yaani binadamu
anakuwa ana shauku ya kupata kwa wingi zaidi.
Tabia au asili hii wewe unayo
na mimi ninayo na kila aliye binadamu ili mradi anahema tu tabia hiyo anayo na
anaitumia pia.
Kinachokuja kutofautisha ni
matakwa ya utakaji wa vitu hivyo. Utakuta kila mtu anapenda kitu ambacho ni
tofauti au hakifanani sana na mwingine ili kiwe kingi.
Kwa mfano, wapo wanaopenda
wawe na mali au pesa kwa wingi, wapo pia wanaopenda wawe waimbaji wazuri na
bora kabisa.
Pia wapo wale wanaopenda
kupata idadi kubwa ya watu wanaowafatilia/ ‘followers’
hasa wasanii na wale watu ambao ni watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii.
Kila mtu kama nilivyosema
kipo kitu ambacho anataka kiongezeke na kuwa kingi kabisa na kutokana na hilo,
hufanya kila linawezekana kukiongeza kitu hicho.
Kutaka kile ulichonacho
kiendelee kuongezeka sio jambo baya ni jambo zuri, lakini badala ya kuwa na
shauku hiyo tu peke yake, unachotakiwa kufanya, ongeza juhudi.
Unajiuliza uongeze juhudi
wapi? Ongeza juhudi ya kufanya zaidi kwa kile kitu ulichonacho au unachokifaya
ili kikusaidie kupata mambo mengine zaidi.
Najua vizuri sana kuna kitu
fulani unakifanya, kitu hicho kinaweza kikawa kidogo na kisikupe hamasa sana,
lakini unatakiwa kuongeza juhudi ili kujenga mafanikio zaidi.
Hakuna kitachoweza
kukusaidia kupata kitu unachokitaka kwa wingi zaidi kama hutaweka juhudi kwa
unachokifanya. Juhudi yako itakupa matunda.
Ila kama unafikiri kila
wakati unataka zaidi, kiuhalisia utaanza kujiona huna kitu kabisa, utaanza
kuona maisha yako yapo tupu na huna kitu kabisa.
Ndio maana nasema unataka
kupata kitu zaidi weka juhudi kwa unachokifanya ili kikusaidie kupata zaidi na
zaidi.
Kuendelea kufikiri makubwa
unayotaka bila kuweka juhudi utakuwa unatengeneza nguvu za kukufanya wewe mwenyewe
ukashindwa kufikia malengo yako.
Acha kuendelea kuweka nguvu
za mawazo yako kwa yale mambo ambayo hauna, weka juhudi kwa kile ukifanyacho,
nguvu hizo zitakupa mambo makubwa.
Kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei
nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT
kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO na PURE KIENYEJI. Kwa
mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767
048 035 au 0686 141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote
mnakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)