Oct 19, 2017
Kama Utang’ang’ania Sana Mpango Huu, Huwezi Kufanikiwa.
Mafanikio
mara nyingi sio rahisi kuweza kuja moja kwa moja kama vile ambavyo mipango yako
uliojiwekea awali jinsi ilivyo.
Si ajabu
sana utakuta unapanga kufanya kitu hiki au kile na kuwa na uhakika kabisa
unafanikiwa, lakini unashangaa mambo yanaingiliana na unashindwa kutimiza
lengo.
Ndio
maana ili kufikia mafanikio yako unatakiwa kupanga kwa umakini sana hatua
unazotakiwa kuchukua ili kufanikiwa, lakini pia unatakiwa uwe tayari
kubadilika.
Ikiwa
wewe mipango yako uliyoiweka au ambayo umeipanga kwamba hii ndiyo itakusaidia
kuweza kukufanikisha ukaamua kuipanga kwa kuimiminia zege huwezi kufanikiwa.
Ninaposema
kuimiminia zege ni kuweka mipango ambayo huwezi kuibomoa tena, kwamba ulichosema
ndicho hicho na hakiwezi kubadilika.
Kama
utakuwa na mipango ya kukufikisha kwenye mafanikio ya namna hiyo, mipango hii
itakuchukua muda sana kuweza kuifikia.
Kila
kitu kinabadilika, hata mipango ambayo unakuwa unapanga haiwezi kukufikisha
kwenye ndoto zako, pia inaweza ikabadilika lakini sio swala la kuing’ang’ania
sana.
Unatakiwa
uelewe mipango uliyoiweka sio malengo yako, hio ni mipango tu unaweza
ukaibadilisha na kufuata mpango mwingine bora.
Ni
sawa na wewe uwe unataka kwenda mjini na gari lako halafu gari likaharibika, je
jiulize hutaweza kwenda mjini mpaka gari lako lipone, sina shaka hapana.
Najua
tu hapa utaamua kutumia njia nyingie ikiwa pamoja na hata kuita teksi ili
ikufikishe kule unakotaka kufika na kwa ule muda ulioupanga na sio kuendelea
kubakia hapo.
Ikiwa
wewe utaendelea kung’ang’ania mpango wako wa awali ukusaidie kufanikisha tu hata
kama ni mbovu basi utakuwa ni mtu ambaye umeamua kuchagua njia ndefu sana ya
kufanikiwa kwako.
Unachotakiwa
kujua ni kwamba mpango wako mmoja unapokataa, uwe na mpango mwingine mbadala wa
kuweza kukusaidia wewe kufikia ndoto zako.
Kuwa
na mpango mmoja tu ambao unasema unaamini na kuamua kuziba masikio na kuacha
kila kitu hii ni hatari kubwa sana kwako.
Badilika
kulingana na mazingira, na pia unatakiwa kubadilika kulingana na wakati wa
utekelezaji wa ndoto zako.
Ikiwa
hautafanya hivyo andika utashindwa tu. Usikubai kutumia njia ndefu kufikia
mafanikil yako kwa kung’ang’ania pengine mpango mbovu kwako, UTAKWAMA.
Kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei
nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT
kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh.
1800/=. Wote manakaribishwa.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.