Oct 3, 2017
Ili Kuzishinda Changamoto Za Kimaisha, Kijue Kwanza Kitu Hiki…?
Vitu
vinabadilika. Watu wanabadilika. Sheria zinabadilika. Mazingira yanabadilika
pia. Mabadiliko yapo kila wakati na kila mahali. Kile ulichokiona jana, leo hakipo
hivyo na kesho pia hakitakuwa hivyo kwa sababu ya mabadiliko.
Fikiria
wale watu unaowajua. Je, unafikiri ni watu wale wale kama ulivyokuwa ukiwajua
mwanzo na wanaendelea na maisha na mienendo ileile? Sina wasiwasi, lazima yapo
mabadiliko kwa watu hao.
Jaribu
kufikiria tena, mambo ambayo umeyabadilisha wewe mwaka mmoja nyuma, kama unaona
yapo mabadiliko ya aina fulani, basi yote hiyo inaonesha kwamba mambo
yanabadilika kwenye maisha kila kukicha.
Kumbuka
mabadiliko yapo, hata wewe unabadilika pia. Ikiwa utakuwa ni mtu wa kukataa
mabadiliko, basi changamoto za maisha zitakusumbua sana. Unatakiwa uendane na
mabadiliko ili kuzishinda changamoto za kimaisha.
Watu
ambao hawabadiliki, watu ambao hawataki kuendana na mabadiliko, sio rahisi
sana kupiga hatua. Maisha yao yako vile vile miaka nenda rudi, tena zaidi yanakuwa
magumu sana.
Nakumbuka
kuna watu ambao nawafahamu tokea nipo kidato cha kwanza, zaidi ya miaka 15
nyuma, watu hao maisha yao yako vile vile, nikiwa na maana shughuli wanazofanya
ni zile zile, ambazo haziwafikishi mbali.
Kitu
gani kimetokea kwa watu hawa hadi kuwa na maisha yale yale ambayo hayabadiliki
kwa zaidi ya miaka 15, si kingine bali kugomea mabadiliko. Ni kitu hatari sana
kama hujui umuhimu wa mabadiliko maishani mwako.
Hebu
jiulize mimea inabadilika, dunia inabadilika kila siku, kipi kinachokufanya
usishutuke na kuamua kubadilika? Kuendelea kubakia vile vile na kutokufanya
mabadiliko yoyote kwenye maisha yako ni kujiweka kwenye hatari kubwa sana.
Kila
siku unatakiwa uwe mpya, kila siku unatakiwa kubadilka kwa kujifunza vitu
vipya. Usipobadilika uwe tayari kuachwa nyuma tena mbali sana na hali ambayo
itasababisha maisha yako yarudi nyuma sana.
Hakuna
mtu ambaye ni mpinga mabadiliko halafu akafanikiwa. Watu wote ambao hawataki
kufungua akili zao na kuamua kubadilika ni watu wa kukwama sana maishani mwao
karibu kwenye kila kitu wakifanyacho.
Hutakiwi
kuionea huruma akili yako linapokuja swala la mabadiliko katika maisha yako. Kwa kawaida akili yako haitaki shida
sana, akili inapenda ipate vitu vya kuburudisha na ndio maana mabadiliko
yanakuwa magumu kwako kutokea.
Huhitaji
kumtafuta ‘mchawi’ wa mtu aliyefanya
maisha yako kuwa mbaya leo, ‘mchawi’
wa kwanza ni wewe. Anza kufanyia kazi mabadiliko yanayojitokeza maishani mwako
ili ujenge maisha ya mafanikio makubwa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.