Oct 15, 2017
Makosa Wayafanyayo Wafugaji Kabla Ya Kuingiza Vifaranga.
Yapo
makosa ya wazi ambayo baadhi ya wafugaji huyafanya wakati wanapoagiza
vifaranga. Haya ni makosa ambayo hutakiwi kuyafanya mara kwa mara ukiwa mfugaji
kwani ukifanya yatasababisha kuku wako wengi kufa.
Ni matumaini
yangu kuwa kusoma makala haya utajifunza makosa haya na kuyaepuka kabisa na
kufanya ufugaji wenye tija kwako.
1.
Kutokuwa na ratiba ya kufanya usafi na maandalizi mengine ya banda mapema
2.
Kununua vifaranga kabla hujamaliza kujenga banda.
3.
Kutokuwakagua vifaranga kule unapowachukua kama wana kinyesi kilichoganda.
4.
Kutokutunza chakula vizuri, na kuacha chakula kikaliwa na panya, ambao wanaweza
kukichafua na kuwasababishia magonjwa vifaranga.
5.
Kujenga banda dogo sana ambalo ni vigumu kulifanyia usafi.
6.
Kununua vifaranga vingi kuliko eneo la banda lako.
7.
Kuchukua aina ya kuku ambayo haiendani na hali ya hewa ya eneo ulilopo.
8.
Kutokuandaa dawa za mwanzo za vifaranga.
9.
Kutotumia dawa ya kuua wadudu na bakteria wakati wa kusafisha banda.
10.
Kutokupata elimu ya kutosha juu ya ufugaji vifaranga vya kuku.
11.
Kuandaa banda la vifaranga lililofungwa sehemu zote, yaani hewa haizunguki.
12. Kutoziba
mashimo na matundu, kuacha mlango wa banda wazi, hivyo panya, paka, mbwa na
vicheche wanaweza kuingia.
Pia kama wewe ni mfugaji wa
kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote manakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.