Oct 26, 2017
Hatua Muhimu Za Matunzo Kwa Kuku Wanaokua.
Katika matunzo ya kuku wanaokua, hapa tunaangalia mitemba au
kuku wenye umri wa kuanzia miezi miwili hadi minne. Kuku hawa wenye umri huu
wanatakiwa watunzwe vizuri ili wakusaidie kukupa mfugaji faida, vinginevyo
ukishindwa hapa kutunza kuku wako vizuri basi usitegemee kupata faida kubwa.
1. Hatua ya 1, waweke
kwenye banda kubwa.
Hatua hii inakuja kama walikua bado kwenye eneo la kulea
vifaranga, wahamishe na uwapeleke kwenye banda kubwa. Kama banda ni hilo
hilo moja, waondolee ‘hardboards’
ulizokuwa umetengea vifaranga, na waachie kwenye banda zima.
2. Hatua ya 2, wawekee
bembea kwenye banda.
Ukumbuke kwamba kuku ni ndege, hivyo kuna wakati wanapenda kuwa
juu. Hivyo ni muhimu kuwawekea bembea ili iwasaidie kufurahia maisha yao na
kuwa huru zaidi. Hiyo itakuwa ni sehemu mojawapo ya kufanya zoezi.
3. Hatua ya 3, weka matandazo safi.
Hakikisha matandazo yasiwe na harufu kali au vumbi. Hakikisha
pia maji hayamwagiki bandani. Na
Mara tu yakimwagika ondoa matandazo yaliyolowa na weka mapya. Pia ukumbuke
kubadilisha matandazo mapema ili yasiweze kutoa halafu na kuleta magonjwa
mengine yatakanayo na matandazo kurundikana.
4. Hatua ya 4, weka
ratiba ya usafi.
Unaweza ukaweka ratiba ya usafi bandani na kwenye eneo la
kuzunguka banda, angalau mara mbili kwa wiki. Tumia dawa ya V-RID kufanyia
usafi na kupulizia dawa hewani. Hii itasaidia banda lako kubaki safi wakti wote
na afya kwa kuku wako pia.
5. Hatua ya 5, wape
kuku maji safi muda wote.
Pia unaweza kuwaongezea vitamin kwenye maji yao hasa kama
wanafugwa ndani muda wote. unapowapa maji safi muda wote si rahisi sana kuweza
kupata magonjwa yatokanayo na bakteria.
6. Hatua ya 6, wape
chakula chenye virutubisho.
Usiwape kuku wako ilimradi tu chakula, wape kuku wako chakula
chenye virutubisho vya kutosha. Unaweza ukaanza kuwapa ‘growers’ au aina nyingine
ya chakula kizuri. Ukiwalisha kuku wako chakula duni, wanadumaa.
7. Hatua ya 7, rudia
chanjo ya newcastle kwa wakati.
Hii unaweza kufanya yaani kila baada ya wiki 10 tangu
walipochanjwa mara ya mwisho. Unaporudia chanjo inasaidia sana kuwafanya kuku
wako wawe imara wakati wote na inakuwa ngumu kukutana na magonjwa.
8. Hatua ya 8, wape
dawa ya minyoo.
Dawa ya minyoo unawapa kuku wakiwa na miezi miwili na rudia kila
baada ya wiki 10. Ukishindwa kuwapa dawa hii basi tegemea kuokota kuku wengi
ambao watakufa kutokana na kushambuliwa na minyoo.
9. Hatua ya 9, walishe
majani na mboga mboga kwa wingi.
Unapowalisha kuku majani ya mboga mboga hiyo itawairishia miili yao
kwa kuiongezea kinga dhidi ya magonjwa. Hata hivyo kama kuku wakilishwa majani
ni rahisi pia kuweza kutaga vizuri inapofikia kipindi hicho.
10. Hatua ya 10, kama
una eneo kubwa, wafungulie nje ili wazunguke zunguke.
Waache kuku wako wazunguke na waoge kwenye mchanga. Kuzunguka
zunguka na kuparua parua kunawafanya bize na kudonoana na kulana manyoya. Kuoga
kwenye mchanga kunawafanya wawe safi na kama wana wadudu, wanaweza kuwaondoka.
11. Hatua ya 11, kuwa
na mawasiliano ya karibu na daktari wa mifugo.
Mara tu uonapo dalili za ugonjwa, wasiliana na daktari wa mifugo
kwa ushauri zaidi. Pia tafuta chanzo cha ugonjwa ili ukiondoe.
Mwisho wa somo letu la leo na tunaamini umejifunza kitu cha
kukusaidia kuboresha ufugaji wako.
Pia kama wewe ni mfugaji wa
kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO na KIENYEJI ASILIA. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote mnakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika
mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.