Oct 16, 2017
Mambo Yako Yanapokuwa Hovyo Kabisa…Fanya Hivi.
Inapofika
mahali kwenye maisha yako unaona kila kitu ulichokifanya hakijafanikiwa na
unaona kabisa umepoteza muda mwingi kwa kufanya kazi ya bure, unapokutana na
kipindi hiki hapa inatakiwa ujifunze
kutulia sana.
Katika
kipindi hiki, hutakiwi kukurupuka na
kuchukua hatua za haraka ambazo hatua hizo lengo lake litakuwa kama ni kufidia
pale ulipodondoka au pale ambapo hujafanikisha.
Unatakiwa kutilia kwa kuliza akili yako sana.
Kama
utataka kukurupuka na kuchukua hatua za haraka , hazitakusaidia sana kwa maana
kichwa chako kitakuwa na haraka sana ya kuwaza kukamilisha mambo yako, hivyo
hakuna hata thamani kubwa utakayoweza kuitoa.
Hiyo
inamaanisha nini, unapoona mambo yamekwenda hovyo, mambo hayaeleweki, usije juu
sana, tuliza akili yako, weka nguvu za uzingativu eneo moja kwanza kutaka
kubadilisha kitu kimoja na hayo mambo mengine utayabadlisha pia.
Lakini ikiwa utaamua kukurupuka na kuchukua hatua zote unazozijua za kufanya maamuzi ya zimamoto, elewa kabisa utakuwa ni sawa na mtu ambaye ameamua kuongeza ‘petroli’ kwenye moto, hakuna utakachokifanikisha.
Lakini ikiwa utaamua kukurupuka na kuchukua hatua zote unazozijua za kufanya maamuzi ya zimamoto, elewa kabisa utakuwa ni sawa na mtu ambaye ameamua kuongeza ‘petroli’ kwenye moto, hakuna utakachokifanikisha.
Kuna
wakati unaweza ukaanguka kwenye maisha, kwa sababu ya maamuzi kama haya ya
kukurupuka hasa mara baada ya kugundua kwamba mambo yako hayaja kwenda sawa
kama wao wanavyofikiri au kama wao wanavyotaka.
Huhitaji
kuwa na wasiwasi mwingi, unahitaji kutulia, hebu jiulize hapa, ukiwa una
wasiwasi kwa sababu ya mambo yako kwenda hovyo hiyo kwako itakusaidia kitu
gani? mpaka hapo umejua ambacho unapaswa kuwa nacho ni utulivu.
Uwezo
wako wa kutulia ndio utakaokusaidia sana kuweza kufanya mambo kwa busara na
umakini mkubwa utakaoweza kupeleka wewe kutoa thamani inayotakiwa, kinyume cha
hapo utakuwa unajidanganya.
Kwa
hiyo, kama unaona mambo yako yamekwenda hovyo, jambo la makini sana unalotakiwa
kulielewa hapa na kulifanyia kazi wewe ni kutuliza akili yako kama tulivyoanza
kusema mwanzoni mwa makala haya.
Akili
yako inapotulia utashangaa changamoto zako utakuwa unazivuka kwa jinsi
unavyotaka wewe. Hakuna kinachoshindikana hasa kunapokuwa na utulivu. Utulivu
ni kitu cha msingi katika kuweza kukusaidia kufanikisha ndoto zako muhimu
ambazo hata ulikuwa unaona hazifanikiwi tena.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.