Oct 8, 2017
Majibu Ya Mafanikio Ni Muunganiko wa Mambo Haya.
Mara nyingi hulka yangu ipo katika misingi ya kuwashirikisha
watu mambo ya msingi yatakayowafanya watu hao waweze kupiga hatua za kimaisha.
Hivyo naomba kama ilivyo ada yangu, naomba nikushirikishe elimu hii ya maisha ambayo
itakusaidia kuweza kupiga hatua, hivyo naomba uwe nami mwanzo hadi mwisho wa
makala haya.
Na siku ya leo nataka kusema nawe kuuhusu ukweli ambao
unatakiwa kujua ili kutimiza jambo fulani katika maisha yako. Na ukweli huo ni
huu hapa.
Kama ujuavyo katika safari yako ya mafanikio ni lazima
kuwe na vitu vikuu vitatu ili uweze kutimiza jambo lako muhimu. Vitu hivyo
vitatu ni, kwanza unatakiwa kuwa WAZO,
pili unahitaji UWAJIBIKAJI juu ya jambo hilo, jambo la tatu mara baada ya hivyo
vyote kufanyika kinachotea huitwa MATOKEO.
Mara nyingi watu wengi huwa tunaangalia katika matokeo
pekee yake huku tukisahau ya kwamba matokeo ya jambo fulani kutokea ni
mnyumbuliko ambao huanza na wazo, uwajibikaji kisha kuja hayo matokeo. Ukisoma
vizuri kitu ambacho kinaitwa ‘power of
cause anda effect’ utaelewa vizuri.
Kwa kifupi ni kwamba ukweli juu ya nguvu ya chanzo na
madhara ipo katika kuangalia madhara kuliko kuangali chanzo cha madhara hayo
kutokea. Kwa mfano, ukifeli katika jambo fulani, watu wengi huwa wanaangalia
pale walipoangukia pasipo kuangalia chanzo cha wao kufeli.
Hivyo ili uweze kuwa bora katika maisha yako jijengee
utaratibu wa kuanza kutazama chanzo cha jambo fulani kutokea kisha uje utazame
matokeo ya jambo hilo. Kitendo cha kuanza kutazama chanzo cha jambo fulani
kutokea humsaidia mtu kuweza kuwa bora zaidi na pia humsaidia mtu kujua nini
chanzo cha kufeli kwa jambo fulani.
Na kama ambavyo nilivyosema hapo awali ya kwamba katika
safari yako ya mafanikio kuna vitu vitatu ambavyo ni lazima kila mmoja wetu aweze kuvifahamu, vitu hivyo
nimeshaviorodhesha hapo awali, hivyo kitu cha kwanza sitakuzungumzia siku ya
leo, bali nitazungumzia jambo la pili na
tatu.
Mara nyingi mara baada ya kupata wazo fulani ili uweze
kuanza kulifanyia kazi wazo hilo, jambo ambalo linafuata ni kuweza kuwajibika juu
jambo hilo. Na katika kipengele hiki cha kuwajibika unahitaji kuwekeza nguvu na
juhudi za kutosha katika kufanya kazi ili kupata majibu unayostahili.
Ukishindwa kuwajibika vizuri, basi tambua fika jambo la tatu
haliwezi kuleta matokeo ya majibu ambayo
uliyatarajia. Mara nyingi upatikanaji wa majibu kwa kwa kile ambacho unakifanya
hutokana na wazo na uwajibikaji wako.
Unaweza ukawa na wazo zuri ila kama uwajibikaji wako ni
mdogo basi fahamu fika ya kwamba matokeo ya jambo hilo utakuwa ni finyu pia.
Swali la msingi linaweza kuja, sasa nifanyaje ili niweze kufanikiwa?
Swali hilo majibu yake ni haya, kwanza hakikisha unakuwa
na wazo bora ambalo limechambuliwa vizuri, lakini pia muhusika wa wazo hilo ni
lazima aweze kujitoa kikamilifu katika kuwajibika ili kuhakikisha linaleta
matokeo mazuri.
Mwisho nimalize kwa kusema MAWAZO MAZURI + UWAJIBIKAJI = MATOKEO MAZURI.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni ndimi Afisa mipango wa mafanikio yako,
Benson Chonya,
Mawasiliano; +255 757
909 942,
Email; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.