Oct 12, 2017
Uwekezaji wa Mafanikio Yako Ni lazima Ujikite Katika Misingi Hii.
Katika sayari hii lipo jambo kubwa ambalo unatakiwa
kulifahamu kila wakati katika maisha yako, jambo hilo si jingine bali lile
jambo la kuhakikisha unawajibika mwenyewe kwa asilimia mia moja. Nasema hivyo
nikiwa na maana ya kwamba kwa kila kitu ambacho unakifanya hakikisha ya kwamba
unajituma vya kutosha.
Kujituma huku ni katika kuhakikisha unajitoa muhanga
katika kuhakikisha unajitoa kikamilifu katika kuyasaka mafanikio hayo. kama
ambavyo umeuchoka umaskini basi yachoke na maisha ambayo hayukupi furaha ya
kweli.
Mara nyingi tunasema ya kwamba watu wengi hawana furaha
ya kweli hii ni kwa sababu ya mambo makuu mawali, japo la kwamba watu wengi
hawana furaha ya kweli hii ni kwa sababu hawafanyi vitu ambavyo hawavipendi,
wanafanya ili mradi wasogeze siku.
Jambo la pili watu wengi hawana furaha katika maisha yao
hii ni kwa sababu watu hao wamechaguliwa maisha ya kuishi na watu wengine. Kwa
mfano wapo baadhi ya watu wanafanyakazi fulani eti kisa mtu fulani alimwambie
afanye kitu hicho kwani kinalipa sana. Watu hao mara baada ya kuanza kufanya
jambo hilo wamejikuta matokea ambayo waliyategemea hayapo tena.
Hii ina maana gani? Hii ina maana ya kwamba furaha ya
kweli katika maisha ya mwanadamu inapatikana kwa kuhakikisha wewe mwenyewe
ndiye ambaye unakuwa kiongozi maisha yako kwa asilimia mia moja huku jitahada
za kweli zikifanyika katika kuhakikisha unafanya kitu ambacho unakipenda pia.
Na sifa kubwa za mtu ambaye anahitaji kuwa kiongozi
katika maisha yake ni kuhakikisha ya kwamba anasimama kidete katika kupanga
mipango na mikakati kabambe ya jinsi ambavyo anavyoweza kuishi ndoto zake.
Hivyo kwa kuwa una shauku kubwa ya kuweza kuisha ndoto
zako huna budi kuhakikisha ya kwamba kitu ambacho unakihitaji kinatokana kwa
asilimia kubwa na kiwango cha uwekezaji wako.
Kiwango hicho cha uwekezaji wako ni lazima kiwe ni cha
kweli, mara zote haiwezekani ukapanda mahindi katika shamba lako huku
ukitegemea ya kwamba uje uvune maharage. Na pia imeandikwa yeyote apandaye kwenye
mawe asitegemee kuja kuvuna mavuno ambayo aliyatarajia.
Huenda nikawa nimekuacha njia panda pale niliposema ni
lazima ufanye uwekezaji ukadhani namanisha pesa, hapana sina maana ya pesa bali
maana yangu ni hii uwezezaji wa msaka mafanikio upo katika mambo yafutayo;
1. Jinsi mtu huyo anavyoipangilia ratiba yake kuanzia
anapoamka hadi anapokwenda kulala. Mara nyingi ratiba za watu wengi kwa siku
nzima huwa hazielewiki, kwa mfano wapo baadhi ya watu ukiwauliza hivi kwa siku
nzima ya leo umefanya nini? Watu hao wanaweza wasiwe na majibu ya moja kwa moja
ya kukupa, kwani wengi wao ratiba zao huwa hazipo katika mpangilio.
Hivyo kama wewe ni miongoni mwa watu hao ambao huwa
hawana ratiba muhimu, unachotakiwa kufanya kuanzia sasa ni huhakikisha ya
kwamba unatengeza ratiba ambayo itakuongoza wewe katika kufanya mambo
mbalimbali ya muhimu. Endapo utaamua kufanya hivyo ambavyo nimekueleza basi
tegemea matokea makubwa sana.
2. Uwekezaji wa msaka mafanikio ni lazima uwe katika
misingi ya kuweka vipaumbele vya kiutendaji wa siku nzima. Huwezi kusema
unataka kufanikiwa harafu ukawa huna vipaumbele ambavyo vitaongoza maisha yako
kwa siku nzima. Vipaumbele hivi ni lazima viwe katika kujua ni nini ambacho
utaanza kukifanya na nini kitafuata.
Endapo hutajijengea utaratibu huu wa kuweka vipaumbele
katika maisha yako ni lazima ujue kabisa maisha yako yatakuwa katika misingi ya
kujiua wewe mwenyewe. Hivyo kwa kuwa sasa ulichokisoma siku ya leo umekielewa vyema ninachotaka kukusihi ni kwamba
hakikisha ya hiki ulichokisoma unakiweka katika matendo.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni ndimi Afisa mipango wa mafanikio yako,
Benson Chonya,
Mawasiliano; +255 757
909 942,
Email; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.