Oct 30, 2017
Kama Utazingatia Hatua Na Mawazo Haya, Tayari Umefanikiwa.
Siku zote ieleweke hivi,
kama unarudia mawazo yako, kama unarudia hatua fulani hivi mara kwa mara ni
wazi utakuwa bora sana kwa hicho unachokirudia kila wakati.
Haijalishi kitu gani
unachokirudia sana kwenye mawazo yako yaani unakifikiria sana ila kitu hicho
kitakuwa sehemu ya maisha yako kama utafanya hivyo sana.
Haijalishi ni hatua zipi
utakuwa unazirudia sana kwenye maisha yako ila hatua hizo zitakua matokeo ya
kitu fulani hivi kwenye maisha yako.
Ikiwa utatenga muda na masaa
kadhaa kwa wiki kufikiria na kutenda jambo lolote lile katika maisha yako, uwe
na uhakika jambo hilo utalivuna.
Kwa mfano, ukiona una maisha
mabovu au una maisha mazuri ujue ni mwendelezo wa mawazo fulani ambayo ulikuwa
nayo kwa siku za nyuma.
Mawazo yapi uliyonayo kwa
muda mrefu, ni hatua zipi ulizonazo kwa muda mrefu hizo ndio hatua zinazokupa
matokeo ya kitu fulani kwenye maisha yako.
Hauhitaji sana kumtafuta mtu
pengine anayefanya maisha yako mabaya, kama iko hivyo kweli, ila unachotakiwa
kufanya ni kukagua hatua na mfumo wa mawazo yako ukoje.
Wakimbiaji wote duniani wanaelewa vyema kabla hujawa mshindi katika
mbio lazima ufanye mazoezi mengi sana yatakayokufanya uwe mshindi.
Kuna wakati itakutaka
ukimbie mbio za muda mrefu zaidi ya mashindano unayochukua na tena mara kwa mara
hadi uweze kushinda.
Kuwa mshindi katika mbio kwa
wakiambiaji wanajua kabisa sio swala la mara moja bali ni swala linalochukua
mazoezi karibu ya kila siku.
Halikadhalika, hata washindi
katika maisha ni watu ambao wanajuhudi endelevu
za kila siku kwenye maisha yao. Kitu hiki leo kikikataa kuna kingine
kitafanyika hadi kieleweke.
Hivyo hata kwako inatakiwa
ieleweke mawazo yanayojirudia mara kwa mara akili mwako, hatua zinazojirudia
hizo ndizo zinazokupa mafanikio yako.
Mafanikio yako yanajengwa
hatua kwa hatua, unatakiwa kujua hata kama hatua unazo chukua ni kidogo lakini
hatua hizo zipo na ipo siku zitakufanikisha.
Una uwezo wa kufanya maisha
yako kuwa bora zaidi ikiwa utakuwa na mawazo na hatua bora zinajirudia akilini
mwako kila wakati.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.