Oct 29, 2017
Acha Kuendelea Kufanya Kosa Hili Tena Na Tena Unapotafuta Mafanikio Yako.
Kati ya kosa ambalo hutakiwi
kuendelea kulifanya kwenye maisha ni kufanya vitu au mambo yako kwa kuingia na
mawazo ya kujaribu.
Hili ni kosa kubwa ambalo
linawangusha wengi wanaposema wanataka kufanya kitu fulani halafu wanasema hebu
ngoja ni jaribu.
Unajua unaposema najaribu
maanake nini? hiyo ina maana hicho kitu ambacho
unakifanya kwanza huna uhakika nacho kama utakiweza.
Kwa hiyo unapojaribu,
usitegemee kama kuna ushindi wowote unaweza ukatokea, maana wewe si unajaribu.
Wale wote wanaojaribu sio
rahisi kuweza kufanikiwa kupata ushindi, kwa sababu akili na kila kitu kinakuwa
kimekaa kwa kujaribu jaribu.
Unapotaka kufanya jambo
halafu ukaingia na mawazo ya kujaribu, kwanza hata ukishindwa unakuwa hauna
uchungu sana, kwa sababu utasema ulikuwa unajaribu.
Pia hata hivyo, utakuwa ni
mtu ambaye una sababu hata kama
ukishindwa, lazima utasema tu si nilikuwa najribu tu sio nilikuwa nafanya
kabisa.
Kwenye maisha hakuna uwanja
wa majaribio hata siku moja. Kama unafanya kitu au vitu vyako kwa kujaribu unajipotezea
muda wako bure na unajidanganya.
Ikiwa kama kuna vitu umeamua
kuvifanya, jitoe kufanya vitu hivyo kwa ukamilifu wako wote lakini sio kufanya
majaribio.
Wakati wewe utaendeleakuendeleza
wimbo wa kujaribu, wapo watu ambao wamejitoa kufanya kweli kwenye maisha yao na
hawajaribu.
Najua hili ni kosa ambao
umekuwa ukilifanya sana na limekuwa likagharimu maisha yako lakini si wakati wa
kuweza kurudia tena.
Kimefika kipindi cha kusimamia
ndoto zako, kimefika kipindi cha kuhakikisha ndoto zako zinaweza kutimia na
kuwa kweli.
Jaribu kujiuliza utaendelea
kujaribu mpaka lini? Jipe muda wa kufanya mambo yako, achana na habari ya
kujaribu maisha hayakusubiri hata kidogo.
Washindi katika maisha ni
watu wa kufanya na si watu wa majaribio. Chagua kufanya kitu hata kama ni kidogo
sana lakini kifanye na usijaribu hata kidogo.
Kujaribu mara nyingi
kunakuandalia mazingira ya wewe kuweza kushindwa moja kwa moja. Hakuna
mafanikio utakayoweza kuyapata kwa kuishi maisha ya kujaribu.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.