Oct 14, 2017
Kama Una Tabia Ya Kulalamika Katika Maisha Yako, Basi Dozi Hii Inakuhusu.
Mara nyingi kama ikitokea afya yako haipo sawa, huwa
unakunywa dawa ili kurudi katika hali yako ya kawaida. kama ilivyo katika afya vivyo hivyo katika safari yako ya mafanikio kama una
tabia za kulalamika unahitaji dozi ya dawa ambayo itakufanya upone kabisa
ugonjwa huo.
Najua utakuwa umeshangaa nilivyosema ni ugonjwa, wala
usishangae, kulalamika katika maisha ni ugonjwa ambao watu wengi wamekuwa
wakiuugua, na wengi wa watu hao wamekuwa hawajui ni dozi gani itawafaa ili
waweze kupona, hivyo katika makala haya nitaueleza ni kwa jinsi gani utapona
ugonjwa huu.
Ugonjwa wa kulalamika umekuwa kizuizi kikubwa katika
kuyafikia mafanikio yako, unajua hii ikoje? Ipo hivi mafanikio ya kweli huanza
kujengwa nafsini mwa mtu, kama itatokea ya kwamba unalalamika sana katika
maisha yako ni lazima utajikuta huna amani ambayo itakufanya uweze kupata
mafanikio.
Ukosekanaji wa amani katika nafsi ya mtu kwa namna moja
ama nyingine hutengeneza kinyongo ndani yake na mtu ambaye analalamikiwa, na
kinyongo hicho kinatakufanya usiweze kupiga hatua zozote za kimaisha.
Mara nyingi ukijaribu kuwachunguza watu ambao hulka na
kalama yao kubwa ambayo ipo katika kulalamika maisha yao yapo katika mstari
mwekundu wa kuelekea kufa maskini, Hii ni kwasababu ya licha ya watu hao
kuendelea kulalamika wamekuwa hawachukui hatua zozote za kuwafanya wao wasonge
mbele zaidi ya watu hao kuendelea kulalamika, ukiwauliza watu hao mara nyingi
watakwambia serikari ndo chanzo, wengine watawataja ndugu na jamaa na marafiki
ndiyo chanzo cha mambo yao fulani falani kutokuwa sawa.
Japo yawezekana ukaona hizo ni sababu na chanzo cha wewe
kuwa hivyo ulivyo, kama ambayo kauli mbiu yetu ituongozayo katika kufanya kazi
ya kwamba “badili maisha yako kwa kuwa fikra sahihi”, hivyo unachotakiwa
kufanya kutumia dozi hii itayokusaidia kupona ugonjwa huo.
Dozi hiyo ni
KUKUBALINA NA HALI ILIYOTEA.
Ili kupona na ugonjwa huu wa kulalamika unachotakiwa
kufanya ni kukubaliana na hali ambayo imetokea. Kama umefukuzwa kazi ambayo
ulikuwa unaipenda basi kubaliana na hali hiyo, kama maisha yako ni magumu huku
ukitoa sababu ya kwamba wewe ni yatima unachotakiwa kufanya ni kuacha
kulalamika bali ni kukubalina na hali hiyo.
Yawezekana zipo sababu nyingine mbalimbali ambazo
unazijua wewe zimekufanya umekuwa mlamikaji mzuri , ninachotaka kukwambia siku
ya leo kulamikia sio dawa bali ni ugonjwa wa umasikini, hivyo ni vyema ukaacha
tabia hiyo mara moja.
Hivyo jijengee tabia ya kutafuta majibu mengine ya
malalamiko yako, na majibu yako hayo yawe chanya na yenye kukujenga katika
kufikia mafanikio yako. Mwisho nimalize kwa kusema kama ambavyo vijana
wasemavyo pambana na hali yako, nami nasema acha kulalamika pambana na hali
yako kwani uwajibikaji wa mtu binafsi katika kuyasaka mafanikio ndiyo siri ya
kufanikiwa kwako.
Tunakutakia kila la
kheri kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE.
Ndimi Afisa mipango wa mafanikio yako,
Benson Chonya,
Mawasiliano; 255 757 909 942,
Email; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.