Oct 20, 2017
Usifanye Kosa La Kuwekeza Nguvu Hizi Tu Basi Kwenye Mafanikio Yako.
Ili
kufanikiwa kwa chochote kile unalazima kwa wewe kuanza kwanza jambo hilo. Hakuna
kitu au mafanikio ambayo utayapata kama utabaki tu kuongelea mafanikio mdomoni.
Kuanza ni lazima uanze bila kujali unaanza kwa namna gani.
Lakini
hata hivyo kuanza peke yake hiyo haitoshi na wala hiyo siyo 'gerentii' ya
mafanikio, unahitajika kuendelea kuongeza juhudi zaidi za kuweza kufanikiwa kwa
kufanya kazi kila siku. Juhudi endelevu ni muhimu kwa mafanikio yako.
Watu
wengi wanaanguka sana kwenye vile vitu wanavyofanya kwa sababu wanakuwa ni watu
ambao wakati wanataka kuanza walikuwa ni watu wa juhudi sana, lakini mara tu
wanapoanza, hujikuta wanajisahau na juhudii zile kuziacha mara moja.
Sasa
inapotokea ukafanya hivi yaani ukaweka juhudi kubwa mwanzoni na mbeleni ukajisahau,
kupiga kwako hatua inakuwa ni ngumu. Mafanikio yako ni rahisi yakaonekana
kwenye hatua za mwanzoni huko mbele hakitaonekana kitu tena kama hutaendeleza
juhudi.
Kwa hiyo
kama unataka kufanikiwa unatakiwa kukumbuka kila mara kuweka juhudi mwanzoni
lakini na kuendelea kuweka juhudi hizo hizo kwenye kila hatua unayopitia. Hiki ni
kitu muhimu sana na msingi sana kwa mafanikio yako.
Ndio
maana siku zote huwa tunasisistiza unapotaka kuanzisha jambo acha kujiandaa
sana, unapokuwa unajiandaa sana hiyo itakupelekea wewe kutumia nguvu nyingi
mwanzoni na kujisahau kufanya majukumu ya msingi mbeleni.
Watu
wengi wamejikuta katika mtego huu wa kushindwa kufanikiwa sana kwenye kila
wanachokifanya kwa sasa kwa sababu tu ya kujivunia nguvu kubwa walizoweka
mwanzoni na kusahau kuweka juhudi hizo mbeleni tena.
Ili kuelewa
hili vizuri, angalia mfano mzuri wa miti mikubwa. Miti hii huwa inaanza kama
kitu kidogo tu. Lakini katika kuendelea kukua hurefuka na mwisho wa siku kuwa
mti mkubwa sana ambao kuukata inahitajika nguvu nyingi sana.
Halikadhalika, hata mto huwa unaanza kidogo kidogo lakini kwa jinsi unavyozidi kwenda mbele
unakuwa una nguvu kubwa ya kuweza kusomba chochote kile kinachoweza kukatisha
mbele.
Vivyo
hivyo na wewe ndio unatakiwa kuwa hivyo. Anza na nguvu fulani hata kama sio
kubwa sana, lakini nguvu hiyo endelea kuiwekeza ili iwe kubwa zaidi na zaidi. Kama
hautafanya hivyo mafanikio yako yatakuwa ya muda tu na kutoweka mara moja.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.