Oct 27, 2017
Kipe Kipaumbele Kitu Hichi Kikupe Mafanikio.
Hivi
umeshawahi kujiuliza au unajua ni kitu gani ambacho ni cha muhimu sana kwenye
maisha yako? je, ni afya, familia, imani yako au ni kitu gani?
Iwe kwa
kujua au kutokujua kwa kawaida kipo kitu cha muhimu sana karibu kwa kila mtu
kwenye maisha yake. Kitu hicho ndicho kinacho ongoza maisha ya mtu huyo.
Hata
hivyo pia, kila siku maisha yanatuuliza kitu cha muhimu kwetu, na kwa bahati
nzuri tunajibu kupitia vitendo vyetu na si midomo.
Kwa mantiki
hiyo, hata nikikuuliza kitu kipi cha muhimu kwako hata usiponijibu najua
vitendo vyako vitanijibu vizuri sana kuliko maneno yako.
Zipo
namna nyingi amabazo zinaweza kukusaidia kujua kipi ni cha muhimu kwako au
kwenye maisha yako na kipi si cha muhimu.
Unaweza
kujua kitu cha muhimu kwako kwa kuangalia jinsi unavyotumia muda wako kufanya
jambo fulani hivi.
Ikiwa
muda wako umeutenga kufanya jambo fulani na kila siku na jambo hilo unalifanya na huachi basi hicho ni
kitu cha muhimu sana kwako na kina matokeo.
Chochote
kile unachokipa muda wako mwingi hicho ndicho kitu cha muhimu bila kujali kitu
hicho kina faida au hakina.
Inawezekana
kabisa kitu cha muhimu kwako ikawa ni maongezi au kufatilia habari na
inawezekana pia kitu cha muhimu kwako ikawa ni kufatilia ndoto zako.
Kitu
kipi kitakachotufanya tujue kitu kipi cha muhimu kwako ni kwa jinsi wewe unavyotenga
muda wako kwenye kitu hicho kila wakati.
Ukumbuke
kitu cha muhimu kwako inaweza ikawa hata kuimba, kuangalia mpira ila kama kina
kula muda wako basi hicho ndicho kitu cha muhimu kwako.
Maisha
yako yako hivyo kutokana na kuna vitu ambavyo ulivipa umuhimu hivyo vitu ndivyo
vimefanya uwe na maisha hayo.
Sasa
ikiwa ulikuwa unatumia muda wako mwingi kwa vitu vya hovyo hovyo itakugharimu
na kwa sababu havijakusaidia kitu.
Kuanzia
leo, anza kufanya vitu vya muhimu kwako ili vikusaidie kukupa mafanikio bora
leo na kesho kwenye maisha yako yote.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.