Oct 6, 2017
Tafuta Majibu Ya Kitu Hiki Utafanikiwa.
Wakati mwingine inawezekana ukawa ni kinara mzuri
wa kulalama juu ya maisha yako, huku ukisahau ya kwamba unachokizungumza mara
kwa mara ndicho ambacho kinasabaisha maisha hayo kuwa magumu zaidi.
Mara nyingine mdomo huumba hicho
unachokizungumza, mara kadhaa nimekuwa nikiwasikia vijana kwa wazee wakisema
vyuma vimekaza, hii ikiwa ina maana ya kwamba mambo ni magumu sana, wapo
wengine ambao wanasema ya kwamba jamaa
anabana, sijui ni jamaa gani?
Swali
linakuja ni kwanini umeyaruhusu maisha yako yaongozwe na fikra za aina hii?
Nasema hivi nikiwa kifua mbele pasina kuona
aibu, nikiwa na maana ya kwamba, watu
wengi tupo vizuri sana katika kuzungumza matatizo yaliyopo
kuliko kuzungumza suluhisho la matatizo hayo.
Yupo mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema katika
maandiko yake ya kwamba, acha kuzungumza kuhusu matatizo bali zungumza kuhusu
suluhisho la matatizo hayo, kwani kutumia muda mwingi kuzungumzia kuhusu
matatizo ni kuongeza matatizo na si kupata majawabu.
Tafuta majibu ya changamoto zako. |
Hebu
tujiulize wale wote wanaozungumzia matatizo ya ajira pasina kutafuta majibu ya
suluhisho la suala hilo wapo wapi? Je tatizo limeisha au ndo kwamba limezidi?
Majibu unayo wewe mpenzi msomaji wa makala haya. Maana yangu ni kwamba laiti tungekuwa
tunazungumza majibu ya tatizo la ajira, huenda tungekuwa tulishapata majibu ya
tatizo hili. Najaribu kuwaza kwa sauti.
Suala la vyuma kukaza pamoja na jamaa kubana ni
kubaki kuzungumzia matatatizo, japo hata kama ukweli unaona upo hivyo,
unachotakiwa kufanya ni kutafuta majibu ya vyuma hivyo kukaza na si kubaki
kuendelea kulizungumzia masuala hayo pasina kutafuta suluhisho.
Mara nyingi katika maisha yako ya kila siku
huna budi kujifunza kuwa chanya, haijalishi maisha ni magumu kiasi gani ambayo
unayapitia. Na sifa kuu ya mtu kuwa chanya si kuungana na watu wengine
kushabikia vitu ambavyo havina msaada wowote katika maisha yako, bali ni
kusimama kidete wewe kama wewe kwani maisha yako uyajue ni wewe.
Pamoja na hali ya kiuchumi kubadilika kama
wengi wasemavyo, kwa kuwa wewe ni mtu
chanya na kama nilivyosema hapo awali uache mara moja tabia ya kuzungumzia masuala ya matatizo bali
jifunze kutafuta majibu ya matatizo hayo.
Hivyo kila wakati, kila saa na kila muda
jijengee utaratibu na mfumo thabiti wa kutafuta majibu ya changamoto
zinazokubali, kwani kufanya hivi ni kujenga utaratibu mpya na mwanzo wa wewe
kuweza kufanikiwa zaidi.
Mwisho ni nimalizie kwa kusema “usizungumzie
hapo ulipo bali zungumza kitu ambacho unataka kukifanya hapo baadae, kisha
uweke mipango thabiti ya kulitenda jambo hilo kwa wakati huu.
Imeandikwa
na Afisa Mipango Benson Chonya,
0757909942.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.