Oct 10, 2017
Jifunze Kuwekeza Mambo Haya Katika Maisha Yako.
Ili uweze kuwa bora katika maisha yako huna budi kuwekeza
mambo mbalimbali ambavyo nitayeleza katika makala haya, ambayo yatakusaidia kwa
namna moja ama nyingine kuweza kuwa bora.
Kama ambavyo mara kadhaa nimekuwa nikinukuliwa nikisema
ya kwamba hatma maisha yako yapo mikononi mwako, hivyo jifunze ni kwa namna
gani wewe binafsi utakuwa kiongozi wa maisha hayo, hata mwanafasafa mmoja wa
kimataifa Mr Jim Rohn aliwahi kusema ya kwamba huwezi ukasema unataka kutengeneza
mwili wako katika misingi ya mazoezi, kisha wewe ukaamua kumuajiri mtu aweze
kufanya mazoezi hayo kwa niaba yako, kisha ukategemea mabadiliko yaweze kutokea
kwako. Jim Rohn anasema mabadiliko ya aina hiyo hayapo.
Hivyo kila wakati kama unataka kufanya mazoezi ya mwili
ni lazima uweze kufanya wewe mwenyewe, halikadhalika katika maisha yako ya kila
siku ili uweze kuwa bora ni lazima uweze kufanya vitu wewe mwenyewe ili uweze
kuwa bora zaidi, kwa watoto wa mjini wana msemo wao ambao unasema ni vyema ujifunze
kupambana na hali yako.
Hii ikiwa na maana ya
kwamba ili uweze kuwa bora ni lazima
uwekeze katika mambo yafutayo;-
1. Simamia vitu vyako kwa ustadi na makini sana.
1. Simamia vitu vyako kwa ustadi na makini sana.
Kusimamia vitu vyako katika ustadi wa hali ya juu pasipo
kuambiwa na mtu na pasipo kusimamiwa na mtu mwingine. Watu wengi wanashindwa
kufikia kilele cha mafanikio kwa sababu wamekuwa wamekeza muda mwingi katika
kufanya kazi bila kuwekeza nguvu na juhudi za kutosha katika jambo hilo.
2. Kila wakati jifunze vitu vipya
vitakavyokufanya kuwa bora zaidi.
Vitu hivyo vipya ni lazima uviweke katika matendo pia.
Wanasema ya kwamba mambo yanabadilika hivyo ni lazima na wewe ujifunze
kubadilika ili kuendana na kasi ya mabadiliko hayo. Daima ni lazima ukumbuke
hicho unachokijua leo hakitakuwa na thamani baada ya miaka miwili ijayo, hivyo
wekeza muda mwingi katika kujifunza vitu vipya.
3. Jifunze kupanga
mipango mikakati ya maisha yako.
Maisha bila mipango ni sawa na bure, hivyo kwa kuwa wewe
unajua ni nini ambacho unakitaka jitahidi sana kupanga fanya mipango na
mikakati itayokusaidia kuwa bora. Yupo mwandishi mmoja jina limenitoka aliwahi
sema usipojenga misingi ya maisha yako vizuri yupo mtu utamsaidia kujenga
misingi ya maisha yake.
Hivyo kila wakati ili uweze kuwa bora ni lazima uzingatie
hayo ili uweze kuwa bora katika maisha yako.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni ndimi Afisa mipango wa mafanikio yako,
Benson Chonya,
Mawasiliano; +255 757
909 942,
Email; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.