Oct 4, 2017
Chukua Hatua Mapema…Utoe Matatizo Haya Maishani Mwako.
Tatizo
kama tatizo lenyewe kwa jinsi lilivyo, haliwezi kuondoka tu hivi hivi kwa kukaa
tu, bali tatizo unaweza ukaliondoa kwenye maisha yako kwa kulifanyia kazi.
Kwa
mfano unaweza ukawa una tatizo la kuwa na kipato kidogo au kwa ujumla huridhiki
kabisa na maisha yako yalivyo.
Unapokuwa
na tatizo kama hili au hata na mengine yanayofanana hivi, elewa tu hayawezi tu
kuondoka hivi hivi yenyewe, lazima utafute fursa ya kukutoa.
Tunapozungumzia
tatizo kwa mfano la kiuchumi, ni fursa pekee ya kibiashara au kilimo ndio
inaweza kutatua na wewe ukabaki salama kiuchumi.
Ikiwa
utakuwa umekaa na kushindwa kuchangamkia fursa ambazo zinaweza zikakusaidia
kuondoa tatizo lako basi, haliwezi kuondoka lenyewe.
Chukua hatua za mafanikio yako mapema. |
Na
kwa jinsi unavyoendelea kukaa chini na kusubiri eti upo muujiza au yupo mtu
atakuja kukutoa kwenye tatizo lako, ndio tatizo hilo linazidi kuwa kubwa.
Kama
nilivyosema huhitaji kusubiri, unahitaji kulitatua tatizo lako mara moja,
unaposubiri unakuwa unajipotezea muda mwenyewe na kujiongezea matatizo zaidi.
Hata
inapotokea fursa ambayo unaona kabisa inakusaidia kutatua tatizo lako,
usichelewe sana kuitumia, kwani itakukimbia na kwenda kwa mtu mwingine.
Fursa
kwa jinsi ilivyo, ina uwezo wa kutoka kwako na kwenda kwa mwingie ikiwa
hautaifanyia kazi mapema na ikiwa wewe ni mtu wa kujishaua.
Acha
kulaza akili yako tena, ni wakati ambao unatakiwa sasa usimame imara kutatua
kila tatizo linakuzunguka.
Jukumu
hutakiwi kumwachia mtu mwingine bali ni wewe. Ila kama unasubiri eti changamoto
zako au matatizo yako yaje yaondoshwe na mtu unajidanganya.
Ukiweza
kutatua changamoto zako mapema sana, basi akili yako inakuwa na uwezo wa
kutatua changamoto nzito zaidi kadri siku zinavyokwenda.
Muda
ni kitu cha thamani kwako sana, hivyo usipoteze muda wako kukaa tu bila
kushughulika na changamoto inayokuzunguka.
Unatakiwa
kila siku, tenga muda wa kutatua tatizo lako hata kama ni kwa kidogo sana na
utashangaa unasogea na mwisho wa siku utatoka na kufanikiwa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.