Oct 18, 2017
Kama Unataka Kufanikiwa, Fikiri Hivi Na Usifikiri Vile.
Jiulize kila wakati ni kitu
gani unachofikiri kwenye akili yako, je, unafikiri dunia iko tofauti na wewe na
haina usawa? Kama unafikiri hivi ndivyo itakavyokuwa kwako.
Jiulize pia ni unafikiri
huwezi kufanya mabadiliko yoyote na umekwama wewe ni mtu wa kushindwa tu? Kama unafikiri
hivi ndivyo itakavyokuwa kwako .
Kipi unachokifikiri kwenye
akili yako, je unafikiri ushindi na kuiona kila siku ni fursa kwako? kile
unachokifikiri, ndivyo itakavyokuwa kwako.
Mawazo hayo unayoyaweka
kwenye akili yako mara kwa mara ndiyo anayokupa matokea ya mambo ya nje yanavyoonekana.
Ndio maana ni muhimu sana
kuweka akilini kile ambacho unataka kikutokea katika maisha yako kuliko kile
ambacho hukitaki.
Usije ukajishangaa umejikuta
umekuwa ni mtu wa majanga sana kila kukicha kwa sababu tu aya akili yako kuweka
vitu ambavyo huvitaki maishani mwako.
Kufikiri yale muhimu ni muhimu
sana kwenye maisha yako. Kipi unachokifikiri sasa, kitu hicho kinaweza kutokea
kwenye maisha yako.
Hii iko hivyo kwa sababu mawazo
unayokuwa nayo yanakuwa yanakusukuma hata wewe kuweza kuchukua hatua za aina
fulani.
Kwa hiyo kile unachokifikiri
ndio kinakufanya uwe mtu wa namna fulani, eidha uwe mtu wa kuchukua hatua au
uwe mtu wa kushindwa.
Hata hivyo uamuzi unabaki
mikononi mwako ni wa kitu gani ambacho ukifikiri. Kama ukiwa utafikiri hovyo,
ujue kabisa utavuna hovyo kwenye maisha yako pia.
Tambua tu chochote
unachokifikiri kinaweza kuwa kweli kwako. Chocchote pia unachokiamini, hicho
pia kinaweza kutokea kwenye maisha yako.
Sasa kwa nini ujitese na
kuumiza maisha yako kwa kufikiri mambo ambayo kwako. inabidi ujifunze kutawala
mawazo akili zako ili ziwaze mema ya maisha yako.
Huhitaji kusema mawazo yanakuja
yenyewe na unasema utayazuiaje? Hilo ni
kweli lakini inabidi utafute mbinu za kuweza kukusaidia kuwa na mawazo chanya.
Mbinu mojawapo ni kukaa na
watu chanya na kusoma vitu vya mafanikio karibu kila siku ili vikujengee
ukomavu wa kuweza kufanikiwa.
Kama umeamua kwa dhati
kufikia mafanikio yako, ni wakati pia umefika wa wewe kujaza fikra zako mambo
chanya ya kimafanikio ili ufanikiwe zaidi.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.