Feb 22, 2018
Hizi Ndizo Biashara Ambazo Haziwezi Kufa.
Mara
nyingi inapotokea uchumi umeyumba au uchumi mbovu kunakuwa na idadi kubwa ya
biashara kuweza kuyumba na zingine kuweza kufa kabisa. Hali hii hupelekea watu hasa
wafanyabishara kuanza kupata tabu kwa kuyumba kiuchumi pia.
Ndio
maana kabla hujafanya biashara unashauriwa kufanya utafiti wa kutosha na
kuangalia ni biashara zipi ambazo zina mahitaji mengi au zinaweza zikadumu kwa
muda mrefu pasipo kuteteleka au kufa kabisa hata kitokee kitu gani.
Pegine
unajiuliza kweli kuna biashara ambazo haziwezi kufa? Katika mazingira ya kawaida
unaweza ukakataa ukasema kwamba, kila biashara inaweza kufa. Lakini hapa leo
nataka ni kukuonyesha biashara chache tu ambazo haziwezi kufa.
Katika
makala hii, biashara hizo sitazichambua kwa kina bali nitakuonyesha tu mwanga au
njia kisha utatafakari na kuangalia ukweli na uhalisia wa biashara hizo ambazo
zinafanywa kwa vizazi na vizazi, na zinaleta mafanikio kwa wengi
Kwa mtu
ambaye ameamua kufanya biashara hizi na akabobea kweli, ni ngumu sana kuweza
kumtoa kwa sababu zinalipa, labda wewe mwenyewe uamue kwamba sasa siwezi
kuifanya tena biashara hii, ukaamua kukaa kwa kubweteka.
Lakini
biashara ambazo nakwenda kukushirikisha hapo ni biashara ambazo zinafanyika
katika mazingira yoyote yale. Zinafanyika kijijini na zinafanyika mjini, lakini
ni biashara ambazo hazichagui kitu ilimradi tu wewe uamue kufanya kwa ufanisi
na utafanikiwa.
Biashara
ambazo haziwezi kufa au hata kama zikifa ndio zitakuwa za mwisho ni biashara
za vyakula kama vile unga wa sembe, unga
wa ngano, mchele, mafuta ya kula, sukari, maharage, dagaa, pamoja na chumvi. Hizi ni biashara ambazo
zinadumu sana.
Ukiangalia
hivi ni vitu ambavyo vinagusa matumizi ya watu ya kila siku. Hakuna siku ambayo
itapita pasipo watu kufanya matumizi ya hivi vitu. Kila siku kwa mfano, unga
eidha uwe wa sembe au wa dona unahitajika sana kila siku.
Watu
wenye mashine au wanaojihusisha na biashara hii kwa mfano ya uuzaji wa unga
wanajua ni biashara ambayo haiwezi kudorola sana, ni biashara ambayo ipo wakati
wote, iwe njaa au kusiwe na njaa lazima watu wale.
Ni jukumu
lako wewe kuangalia kwa mfano ni kipindi gani mahindi yanapatikana kwa urahisi
na kusaga ili kupata unga huo na kuusambaza mtaani. Kuuza ni lazima utauza hata
bila kujali kama utauza kwa faida ndogo au kwa faida kubwa.
Mbali
na unga wa sembe ukiangalia upande mwingine maharage nayo, yanatumika sana
kwenye familia zetu karibu kila siku na uzuri wake yapo maeneo mengi ambayo
maharage haya yanapatikana kwa bei nafuu hususani hasa kipindi cha mavuno.
Unaweza
ukanunua na kuyauza moja kwa moja au ukasubiri kipindi yakiadimika ukaanza kuyauza
moja kwa moja na ikakusaidia kupata pesa. Uzuri soko lake liko wazi ukizingatia
familia nyingi, zinatumia maharage kila siku.
Hali
hiyo hiyo ndio inayoenda mpaka kwenye sukari, dagaa, mafuta ya kula,
halikadhalika na ngano. Ni biashara ambazo zinawalaji wengi. Na watu wengi
wametoka kupitia biashara hizo na kuwa na pesa nyingi sana.
Ukiwauliza
watu wenye maduka ya reja reja ambayo yanauza vitu mchanganyiko, watakwambia
vitu vinavyoendesha duka la reja reja au roho ya duka la reja reja ipo kwenye
hivyo vitu na ndivyo vyenye faida.
Kama
utaamua kufanya, kwa sababu pia wengi wanafanya, ni jukumu lako wewe kuingia na
kufanya kwa akili, au kuongeza kitu cha ziada ili ufanye kwa ufanisi ikiwa ni
kuanzia kwenye vifungashio na hilo litakusaidia kupata wateja wengi.
Kumbuka
sijasema kwamba biashara hizi hazina changamoto. Kila biashara ina changamoto
zake, lakini hata hivyo ni biashara ambazo walaji wake ni wengi na wanapatikana
kila siku.
Mpaka
hapo angalau umepata mwanga wa kile ambacho nilikuwa nataka kukuonyesha
biashara ambazo haziwezi kufa au hata kama zikifa zitachukua muda mrefu sana
kudondoka. Usichelewe kuchukua hatua, ndoto zako zinawezekana.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
.DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.