Feb 26, 2018
Mbinu Za Kuongeza Mauzo Katika Biashara.
Yapo mambo ya msingi ambayo mfanyabiashara yeyote yule ili aweze
kukua katika biashara yake ni lazima ayafahamu, na mambo hayo si mengine bali
ni jinsi gani anatakiwa kuongeza kiwango chake cha mauzo.
Na si kuongeza kiwango cha mauzo pekee, bali kuhakikisha anapata
faida kubwa kwa kile anachokifanya. Wapo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa
hawalizingatii hili na kupelekea bidhaa au huduma wanazozitoa kutofanya vizuri
sokoni.
Kwa minajili hiyo nikaona ni vyema ili kuweza kuwasadia
wafanyabiashara hao ili wapone ni vyema niandike makala haya ili ikusaidie
kuweza kuongeza kiwango chako cha mauzo katika biashara unayoifanya.
Kwanza kabisa ili uweze kuongeza kiwango cha mauzo katika
biashara ambayo unaifanya unatakiwa kuachana na mfumo wa zamani ambao ulikuwa
unatumia katika kufanya biashara yako, kama inashindikana kuachana na mfumo huo
wa zamani basi unachotakiwa kufanya ni kuboresha mfumo huo wa zamani ili uweze
kufanikiwa kibiashara.
Jambo jingine ambalo ni muhimu kabisa ambalo unatakiwa
kulikumbatia katika biashara yako ni, kuelewa mbinu za kufanya
biashara ya yako kwa kutumia mitandao ya kijamii. Kwa wenzetu wazungu
mfumo huu huitwa affiliate marketing, ambapo kwa kibantu
tunaweza tukasema ifike mahala utengeneze mifumo thabiti, mfumo huu utakusadia
kutenggeza pesa ukiwa umekaa tu nyumbani.
Wakati mwingine unaweza ukasema labda njia hii haiwezekani
kuleta matokeo chanya, lakini ninachotaka kusema hakuna lisilo wezekana chini
ya jua hii ni kwa sababu dunia ya sasa imekuwa kiganjani mwa wadamu, kila kitu
ambacho unakitaka utakipata kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kifupi
dunia ya sasa inakwenda kasi sana tofauti na ilivyokuwa nyuma.
Na ili uweze kwenda sawa na kasi hiyo ni lazima jifunze mbinu
mbalimbali zitakazokusaidia kuuza bidhaa au huduma kwa kutumia mitandao ya
kijamii, kwani kwa sasa wanaitumia njia hiyo ndiyo ambao wanafaidi matunda ya
kutumia mbinu hizo.
Jambo jingine ambalo litaweza kukusaidia kuweza kuongeza mauzo
ya katika biashara unayoifanya ni kuhakikisha unakuwa mtalamu katika biashara
husika. Hii mbinu muhimu sana katika kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara
kwa sababu pindi utakapokuwa mtalamu au m-bobezi wa jambo hilo itakusaidia sana
kuweza kuizungumzia vizuri bidhaa au huduma unayoitoa kwa mteja wako,
kufanya hivyo kutamfanya mteja huyo ainunue bidhaa hiyo. Hivyo ili uweze
kuongeza kiwango cha mauzo katika biashara yako jifunze kuwa mtalamu katika
eneo husika unalolifanya.
Jambo la mwisho ambalo ni muhimu sana litakalo kusaidia kuweza
kufanya biashara yenye tija ni kuhakikisha unaimarisha vizuri upande wa huduma
kwa mteja, kwa sababu ule usemi wa kwamba mfalme ni mteja hakuwepo tu, bali
msemo huo upo kumanisha kweli, mteja ni mfalme pindi awapo na asipokuwapo
katika eneo lako la kibiashara pia.
Ufike pahala neno mteja liwe lina maana kubwa sana
katika biashara yako, yaani mfanye mteja kuwa ni sehemu ya biashara ya yako.
Mfanye mteja ajisikie huru katika suala zima la kibiashara.
Mwisho nimalize kwa kusema biashara yenye tija hujengwa na vitu
vitatu vya msingi ambavyo ni bidhaa au huduma nzuri+ masoko mazuri= wateja
wengi.
0757-909942.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
kama kuna group whstsapp niunge kaka
ReplyDelete0658449515