Nov 28, 2017
Ijue Siri Ya Kuondokana Na Ukata.
Siku
ya leo katika pekua pekua zangu za kuongeza chakula cha ubongo nilikutana na
kauli ambayo kiukweli ilifanya mishipa yangu ya ardenalini kuweza kushtuka kwa kasi kama vile nimeona kitu cha
hatari sana.
Kauli
hiyo ilikuwa na maneno mawili yenye kubeba ujumbe mzito ambao sina uhakika
kama, ujumbe huo upo mzani ambao ataweza kupima kilo zake, hii ni kutokana na uzito uliopo katika ulipo katika
ujumbe huo, labda ujumbe huo upimwe na
kichwa cha mwanadamu mwenye mtazamo chanya ndio anaweza kuuelewa.
Ujumbe
huo unasema “unachokiogopa ndicho kitakachokua” narudia kusema tena
unachokiogopa ndicho kitakachokua. Kwa haraka haraka unaweza usielewe maana ya
msemo huo ila pindi utulizapo fikra ya ujazo wa akili unaweza kuelewa.
Binafsi
nilichokielewa katika kauli hii ni kwamba, moja kati changamoto kubwa ambayo
huwazuia watu wake kutoweza kutimiza makusudio yao hapa dunia ni kitu ambacho
tunachokiita ni woga.
Woga
ndio ambao umekua tatizo sugu lilojengeka machoni mwa watu wengi hata
kuwapelekea watu hao kuweza kufa maskini huku watu hao wana uwezo mkubwa wa kufanya
mambo makubwa yenye kuleta mapinduzi ya kufikia kilele cha mafanikio yao.
Woga
huu si mwingine ni ule woga wa kuthubutu kuweza kufanya mambo mbalimbali. Wapo
watu ambao wanatamani kufanya biashara kubwa ila wakiwatazama watu ambao
walifanya biashara hiyo na kuona ya kwamba walifeli basi nao hujikuta wanaogopa
kufanya jambo hilo.
Achilia
mbali biashara, wapo baadhi ya watu wanavipaji mbalimbali lakini watu hao
wamekuwa ni waoga wa kuonesha vipaji hivyo machoni mwa watu wengine huku
wakiamini ya kwamba watachekwa, watu wa aina hii mara nyingi hufa na ndoto zao.
Wapo
baaadhi ya watu wanaogopa kujenga nyumba zao za kuishi huku wakisema, “kwa
heshima niliyonayo nikijenga nyumba ya kawaida watu wengine wanatanishangaa”
kwa kauli kama hizi basi hujikuta miaka inazidi kukatika bila watu hao kuweza
kufanya kitu chochote cha maana.
Wapo
baadhi ya wanafanzi wamekuwa wanaogopa kusoma masomo ya sayansi huku wakiamini
masomo hayo ni magumu mwisho wa siku watu hao hujikuta wanafeli masomo hayo,
kwa mtazamo wa aina hii ndipo ninapokubaliana na kauli ile ambayo nimesema hapo
awali ya kwamba unachokiogopa ndicho kitakachokua.
Kabla
sijamaliza kusema nawe siku ya leo nitakuwa ni mchoyo wa fadhira kama
nitashindwa kutoa ufumbuzi wa tatizo hili, yawezekana ukawa na tatizo la aina
hii ya kuogopa kufanya jambo fulani la maendeleo eti kwa sababu ya woga uliojengeke
ndani mwako, unachotakiwa kukufanya ni kuhakakisha kila jambo ambalo unataka
kulifanya, kabla hujaanza kulifanya jambo hilo hakikisha ya kwamba jambo hilo
unalichunguza kwa makini na sio
kutanguliza woga mbele na ndiyo itakuwa siri ya kuondokana na ukata.
Mwisho
nimalize kusema ya kwamba “kile unachokigopa kukifanya leo ndicho
kitachokufanya uweze kuwa maskini”. Jambo lolote unalifanya hakikisha
ya kwamba linakuwa jambo chanya ambalo halitavunja sheria na taratibu za sehemu
ambayo unaishi.
Asante
sana kwa kusoma Makala haya nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Ndimi Afisa Mipango; Benson Chonya
0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.