Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Sunday, July 2, 2017

Unahitaji Vitu Hivi Sana Ili Kutengeneza Pesa.

No comments :
Hauhitaji sana pesa ili kutengeneza pesa. Unahitaji sana ubunifu .
Hauhitaji sana pesa ili kutengeneza pesa. Unahitaji sana kufanya kazi kwa bidii.
Hauhitaji sana pesa ili kutengeneza pesa. Unahitaji sana kujitoa kikamilifu.
Hauhitaji sana pesa ili kutengeneza pesa. Unahitaji sana kujua elimu ya pesa.
Hauhitaji sana pesa ili kutengeneza pesa. Unahitaji sana kujenga nidhamu binafsi.
Hauhitaji sana pesa ili kutengeneza pesa. Unahitajika sana kutoa thamani.
Hauhitaji sana pesa ili kutengeneza pesa Unahitajika sana kutoa vile vilivyobora.
Hauhitaji sana pesa ili kutengeneza pesa. Unahitajika sana kuwa mtu wa shukrani.
Hauhitaji sana pesa ili kutengeneza pesa. Unahitajika sana kuweka nguvu za uzingativu.
Hauhitaji sana pesa ili kutengeneza pesa. Unahitajika sana kuwa na maono yako ya kipesa.

NI KWELI HAUHITAJI SANA PESA ILI KUTENGENZA PESA?
Ndio. Ile tu kujibebesha dhana kwamba ili upate pesa ni lazima uwe na pesa imewakwamisha wengi. Kipi unachoshindwa kuanza?
Kama unaanzia chini kabisa, anzia hapo hapo ulipo, anza na ulichonacho katika kutafuta mafanikio pesa itakuja.
Unaweza ukaanza na nguvu zako, unaweza ukaanza na kuuza wazo au chochote unachoona kinafaa kwako.
Usitumie pesa ikawa sababu ya kushindwa kuanza kabisa, ukianza na ukapata pesa kiasi, basi pesa hizo utazitumia kama ngazi ya kukusaidia kupata pesa zingine.
Kila wakati zingatia misingi ya kupata pesa kama nidhamu, ubunifu, kufanya kazi kwa bidii, kutoa thamani na mingineyo mengi, hiyo itakusaidia kupata pesa.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.comNo comments :

Post a Comment