google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 24, 2018

Sehemu Sahihi Ya Kuanzia Mafanikio Yako Ni Hii Hapa.

No comments :

Bila kujali upo mbali kimafanikio kwa kiasi gani, lakini bado unayo nafasi ya kuchagua kuendelea mbele kwenye safari ya mafanikio yako.
Si kitu cha ajabu sana kwako na kwa wengine pia wanapoona wako mbali kimafanikio, hasa kwa kuwalinganisha na wengine wanaanza kukata tamaa.
Kitu ambacho watu hawa wanakuwa hawajui ni kwamba, mafanikio hayategemei sana au hayajali eti upo mbali sana, bali kinachojalisha ni mwelekeo wako.
Mwelekeo ndio kitu cha msingi sana katika safari yako ya mafanikio, hiyo ikiwa na maana pale ulipo kwa sasa unaelekea wapi kimafanikio.
Kama mwelekeo wako ni sahihi, basi hakuna shaka hata kama mwendo wako ni kidogo kama wa kinyonga lakini wakati upo utafanikiwa.

Kikubwa ambacho hutakiwi kukipoteza kwenye maisha yako ni ule mwelekeo wa kule unakoenda kwenye maisha yako. Ukipoteza mwelekeo ndio basi huwezi kufanikiwa.
Watu wengi hawafanikiwi katika maisha sio kwa sababu ya kwamba wapo mbali kwa hiyo ni ngumu kufanikiwa. Hawafanikiwi kwa sababu hawana mwelekeo.
Hata katika mazingira ya kawaida kitu chochote kikosa mwelekeo hakiwezi kufika kule kunakotakiwa kufika, lazima kitapotea hapa katikati.
Kwa mfano, ukiangalia ndege inaporuka hewani inakuwa na mwelekeo fulani unaoongozwa na rubani. Inapotokea mwelekeo huo haupo, basi ndege haiwezi kufika.
Na maisha yako hayana tofauti sana na hivyo. Maisha yako yanahitajji mwelekeo kwanza na sio wapi ulipo kimaisha ndio iamue hatma yako.
Kama umekuwa bado unasingizia kwamba eti uko mbali kimaisha na ndio maana hufanikiwi, huo sio ukweli ni uongo.
Wewe sehemu ya kuanzia kwenye safari yako ya mafanikio ni kutafuta mwelekeo. Ukiupata mwelekeo basi njia kuu ya mafanikio umeiona.
Unatakiwa sasa kujiuliza karibu kila siku, mwelekeo wa maisha yako uko wapi. Kitu gani utakachofanya ambacho kitakupa mwelekeo sahihi wa maisha yako.
Hutakiwi kulaumu hata siku moja pale ulipo, unatakiwa ushukuru kwanza, kwani sehemu ulipo hapo ndipo unatakiwa kuanza kutafuta mwelekeo wa mafanikio yako.
Hutaweza kufanikiwa kama hautaweza  kuanza kutafauta mwelekeo wako, sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio kama nilivyosema ni kujua mwelekeo wako pale ulipo.
Hakuna kitu ambacho kitaweza kushindikana kwako, kwa sababu utakuwa umeamua kutafuta kwa dhati sehemu ya kuanza kutafuta mafanikio yako.
Amua leo iwe siku ya kuanza kutafuta sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio yako kwa kutafuta mwelekeo wa wapi uende.
Usiruhusu mtu akwambie huwezi kufika, kule unakotaka kufika kimafanikio, wakati una uwezo wa kuanza kutafuta mweleko wako na kusonga mbele unao.
Usiruhusu mtu akakukatisha tamaa iwe kwa vitendo au kwa chochote kile kwamba wewe upo mbali sana na hautaweza kufanikiwa.
Usiruhusu tena wewe mwenyewe ndani yako ukajiambia kwamba, kwa maisha haya niliyonayo ndio basi tena siwezi kufanikiwa.
Hutakiwi kuruhusu chochote kile ndio kikawa chanzo cha wewe kushindwa kuwa na mwelekeo sahihi wa maisha yako.
Kila wakati unatakiwa kujua ule uwezo wa kufanikiwa na kufika ngazi ya juu kimafanikio unao,  kwa sababu sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio yako umeshaiona.
Kama kuna watu wanaoendelea kukubeza, waache waendelea kukubeza na hiyo itakula kwao, wewe endelea kuchanja mbuga kutafuta mwelekeo wako kimafanikio.
Hutakiwi tena kujiuliza uliza au kumuuuliza mtu kwamba ni wapi mafanikio yanapoweza kuanzia au ni sehemu gani.
Kitu cha kukumbuka ulichojifunza hapa ni kwamba mafanikio yako, sehemu sahihi ya kuanzia mafanikio yako ni kwa wewe kuchukua hatua.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com











\



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.