Feb 25, 2018
Kwa Chochote Unachokifanya Ili Ufanikiwe, Anza Hivi Na Maliza Hivi.
Iwe
wewe ni shabiki wa kuangalia mchezo wa kukimbia alimaarifu riadha au siyo,
lakini kwa vyovyote najua umeshawahi kuangalia mchezo huo hata mara moja na
kushuhudia wale washindi wanakuwa wanapatikanaje.
Kama
utakuwa umesahau kidogo naomba nitakukumbusha hapa, washindi katika riadha, hususani
zile riadha za mita mia moja, wanakuwa wanapatikana kutokana na kuanza kwao kwa
kasi na kumaliza kwa kasi.
Hayupo
mshindi katika riadha wa mita hasa mia moja kama nilivyosema anayeanza kukimbia
kidogo kidogo halafu akawa mshindi kwa madai ya kukazana mwishoni au hakuna ambaye
anaanza kwa kasi na mwishoni kukimbia kidogo kidogo na akawa mshindi.
Mchezo
huu wa riadha mara nyingi kama unataka ili uwe mshindi ni lazima uanze kwa
nguvu, uendelee kukimbia kwa nguvu ukiwa kwenye mbio na wakati huoho umalize
kwa kukimbia kwa nguvu sana kwani washindi wanapatikana pale mwishoni.
Hiyo
yote inatuonyesha mtu anayeshinda mbio, huwa hapunguzi kasi pale mwishoni bali
ndio huongeza kasi, bila kujali anakutana na changamoto za aina gani iwe
kuchoka au kuna hata wakati alidondoka, lakini ni lazima kuongeza kasi ili kushinda.
Halikadhalika
pia kwa upande wa mafanikio, yanategemea na watu wanaonza kitu chochote kwa
nguvu na kumaliza kwa nguvu pia. Kufanikiwa kwa kitu chochote kile ndio
kunakuja kwa namna hiyo na sio vinginevyo.
Tatizo
hapa la watu wengi wanapoanza jambo fulani wanakuwa wanaanza kwa kasi sana, lakini
inapofika katikati ile pumzi yao ambayo wanakuwa wameanza nayo kwa hakika
inakuwa inakata hali ambayo hupelekea kushindwa kabisa.
Na
kinachokuwa kikipelekea wao kuzidi kupunguza kasi na mwisho kuweza kupotea hapa
katika ni kutokana na changamoto, kutokijiamini na wasiwasi ambao wanakutana
nao hapa kati kati na mwisho wa siku hujikuta wako nje ya mstari wa mafanikio.
Unatakiwa
ujue mafanikio yanategemea sana wale wote wanaoweka juhudi kuanzia mwanzo na
kendeleza juhudi hizo mpaka mwisho wa mafanikio yao. Mafanikio ndivyo
yanavyotengenezwa na watu wa namna hiyo.
Kitu
pekee ambacho kitakufanya uanze jambo lolote kwa nguvu na umalize kwa nguvu ile
ile pasipo hapa wewe kati kati kuweza kupotea kwa namna yoyote ni kujitoa kwako
na kujenga mtazamo. Haya mambo yatakusaidia sana.
Unapokuwa
umeamua kujitoa na kujenga mtazamo chanya, hapa kati kati hata ukikutana na
changamoto nyingi, hutaweza kulalamika zaidi utaongeza mwendo kwa sababu unajua
vyema ni wapi unakoenda na unatakiwa umalize vipi ili uwe mshindi.
Nikukumbushe
tena washindi katika mafanikio wana anza kwa nguvu, wanaendelea kufanya kwa
nguvu na wanamaliza kwa nguvu pia kila wakati. Hii ndio kanuni wanaoyoitumia na
wewe unatakiwa uitumie vivyo hivyo pasipo kubabaishwa na kitu.
Kwa
chochote ambacho umechagua kukifanya, kianze kwa nguvu, endelea kukifanya kwa
nguvu na pia kimalizie kwa nguvu. Usije ukafanya kosa la kuanza kwa nguvu na
kumalizia kwa udhaifu, hutashinda ila utashindwa ukifanya hivyo.
Chochote
unachokifanya kitakupa ushindi ukiwa utakianza kwa nguvu na kukimalizia kwa
nguvu pia. Hakuna hali au mazingira ambayo yatakuzuia kufanikiwa kama moto ule
ule ulionanza nao na ndio huo utakaomaliza nao.
Amua
sasa kuwasha moto wa mafanikio yako kuanzia mwanzo hadi mwisho, pasiwepo kitu
chochote hapa kati ambacho kitaweza kujitokeza na kuzima moto huo. Wewe ni mshindi,
anza kwa nguvu, endelea kufanya kwa nguvu na maliza kwa nguvu.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.