google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 20, 2018

Nguvu Ya Mafanikio Katika Kushukuru.

No comments :
Wakati jambo moja linapokwenda hovyo kwenye maisha yako, chukua muda kidogo kushukuru kwa mambo mengi ambayo yanakwenda sawa kwenye maisha yako. Si kila wakati mambo yote yatakaa sawa kabisa, kama utakavyo wewe.
Inapotokea jambo moja limekaa hovyo au halijaenda sawa kama wewe unavyotaka, shukuru kwa yale mazuri kwanza. Huna haja ya kulaumu wengine au kijialumu sana wewe kwamba kuna sehemu ambayo ulikosea.
Wakati huu unapoona jambo lako linakwenda vibaya, weka nguvu na mawazo yako yote kwa hatua ambazo utachukua na zitakusaidia kurudisha mambo yako kukaa  sawa. Usichukue hatua za kukurudisha nyuma hata kidogo.
Kila wakati fikiri juu ya kukazana kuchukua hatua za kusonga mbele huku ukishukuru kwa hayo matokeo ambayo yatakufanya ujifunze. Kwa lugha nyingine kuwa mtu wa shukrani kwa yote yanayokutokea.

Ukumbuke, tukiwa kama bindamu kuna wakati tunakuwa ni watu wa lawama sana kuweza kulaumu kwa kile ambacho kinatutokea na kuona ni kitu kibaya sana. Hata hivyo pia tunakuwa ni watu wa kusahau kabisa kwamba yapo mambo mazuri ambayo tunayapata pia.
Moja ya sifa ya mafanikio ya kweli yanapatikana kama utakuwa mtu wa shukrani. Unapojijengea tabia ya kuwa mtu wa shukrani, inakusaidia kuweza kufanikisha mambo mengi, hii ni tabia ambayo unaweza kuwa nayo bila kujali wewe ni nani.
Haihitaji kuwa na pesa au kuwa na uwezo wa kipekee ili kuwa na shukrani. Mtu yeyote anaweza kuwa na shukrani na unapokuwa unashukuru unajipa uwezo na mamlaka ya kuweza kushinda mambo mengi kwenye maisha yako.
Ukiwa ni mtu ambaye unaishi tu maisha yako pasipo kushukuru, ni jambo la hatari sana kwako na itafika wakati maisha yako yatakuwa katika wakati mgumu sana. Hata ukiwaangalia watu ambao hawana shukrani katika maisha yao, mafanikio yanawasumbua pia.
Ipo nguvu ya shukrani katika mafanikio. Unaposhukuru kwa Mungu, unaposhukuru kwa siku ya leo kuifikia hicho ni kitu kizuri sana kwako. Unaweza ukajitazama wewe mwenyewe kama ni mtu wa shukrani au si mtu wa shukrani.
Unatakiwa kujua kabla hujalaumu, kabla hujalalamika, na kuwaona wengine ndio wabaya wako, kwanza tumia muda kidogo kushukuru yale mazuri uliyonayo. Ipo nguvu ya kubadili hata hali yako inayoonekana mbaya kuwa nzuri ikiwa utakuwa mtu wa kushukuru.
Fanyia kazi somo hili na uwe na mafanikio mema wakati wote, anza leo kwa kushukuru baraka na mafanikio uliyonayo maishani mwako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.