google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 21, 2018

Huna Sababu Ya Kuendelea Kukosa Pesa, Kama Utapata Maarifa Haya.

No comments :
Siri na muujiza wote wa mafanikio makubwa upo kwenye maandishi. Wasomaji wazuri wa vitabu wanaelewa hili vizuri kwamba kwenye maandishi ndio kuna siri nyingi za mafanikio ambazo watu wengi hawazijui.
Ukiwaangalia watu wengi, wanataka sana kuona wakifanikiwa, lakini watu hao hao tena hawako tayari kupata maarifa ya kuwasaidia. Hiyo inakuwa ni sawa na mtu anayetaka kusafiri kwa gari tena wakati huohuo mtu huyo hataki kuweka mafuta.
Kama ndio kufanikiwa kwa namna hiyo hakupo, mafanikio makubwa na ya kweli yanakuja kama una maarifa bora ambayo unayatumia kila wakati kuweza kusaidia kufikia mafanikio hayo. Maarifa hayo hayapatikani popote zaidi ya kujifunza.
Kuna wakati nimekuwa nikueleza faida za kujifunza, ingawa bado kuna watu wanakuwa hawaelewi hili, lakini nikikazia hapa moja ya faida kubwa ya kujifunza pia ni kupata maarifa ambayo yatakusaidia kifedha ukae vizuri kama utajikita katika hilo eneo.
Kwa lugha nyingine huna sababu ya kuendelea kuishiwa au kukosa pesa kila wakati kama kuna aina ya maarifa fulani ukiyapata. Maarifa haya ya msingi ambayo yatakusaidia kwenye maswala ya pesa ndio tunakwenda kujifunza hapa.
Kumbuka, huna sababu ya kuendelea kukosa pesa kama utapata maarifa haya ya msingi. Ni jukumu langu ukifanyia kazi kile utakachokwenda kujifunza uwe na uhakika utapiga hatua. Sasa twende pamoja tuweze kujifunza.

1. Mtazamo wa kimafanikio.
Kama wewe una mtazamo sahihi, mtazamo wa kimafanikio ambao unakuwezesha si kuishi tu bali na kupata mafanikio ya ziada, basi unayo nafasi kubwa ya kufanikiwa na kuepuka na kuishiwa au kukosa pesa kila wakati.
Kinachowaangusha wengi kwenye safari ya mafanikio ni kwamba ni watu ambao hawana mitazamo ya kimafanikio, bali ni watu ambao wana mitazamo ya kushindwa. Hiki ndicho kitu ambacho unatakiwa ujiulize una mtazamo wa mafanikio au kushindwa?
Ukiona una mitazamo mingi sana ya kushindwa, unatakiwa kubadilika mara moja na kutafuta namna utakavyoweza kujenga mtazamo bora wa kukusaidia kufanikiwa. . Mitazamo una nafasi kubwa sana ya kubadilisha maisha yako, hilo unatakiwa ujue.
2. Umiliki wa muda kwa usahihi.
Watu wenye mafanikio wanajua vyema jinsi ya kutunza muda wao vizuri na kupangilia kila kitu. Ni watu ambao hawaishi kwa kubahatisha wanajua kwa uwazi muda ndio rasilimali ya kwanza kuitumia kufanikiwa ikiwa hata huna kitu.
Hivyo hawako tayari kupoteza muda wa wengine na hawako tayari pia kupotezea muda wao. Kwa maarifa haya huwasaidia sana kuweza kufanya shughuli za ziada ambazo zinawaingizia kipato cha ziada.
Kwa muda kidogo wanaoupata hufanya jambo hili au like la kuingiza kipato na mwisho wa siku hujikuta kupata pesa za kutosha. Hapa ninataka kusema nini, ukijifunza juu ya kutunza muda ni nyenzo mojawapo muhimu ya kukufanikisha.
3. Mahusiano sahihi na watu.
Watu wenye mafanikio hawaishii tu kwenye kuwa na mtazamo sahihi wa kimafanikio na kutunza muda wao vizuri. Ukiwafatilia utagundua ni watu ambao wana mahusiano sahihi na watu. Kila wakati hutafuta watu sahihi ambao wataenda pamoja.
Ni ukweli uliowazi unapokuwa na watu sahihi, si rahisi sana wao kuweza kukuangusha. Hivi ndivyo watu wenye mafanikio wanavyojenga mafanikio yao kwa kiasi kikubwa. Kwa sababu hii hata wewe ukifata maarifa haya huna sababu ya kuendelea kuishiwa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.