Dec 30, 2016
Mabadiliko Katika Maisha Yako Hayasubiri Kitu Hiki...
Upo
uwezekano mkubwa sana kwa wewe kuamini kwamba kila mwaka unaanza utakuwa ni
bora zaidi kuliko mwaka uliopita.
Upo
uwezekano wa wewe kuamini sana kwamba kesho yako itakuwa ni bora sana kuliko
ilivyo leo.
Pia upo uwezekano wa wewe kutokuchukua hatua
ndogo ndogo katika maisha yako na kusubiri kuchukua hatua hizo katika
mwaka unaokuja.
Mipango
na matumaini unayojipa naweza kusema ipo sawa kwa kiasi fulani, lakini tena
wakati huo naweza nikakwambia haiko sawa kabisa. Ki vipi?
Badala
ya kujipa matumaini nitafanya hili mwaka kesho au siku fulani na kuamua kutulia,
hebu amua kuchukua hatua leo hii za kufanya kitu, hata kama ni kidogo.
Acha kusubiri mwaka mpya uanze, fanya mabadiliko ya maisha yako sasa. |
Acha
kusubiri hadi mwisho wa mwaka ndio uanze kutafakari kipi cha kuboresha na kipi
sio cha kuboresha katika maisha yako. Jenga utaratibu wa kujikagua karibu kila
siku na kuboresha maisha yako.
Tatizo
kubwa ulilnalo unajipa muda sana wa kuahirisha mambo mengi ikiwa pamoja na
mipango yako. Maisha tuliyonayo hayatusubiri hata kidogo. Kipo kitu ambacho
unatakiwa kufanya kila siku ili kufanya
mabadiliko na kuboresha maisha yako.
Inawezekana
ili kufanya mabadiliko ya maisha yako kuna maarifa unatakiwa uyapate. Pia inawezekana
ili kufanya mabadiliko ya maisha yako kuna watu unatakiwa kushirikiana nao
vizuri ili wa kusaidie kufikia ndoto zako.
Sasa
kama iko hivyo ni kwa nini uendelee kusubiri hadi mwaka ujao?
Chukua
muda mchache kila siku asubuhi kujiuliza ni kipi ambacho utakwenda kufanya ili
kuboresha maisha yako?
Chagua
jambo moja dogo tu la kufanya litakalokusaidia kuboresha maisha yako. Nimesema jambo moja tu, usichague mambo mawili au matatu, nimesema chagua jambo moja tu, ambalo unaamini litakuletea
mabadiliko.
Hiyo
yote inaonyesha mabadiliko ya maisha yako unaweza ukayaanza sasa na si kesho au
wakati mwingine unaona ni bora zaidi kwako.
Mabadiliko
katika maisha yako hayasubiri mwaka mpya uanze, mabadiliko yako hayasubiri
kesho, unatakiwa kufanya mabadiliko sasa, kwani huu ndio wakati bora sana kwako.
Katika
maisha, hakuna mtu ambaye ni rafiki wa kesho. Huwezi kujua kesho hiyo unayoisubiri
ni nini kitatokea. Anza kufanya mabadiliko ya maisha yako sasa na si kesho au
siku nyingine.
Ukichukua
hatua hiyo utayapa maisha yako nguvu sana ya kusonga mbele kuliko ambavyo
ungesubiri. Chukua hatua sasa. Ni muda wa kufanya mabadiliko makubwa kwenye
maisha yako.
Tafakari
juu ya hilo, chukua hatua na endelea kubadili maisha yako kwa kupata maarifa
sahihi kupitia mtandao wako wa DIRA YA
MAFANIKIO kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Dec 29, 2016
Hata Kama Huna Pesa, Ukiwa Na Kitu Hiki Kitakufanikisha.
Inawezekana
umekata tamaa kwa sababu unajiona mipango yako inaenda hovyo, huna pesa na
hivyo unajiona huwezi kufanya kitu cha kukusaidia tena kufanikiwa kwa sababu ya
hali hiyo uliyonayo.
Pengine
usichokijua, kipo kitu kimoja ambacho huwa kinatoa mwelekeo na dalili ya
mafanikio hata kama wakati huo huna pesa. Unapokuwa na kitu hicho ni rahisi
kupiga hatua za kimafanikio. Kitu hiki si kingine bali ni matumaini.
Unapokuwa
unaishi kwa matumaini ya kutambua kwamba utafanikiwa huku lakini ukichukua
hatua karibu kila siku, ni rahisi kuweza kubadilika katika maisha yako na kuwa
mtu wa mafanikio.
Inapotokea
umeshindwa lakini ukawa una tumaini la kufanikiwa, hiyo itakupa nguvu tena ya
kujaribu kitu kipya katika safari yako ya mafanikio uliyonayo.
Matumaini
yanakupa nguvu ya kufanya zaidi na zaidi hata kama unachokifanya unaona kama
hakilipi kwa sasa, kwa sababu una matumaini ya kufanikiwa, ni lazima utafanya
hata kama upo kwenye hali ya mbaya kimafanikio.
Unaweza
ukawa una maumivu makubwa ya kushindwa kwa kile unachokifanya na pengine umekata
tamaa kabisa, lakini matumaini yatakuamsha na kusema fanya tena.
Lakini
hata hivyo, ili uweze kuwa tumaini sahihi la mafanikio yako mara nyingi
tumaini haliji hivihivi, ipo gharama
ambayo unatakiwa kuilipia ili kupata tumaini sahihi la kufanikiwa kwako.
Huwezi
kukaa tu, halafu ukategemea upate tumaini au kitu cha kukupa faraja ni lazima
ufanye kitu cha tofauti kila siku. Ni lazima uchukue hatua ya pale ulipo na
kutaka kwenda sehemu nyingine.
Ikiwa
utakuwa ni mtu wa kukaa tu na bila kuchukua hatua, elewa kabisa utahangaika
sana na utakuwa mtu wa kukosa tumaini karibu kila siku ya maisha yako na kuiona
dunia haifai.
Hakuna
kisingizio chochote katika hili, tumaini la mafanikio yako ni matokeo ya wewe kuwajibika
kwako kila siku. Ikiwa huwajibiki sahau kuwa na matumaini, utakuwa ni mtu wa
kukatishwa tamaa kila siku.
Watafute
watu ambao ni wakata tamaa maarufu, uangalie maisha yao yalivyo, utagundua ni
watu ambao mara nyingi hawachukui hatua sahihi za kuweza kubadili maisha yao.
Kitu
unachotakiwa kufanya ni kujenga tumaini jipya la mafanikio yako, kufanya kitu hata
kama ni kidogo ambacho lakini unaamini kitabadilisha maisha yako.
Kwa
kuishi maisha hayo hiyo itakusaidia sana kujitengenezea matumaini makubwa kwa
maisha yako na utapata hamasa ya kufanya mambo mengi yakuweza kubadili maisha yako.
Kitu
cha kukumbuka tumaini lolote lile linajengwa kwa wewe kuchukua hatua ya kufanya
kitu fulani ambacho unaamini ni msaada kwako, vinginevyo itakuwa ni ngumu sana
kufanikiwa.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Dec 26, 2016
Je, Unashindwa Kufanikiwa Kwa Sababu Ya Changamoto? Fanya Hivi…
Ni
hali ambayo hutokea kwa wengi unapokutana na changamoto au tatizo fulani kuona
kwamba kila kitu ni kibaya katika maisha, ingawa ukweli hauko hivyo.
Kwa
sababu ya tatizo linalokakubali ni rahisi kuona ndugu, rafiki, jamaa zako wote
wa karibu ni wabaya kwa sababu huoni ule msaada wao wa moja kwa moja
kukusaidia.
Usichokijua
yote hayo yanapotokea si uhalisia wa maisha jinsi ulivyo. Hakuna mtu mbaya sana
katika maisha yako hata mmoja. Si dunia wala ndugu zako ndio wabaya sana, vitu
vyote hivyo viko sawa.
Mbaya
wa kwanza katika hayo yote unayoyaona ni wewe mwenyewe, inawezekana hukusaidiwa
kwa sababu ni kweli watu hao hawakuwa na uwezo. Sasa kwa nini ulalamike.
Kama
hali au tatizo uliloingia limesababishwa na mwingine kwa namna moja au nyingine,
jiulize wewe unamchango gani wa kusababisha hali hiyo kutokea? Kwa sababu ni
lazima uwe na mchango wa aina fulani.
Hivyo unapoona una changamoto, ama tatizo fulani badala ya kulalalimikia wengine au kuumia chukua hatua muhimu ya kuweza kutatua tatizo hilo mpaka uweze kulishinda.
Kujijengea
tabia ya kuwa na lawama sana hakuwezi kukusaidia kitu hata siku moja. Unajiona
una tatizo au changamoto likabili kwa nguvu zote bil kutafuta ‘mchawi’ wa
tatizo lako.
Fanya
kitu juu ya changamoto yako. Hakuna wa kukusaidia usipokubali kufanya kitu cha
kuweza kukutoa kwenye changamoto ambayo inaweza ikawa inakukabili.
Unaweza
ukawa ni kweli hujisikii vizuri, unajisikia vibaya sana kiasi cha kwamba
unashindwa kuchukua hatua, lakini hebu fanya kitu ambacho kitakusaidia kutatua
changamoto yako hata kwa sehemu kidogo.
Acha
kuruhusu kusimama kimaisha kwa sababu ya changamoto zinazokuzunguka.
Acha
kuwa chanzo cha kujiangusha mwenyewe kwa sababu ya changamoto za kimaisha.
Fanya
kitu muhimu cha kukusaidia kuweza kusogea mbele kimafanikio hata ukiwa katikati
cha matatizo au changamoto zinazokuzunguka.
Kutokufanya
kitu, lisiwe moja ya suluhisho ambalo unaweza ukawa umechangua.
Kumbuka
unao uwezo wa kubadilisha maisha yako ukiamua, changamoto zisiwe kizuizi
kikubwa sana cha kukufanya ushindwe kufanikiwa.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
dirayamafanikio@gmail.com
dirayamafanikio.blogspot.com
Dec 20, 2016
Hiki Ndicho Kinachoitwa Kichaa Cha Mapenzi.
Kabla
mtu hajaoa au kuolewa , huamini kabisa kwamba, kabla hajafanya mapenzi au tendo
la ndoa na mtu anayemwita mpenzi wake, bado hawezi kudai kwamba, huyo mtu ni
mpenzi wake na kwajibika kwake kama mpenzi.
Vijana
wengi huamini kwamba, baada ya kukutana kimwili, ndipo wanaweza kudai kwamba,
hao ni wapenzi wao na kwamba kukutana kimwili, ndiyo mapenzi au kupenda kwenyewe.
Inapotokea
wanapokutana huvutiwa na tendo la ndoa, huamini kabisa kwamba, uhusiano nao
utakuwa mzuri. Kwao, tendo la ndoa ndio kipimo cha uimara wa uhusiano wao.
Baada
ya kufanya mapenzi, wapenzi hao huamini kwamba, sasa wanaweza kujitolea kwenye
uhusiano huo na kwamba, wanaweza kuwa na nguvu nao kwa asilimia kubwa.
Suala
hili, kuna wataalamu huliita mtego wa kimapenzi. Huitwa hivyo, kwa sababu
huwafanya wapenzi kutokuangalia sifa nyingine na badala yake kuweka nguvu
kwenye mwili, yaani tendo la ndoa.
Kuna wakati kupenda inakuwa kama upofu. |
Upofu
hutokea kutokana na kuzalishwa kwa kemikali nyigi mwilini, zenye kumfanya mtu
asiweze kujiuliza kuhusu maeneo mengine ya kimasha ya binadamu, zaidi ya mwili.
Kinachotokea
ni mwili kuvutwa na wale tunaowapenda kwa kuzalisha homoni inayofahamika kama ‘phenylethylamine’ au PEA kwa kifupi.
Kemikali
au homoni hii pamoja na nyingine kama vile ‘depomine’
na ‘norepinephrine’ (ambazo huchochea
hali za kimwili) na ‘ testosterone’(ambayo
huongeza hamu ya kujaamiana), huzalishwa mara baada ya kukutana kimwili.
Baada
ya kuzaliswa kwa homoni hizi, akili ya mtu huona mwili tu, yaani mapenzi na
siyo sifa nyingine. Hapa ndipo ambapo, mtu hujikuta hawezi kujizuia tena
kukutana kimwili na mpenzi wake, mara baada ya kukutana naye mara ya moja.
Baada
ya kufanya mapenzi na kufikia kileleni, huzalishwa homoni iitwayo ‘oxytocin’ (ambayo huhusika na mihemiko),
homoni hii humfanya mtu kujikuta anapenda kuwa karibu na kujifungamanisha na
mtu aliyefanya naye mapenzi. Tunaweza kusema, ukaribu kwa wapenzi wawili huongezeka
na unakuwa ni ukaribu wa mwili zaidi.
Kuzalishwa
kwa homoni hizi, ni jambo ambalo mtu hawezi kulizuia na huwa linakuja kwa nguvu
sana, kiasi kwamba, mtu kuwa kama amepoteza ufahamu wa maeneo mengineyo ya
kimaisha isipokuwa mapenzi tu.
Homoni
hizi humfanya mtu kuwa na hisia za kuvutiwa na mwingine, uchangamfu, ukaribu,
kuvutiwa na hisia za ukamilifu zaidi. Wale waliowahi kuwa na uhusiano wa
kimapenzi kabla ya ndoa au wale waliowahi au wanaotoka nje ya ndoa zao kwa kuvutwa
kimwili na wapenzi wengine, wanajua inavyokuwa.
Lakini
homoni hizi, hatimaye huanza kupungua na mtu huanza kuhisi kwamba alikosea. Huoni
tena na huhisi kama ilivyokuwa awali. Sasa haoni kuwa mpenzi wake ni mzuri au
anafaa kama iivyokuwa awali. Kwa sababu, homoni zile zimeshuka sana, mwili
unakuwa hauna maana tena.
Kwa
bahati mbaya kile kilichokuwa kinaitwa
upendo, kilikuwa kimefungiwa kwenye mwili na homoni hizo ambazo kwa sasa
hazipo. Hivyo, wapenzi hawana kingine cha kushika ambacho, wataweza kukiita
mapenzi.
Unajua
sasa ni kwa nini, tangu kale kabisa suala la wachumba kukutana kimwili kabla ya
ndoa lilikuwa likipingwa sana? ni kwamba, watu wanapokutana kimwili, uwezo wa
kukaguana tabia unakuwa umefungwa kutokana na kufumuka kwa homoni hizi, ambazo
hubadili hali ya mtu na hisia zake kwa ujumla.
Kwa
nini unadhani watu, hasa wanaume wakishaanza mapenzi ya kimwili na mtu mpya,
yaani nyumba ndogo au yeyote, inakuwa rahisi sana kwao kujisahau na kukamatwa? Sababu
ni hiyo hiyo, kwamba, uzalishwaji wa homoni hizi huwa ni mkubwa kiasi cha mtu
kuamini kwamba, hakuna kingine chene kufurahisha na kuliwaza kama uhusiano huo.
Kumbuka,
watu wawili wanapovutana, kwa maneno mengine tunasema kuna kemia kati yao. Hii ina
maana kwamba, huwa kuna mabadiliko ya badhi ya homoni kama nilivyosema. Lakini,
wanapokutana, homoni hizi huwa nyingi kiasi cha kufanya upofu wa muda. Unaweza kuwa
upofu wa mwezi, mwaka au miaka.
Upofu
huu unapmalizika, uhusianao huwa ni wa vurugu tupu, kwa sababu kama nilivyosema
awali, hqakuna mahali pengine pa kushika
siyo tabia, mienenfo waa haiba.
Upofu
huu unapomalizika, uhusiano huwa ni wa vurugu tupu, kwa sababu kama nilivyosema
awali, hakuna mahali pengine pa kushika siyo tabia, mienendo wala haiba.
Inashauriwa
kwamba, mtu anapovutiwa na mwingine au watu wanapovutana ni vema wakawa
wangalifu sana. kwanza, wajue kwamba, uhusino ambao msingi wake ni miili tu,
yaani tendo la ndoa haudumu, kwani homoni zitokanazo na kukutana watu kimwili,
hazina maisha, huwa zinaisha haraka.
Lakini
pia inashauriwa kwamba, mtu anapoingia kwenye mapenzi ajaribu kushariana au
kuukagua moyo wake, akili pamoja na hisia zake. Kuacha tu mabadiliko ya hali ya
mwili yakatawala ni kutafuta maumivu.
Hebu
jiulize, ni kwa nini mapenzi yanapoanza kwa moto sana, huzimika haraka au kwa kishindo sana? ni kwa sababu yanajengwa
kwenye msingi usioaminika, yaani katika mihemiko na kimapenzi. Penzi linalokua
polepole ndilo lenye kushika, kwani halina msingi wa mwili.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Dec 19, 2016
Je, Wajua! Kila Kitu Hutokea Kwa Sababu Maalumu?
Kijana mmoja baaada ya kuhitimu
masomo yake ya chuo alipanga kwenda kumtembelea mjomba wake ambaye kwa wakati
huo alikuwa anaishi kijijini. Kijana Aliamua kufanya hivyo kwani zilikuwa
zimepita siku nyingi bila kuonana kwa mjomba wake.
Hivyo siku uliyofuata kijana aliamka
asubuhi na mapema kabla jua halijaleta faraja kwa watu wake, alijiaanda
kwa kasi zaidi ya 4G kabla ya kuanza safari ya kuelekea kijijini
kwani muda haukuwa rafiki kwake.
Kwa kuwa safari ilikuwa ni ndefu sana
kijana huyo aliamua kubeba chakula ambacho kingemsaidia kupungunguza njaa
wakati wa safari, safari iliendelea huku kijana mawazo ya mjini akiyaacha na
wenye miji yao huku akili yake ikiwa ina shuaku na msukumo thabiti kuhusu
maisha ya kule kijinini.
Ilipofika mida ya muda wa mchana kwa
kuwa njaa ilikuwa inamuuma sana alichua chakula chake na kuanza kula.
Aliuamini ule usemi ambao unasema "usiudharau mkono kwa sababu ya
kijiko" hivyo chakula kile alikula kwa kutumia mkono ambao anaumini
zaidi, lakini kama ujuavyo wakati wa safari utaratibu wa kunawa mikono wakati
wa safari huwa si zingatio sana aliamua kula bila hata kunawa mikono yake.
Baada ya dakika chache kula chakula
kile, tumbo la ghafla lilimkamata huku akikaa kila aina ya mkao ujuao wewe
katika siti ile, alifanya vile ili kuyanusuru maumivu ambayo yalikuwa
yametawala katika tumbo. Hata hivyo kadri muda ulivyozidi kuyoyoma na tumbo
nalo lilikuwa linazidi kuuma zaidi.
Aliwaza ni kitu gani ambacho
kimesababisha tumbo lake kuuma, lakini kadri anavyozidi kuzama katika dibwi la
halmashauri ya fikra zake aligundua ya kwamba chakula alichokula kulikuwa ni
chanzo cha kuuma kwa tumbo lake.
Hivyo safari iliendelea mpaka
alipowasili katika kijiji ambacho alikuwa anaishi mjomba wake.
Mjomba alifurahi kumuona kijana yule,
lakini mjomba alishtuka kumuona kijana yule akiwa hana furaha, ndipo mjomba
akaamua kushirikisha mdomo katika kumuuliza swali kijana yule ni kipi ambacho
kimemtoa katika ulimwengu furaha, ndipo kijana akamueleza mjomba wake tumbo
lilikuwa linamsumbua kidogo.
Baada ya mjomba kusikia hayo
alimueleza ya kwamba asipate tabu kwani atakuwa sawa muda si mrefu, walipofika
nyumbani kwa mjomba, mjomba alimpa dawa za miti shamba, kijana yule baada
ya kula alikuwa sawa.
Baadae mjomba pamoja na kijana yule
walikaa katika mkeka kwa ajili ya kupata chakula. Chakula chenyewe ulikuwa ni
ugali wa mhogo pamoja nyama ya swala.
Chakula kile kilikuwa ni kitamu sana
kwani kilikuwa kimepikwa kwa ustadi wa hali ya juu sana. Wakati wanaendelea
kula huku hadithi mbalimbali zilikuwa zimetawala mahali pale kwani muda mrefu
ulikuwa umepita bila wao kuonana. Lakini katika ya maongezi yao mjomba
hakusahau kumpongeza kijana yule kwa kuhitimu masomo yake ya chuo.
Basi huku maongezi yao yakiendelea
walijikuta chakula kimeisha bila hata wao kujua. Hivyo kijana yule akaona asiwe
mchoyo wa fadhira hivyo akaamua kumshukuru mjomba kwa chakula kitamu, lakini
zaidi alisema ya kwamba alifurahishwa na nyama ile.
Lakini mjomba alimuahidi siku
iliyofuata kwamba wangeambatana pamoja kwenda kuwinda pamoja. Kijana yule
alifurahi maneno hayo kutoka kwa mjomba wake kwani alitamani kujua mbinu
amabazo zilitumika kuwinda. Kwani alimini ule usemi "usimpe mtu
samaki" bali mpe samaki siku ya kwana siku inayofuata mpe nyavu akavue
mwenye.
Ilipofika asabuhi na mapema kila
mmoja aliamka akiwa ni mzima wa afya tele, kijana alimuuliza mjomba wake ni
muda gani ambao wangeenda mawindoni? Mjomba akamwambia ya kwamba muda wa
kufanya mawindo ni muda wa usiku ambapo wanyama wengi huwa wamechoka sana.
Hivyo ingefaa waendee muda usiku.
Hivyo ilipofika usiku mjomba pamoja
na kijana yule walichukua dhana za uwindaji kwa ajili ya kuelekea mawindoni.
Harakati za mawindo zilikuwa zimepamba moto katikati ya msitu, lakini matarajio
yao yalikuwa hayapo sawa kwani hawakupata hata mnyama mmoja lakini hawakukata
tamaa waliendelea kufanya mawindo.
Muda ulizidi kwenda bila ya kupata
chochote. Kijana yule alikuwa amechoka sana, kwani aliamini ya kwamba kufanya
mawindo ni kitu rahisi sana. Kwa kuwa kijana yule alikuwa amechoka sana, licha ya
kuchoka alikuwa tayari ana usinginzi mzito, Hivyo mjomba aliamuru washushe hema
ili waweze kupumzika. Waliingia ndani ya hema na kulala ndani ya hema.
Baada ya dakika chache wote
walipitiwa na usingizi mzito ndani ya hema lile, baada ya masaa machache mjomba
alishtuka usingizini hivyo akaamua amuamshe kijana yule. Mjambo alimuasha
kijana yule, kijana aliamka, mjomba akamuuliza kijana "unaona nini
angani?" kijana akajibu naona nyota pamoja na mwezi unaoangaza kwa
mwanga mzuri.
Mjomba akauliza tena
"unachokiona kinamanisha nini? Kijana akajibu ya kwamba kile anachokiona
ni ishara ya kwamba Mungu yupo pamoja nao, pia mng'ao wa nyota
zinaonyesha ya kwamba siku uliyofuata ilikuwa ni njema . mjomba akasema umejibu
vyema, lakini tumeibiwa hema hivyo kikubwa zaidi nilitegemea utajibu ya kwamba
"tumeibiwa hema"
Mwisho umejifunza nini kupitia kisa
hiki?
Tafsiri ya kisa hicho ni;
Kisa cha hadithi hii ni kwamba wapo
baadhi ya watu wamekuwa na maisha magumu kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa
kupambanua vitu kwa mapana, hata hivyo naweza nikasema tumekuwa tukiishi
katika hali ya kimazoea. Wengi tumekuwa tukitazama mambo kwa kuanza na vitu
ambavyo vinaonekana mbali kuliko kuanza na vitu vilivyopo karibu.
Kwa mfano wahitimu wengi wa vyuo
huamini ya kwamba baada ya kuhitimu masomo yao ni ajira, wao hawaamini ya
kwamba wanaweza kujiri. Wapo baadhi ya watu ambao wanaishi mahali fulani
wanawaza kwenda sehemu nyingine huku wakiamini kufanya hivyo ni njia ya
mafanikio kwao, lakini ukweli ni kwamba kila mahali ambapo leo hii upo pana
fursa.
Hivyo chunguza kwa umakini na uweze
kujua fursa zile ambazo zinakuzunguka ndipo uje kuwaza fursa ambazo zipo
nje na hapo ulipo.
Mwisho nimalize kwa kusema ya kwamba
kiporo hakihitaji moto mwingi, maana yangu ni kwamba mafanikio yako hayahitaji
mambo makubwa sana ila yanahitaji kujiongeza zaidi kwa kila kitu ambacho
unakifanya.
Ndimi; Afisa mipango Benson Chonya,
0757909942
Dec 16, 2016
UTAFITI; Mwanamke Huota Tofauti Na Mwanaume.
Wanasema
mwanamke na mwanaume ni tofauti kwenye baadhi ya mambo, kimaumbile. Lakini, sio
yale mambo yenye kuonekana peke yake, kwani imebainika sasa ni kwamba, tofauti
huenda hadi kwenye usingizi. Ni kwamba mwanamke na mwanaume huota tofauti.
Kwa
hiyo, hata wakiwa usingizini, mwanamke na mwanaume wanaendelea na tofauti zao.
Dk.
Mark Blagrove, ambaye ni mtaalamu wa saikolojia, anasema kwamba, yeye pamoja na
mwenzake wamefanya utafiti kwa watu zaidi ya 100,000 na kubaini kwamba, kuna
tofauti kati ya mwanamke na mwanaume hasa linapokuja suala la kuota ndoto.
Utafiti
uliofanywa na Blagrove na wenzake umehusisha watu wa dunia nzima, sio ulaya na
marekani peke yake.
Hivyo,
ni utafiti ambao unazungumzia jambo linalohusu dunia nzima, siyo upande fulani
tu wa dunia.
Ipo tofauti kubwa kati ya ndoto ya mwanaume na mwanamke. |
Katika
utafiti huo, wamegundua kwamba, wanandoa ambao wamelala kitanda kimoja, ubavu
kwa ubavu, wanakuwa na ndoto tofauti kabisa, ingawa wanaweza wakawa wanaota
wakati mmoja.
Ndoto
za wanawake zinaonekana wazi zinahusu kazi, zimejaa hisia sana ndani yake na
huchukua muda mrefu zaidi.
Mwanamke
anaweza kusimulia kuhusu ndoto yake, ukadhani imechukua saa kadhaa kuota kwa
jinsi ilivyo ndefu. Huwa wanaota ndoto moja kwa muda mrefu zaidi.
Ndoto
za wanawake zimejengwa kwenye msingi wa nyumbani na kuhusisha watu wengi na
hasa wa familia zaidi, kuliko watu wa nje ya familia.
Kwa
upande wa ndoto za wanaume, kuota wageni ni jambo la kawaida sana kwao. Wageni,
ina maana watu ambao hawawafahamu. Ndoto za wanaume zimejengwa kwenye msingi wa
maeneo ya barabara, magari na vurugu.
Hauwezi
kupita muda mrefu kabla mwanaume hajaota kuhusu gari, barabara au vurugu za
aina fulani.
Huhusisha
pia tendo la ndoa na wanawake wasiowajua, mara nyingi.
Ndoto
za wanaume pia zimejengwa pia kwenye mazingira ya kazi, na kuhusiana na hofu za
kipato na hofu za kupoteza kazi au kufilisika. Zimejaa masuala ya kazi au
shughuli.
Mwanasaikolojia
aliyeandika pia vitabu kadhaa kuhusu ndoto, Veronica Tonay, anasema, utafiti
huu unathibitisha tafiti za siku nyingi ambazo zilikuwa zinadai kwamba,
wanawake huota tofauti na wanaume.
Hivi
sasa, inaweza kusemwa kwamba, suala hilo halina utata tena. Inaonyesha pia
kwamba, zaidi ya nusu ya watu wote wanapata ndoto mbaya angalau mara moja kwa
wiki.
Kuna
wengine ambao ndoto mbaya ni sehemu ya maisha yao ya kindoto,yaani karibu kila
siku zinawatokea.
Inaelezwa
kwamba, kazi anayofanya mtu inaweza kuchangia kwenye kuwa kwake na ndoto za
jinamizi au ndoto mbaya.
Kwa
mfano, wauguzi wahasibu na watumishi kwenye vyombo vinavyohusiana na
mawasiliano, ndiyo ambao hukumbwa sana na ndoto hizi mbaya.
Kukimbizwa,
meno kudondoka, kuanguka, kutegewa au kuwekewa kizuizi, ni miongoni mwa mada
zinazootwa sana, hasa na wale wanaoota majinamizi.
Wanasaikolojia
wanasema, ndoto zinahusiana na shughuli ambazo hatujazimaliza kwenye mpangilio
wetu wa kazi wa siku au kujaribu kufanya kile ambacho tulishindwa kukifanya
tukiwa macho.
Kwa
mfano, kuota kupata fedha, jambo ambalo katika hali ya kawaida, limekuwa gumu
kwetu.
Watafiti
hapo wanazidi kuchambua ndoto kwa kusema kwamba, ndoto zinazohusu mambo mabaya
ndizo ambazo zinaotwa zaidi kuliko zile zinazohusu mambo mazuri.
Hata
wale watu wenye furaha maishani, wanaonekana kuota ndoto zenye mada
zisizopendeza kuliko mada zenye kupendeza.
Ingawa
wataalamu wa ndoto wanasema, kila ndoto ina maana kutegemea na mtu aliyeota,
utafiti huu unaonyesha kwamba, pamoja na kuwa hilo ni kweli, kuna mambo ambayo
mtu mmoja akiyaota , maana yake ni ile ile kwa mtu mwingine yeyote.
Kwa
mfano, kuanguka, kwenye ndoto ina maana ya mtu kukosa uhakika wa usalama.
Kukimbizwa
au kufukuzwa, bila kujali ni nani anaota, inaweza kuwa na maana ya kukimbia
matatizo.
Ndoto
ya kupoteza au kung’oka meno inahusiana na mtu kujali namna anavoonekana au
sura.
Ndoto
ya mtu kukimbia, lakini lakini akajikuta bado yupo pale pale, yaani hasogei,
ina maana au inahusiana na mtu kuwa na kazi nyingi kumzidi uwezo.
Ndoto
ya mtu kuwa uchi, ina maana kwamba, mhusika ana matamanio ya kuwasiliana na
mwingine au wengine.
Kile
ktiendo cha kuvua nguo ndotoni kina maana ya mtu kuondoa vikwazo vinavomkabili
kwenye maisha ake.
Pamoja
na kwamba, lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuona kama mwanamke na mwanaume
wanaota tofauti, bado umezaa masuala mengine muhimu ynayohusiana na ndoto. Moja
ya hili lilozaliwa ni maana ya ndoto, ambazo hazibadiliki, bila kujali ni nani
ameziota.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Dec 15, 2016
Ifahamu Nguvu Ya Kufikiri Na Kushukuru Katika Maisha.
Katika vitu ambavyo wanadamu tumekuwa
hatuvitilii maanani ni vitu vikubwa viwili, vitu hivyo ni kufikiri na
kushukuru. Nimesema hivyo nikiwa na ushahidi tosha kwa kile ambacho nakiamini,
na pia ni sahihi kwa asilimia zote ambazo unazifahamu wewe.
Unashangaa kwanini nasema kwa
kujiamini? Wala usishangae bali tuendelee kusonga mbele mwanzo mpaka mwisho wa
makala haya ili tuweze kwenda sawa.
Ukweli ambao upo wazi ambao hauhitaji
hata mwanga wa jua ili kuonekana kwa watu wake upo bayana kabisa, ni kwamba
tumekuwa tukilalamika kwa kutoa sauti au hata kutotoa sauti ya kwamba maisha ni
magumu.
Yote hiyo inaweza ikawa hivyo kwa sababu watu tumeshindwa kuwekeza muda wetu katika suala zima
la kufikiri, huenda nikawa nimekuacha ila nataka tusemezane bila kuoneana haya.
Ipo sababu kubwa leo kuweza kutenga muda kwa kila siku angalau masaa mawili kwa
ajili ya kufikiri, si kufikiri tu bali kufikiri vitu vipya.
Kama unafanya biashara, kilimo au
kitu chochote ni vyema ukatenga angalau masaa hayo mawili kwa ajili ya
"kuwaza". Kufanya hivyo kutakufanya uweze kuwa bora hatimaye kuonesha
utofauti na wengine.
Itumie nguvu a kufikiri vizuri ikusaidie kufanikiwa. |
Hakuna maisha bora kama utaamua
kufanya kitu kile kile, kila wakati kwa njia ambazo umezizoea. Fanya kitu cha
tofauti kwa kuwa wewe ni wa tofauti.
Na kama ilivyo kauli mbiu ya mtandao
huu ni kwamba badili maisha yako kwa kuwa na fikra sahihi, hivyo fikiri sana
kwani fikra chanya huleta mabadiliko ya kweli hakuna jambo lolote litafanikiwa
kama litakuwa katika mtazamo hasi.
Lakini tukija katika upande wa pili
ni kwamba katika vitu ambavyo havipo katika tamaduni zetu ni jambo zima la
kutoa "Shukrani" kutoa shukrani ni jambo la faraja sana mbele za
Mungu na mwanadamu ambaye amekusaidia wewe kwa namna moja ama nyingine kuweza
kufika hapo ulipo.
Elewa na tambua ya kwamba usingefika
hapo ulipo kama ungesimama peke yako. Mbele ya Mafanikio yako kuna mtu nyuma
yake. Swali la kujiuliza ni shukrani gani ambazo umezitoa kwa mtu huyo?
Ukifikiri kwa umakini utagundua ya
kwamba hakuna hata mtu mmoja ambaye umewahi kutoa shukrani kwake, hii ni kwa
sababu shukrani zetu ni za mara moja kama mla ndizi.
Naendelea kujihoji pasipo kupata
majibu ni maisha gani hayo ambayo umeyachagua? Kwanini uishi maisha hayo
yasiyokuwa na faida na chukizo mbele za Mungu?
Unafikiri ya kwamba ukitoa shukrani
kwa Mwenyezi Mungu na mtu ambaye amekusaidia kuwa hapo utapungua uzito au
utafirisika? La
hasha binafsi naona kama ukiweka
utaratibu wa kushukuru itakusaidia kuweza kufanikiwa zaidi.
Huenda ninachokisema leo kikagusa moja
kwa moja. Utajiuliza labda leo Afisa mipango kaamuka na mimi, la hasha kwa kuwa
mawazo yangu hayana ukomo wa kuwaza wacha niseme tu, huenda yakagusa kwa namna
moja ama nyingine na yakakusaidia.
Nguvu ya kushukuru huongeza baraka za
kimafanikio kila wakati, haiwezekani wewe ukawa ni mtu kuomba tu kuliko
kushukuru, kufanya hivyo ni sawa na bure hata vitabu vya dini havijakaa mbali
nasi kwani vinatukumbusha ya kwamba "kila
ajuaye kuomba lazima ajue na kushukuru".
Hivyo jiwekee utaratibu wa kufikiri
na kushukuru ili uweze kupata amani ya moyo hatimaye kufikia ile ndoto kubwa
uliyonayo. Kama umenielewa vizuri baada ya kumaliza kusoma makala hii chukua
dakika chache kuwashukuru wote ambao wamekusaidia kufika hapo ulipo.
Lakini ikumbukwe kumshukuru mtu ni lazima
umwambie mtu huyo. Pia utakuwa mchoyo wa fadhira kama utashindwa kujishukuru
mwenyewe. Endapo nimekukwaza utanisamehe sana kwani wajibu wangu kukueleza
ukweli kila nipatapo nafasi.
Ndimi :Afisa Mipango Benson Chonya,
Dec 13, 2016
Siri 6 Za Kuishi Maisha Ya Ushindi.
Kwa
kawaida zipo siri na mbinu nyingi sana za kukusaidia kuishi maisha ya ushindi
wakati wote. Hakuna haja ya kulaumu au kulalamika maisha ni magumu, zipo siri za kukusaidia
kukabiliana na changamoto zako.
Leo
kwa kifupi, naomba nikushirikishe mbinu au siri chache za mafanikio ambazo
zitakusaidia kukupa hamasa na nguvu ya kuishi kwa ushindi na mafanikio makubwa
sana.
1. Kila wakati, pambana na mambo magumu, wakati
mambo hayo bado ni rahisi. Pambana na changamoto zako, wakati changamoto hizo
bado ni kidogo. Pambana na kuitunza afya yako, wakati bado umzima. Pambana na
umaskini, wakati bado ukijana mwenye nguvu.
Kila changamoto unayokutana nayo kwenye maisha,
unaweza kuishinda ikiwa utakabiliana nayo mapema. Acha kusubiri mambo
yameharibika ndio uanze kukomaa na changamoto yako. Acha kusubiri nyumba
imeungua ndio utafute maji ya kuzimia moto.
Jifunze kutokuishi maisha ya zima moto. Ishi kwa mipango
sahihi, ambayo mipango hiyo mwisho wa siku itakuongoza wewe kuweza kufikia
katika mafanikio yako makubwa. Wengi wanashindwa katika maisha kwa sababu ya
kuchelewa kuthibiti mambo ambayo walitakiwa wayathibiti mwanzoni.
Jiulize ni mara ngapi umekwama, kwa sababu ya
kushindwa kuithibiti hali fulani ambayo ulitakiwa kuithibiti mapema? Acha
kuendelea kuharibu maisha yako kwa kusubiri eti mpaka mambo yameharibika ndio
utafute dawa yake. Changamka sasa na anza kutekeleza majukumu yako mapema.
7
Tunza na kuilea ndoto yako kwa uangalifu, ili ikupe mafanikio. |
2. Siku zote katika safari ya mafanikio, kuwa
makini sana na jinsi unavyoitunza na kuilea ndoto yako. Kama ndoto yako
unaitunza na kuilea katika hali ya hofu na mashaka sana basi, utavuna magugu na
hautaweza kufanikiwa.
Na pia kama ndoto yako unatitunza na kuilea katika
matumaini makubwa ya kufanikiwa, imani ya mafanikio na kujiamini, uwe na
uhakika ni lazima utafanikiwa. Wapo wengi wanaoshindwa kufikia ndoto zao kwa
sababu ya kuzielea ndoto zao katika mazingira mabovu.
Kama ulivyo mmea ili ukue ni lazima umwagaliwe maji
safi, halikadhalika ndoto yako iko hivyo
hivyo. Ni lazima ndoto yako ituzwe kwa matumaini na imani ya mafanikio na sio
kuitunza katika hofu na woga ambapo mwisho wa siku ni lazima utakwama.
Najua hapo ulipo una ndoto ya iaina fulani, jiulize
unailea ndoto yako katika mazingira yapi? Je, unajiamini utafanikisha? Au au upo
kwenye mazingira ya mashaka na hofu? Mazingira yoyote yale unayoyatumia
kuilelea ndoto yako yanakupa jibu kama utafanikiwa au hautafanikiwa
kuifanikisha ndoto yako.
3. Ili kufikia mafanikio zaidi ya hapo ulipo, ipo
haja na ulazima wa wewe kujituma na kufanya kazi kwa bidii sana nje ya yale
mazoea uliyojiwekea. Kwa mfano, kama umezoea kufanya kazi kwa saa 8, ongeza masaa
mengine manne ya ziada. Kama umezoea kuamka sa 12, anza kuamka saa 11 alfajiri.
Fanya kitu ambacho kitakutoa nje ya mazoea yako yaani ‘comfort zone’. Kwa chochote kile unachokifanya, fanya nje ya mazoea
yako. Hiyo itakusaidia sana kujenga misuri mikubwa ya kukuwezesha kufika mabali
kimafanikio.
4. Kwa hali yoyote ile ambayo inatokea nje ya
wewe haina mchango mkubwa sana wa kuweza kukukwamisha au kukufanya ushindwe
kufikia mafanikio yako. Kitu ambacho kitakufanya ushindwe kufanikiwa ni ile
hali inayotokea ndani mwako tu.
Hali hiyo inayotokea ndani mwako, ndiyo ina nguvu
kubwa sana ya kubadillisha maisha yako na kuwa ya mafanikio kabisa. Hebu
jiulize kila unapowaza mafanikio, ndani mwako unajionaje? Unajiona ni kwamba
utafanikiwa au utashindwa? Kipi unachokiona ndani mwako?
Haijalishi watu wanasemaje au watasema nini juu
yako, hata watu dunia nzima waseme kwamba utafanikiwa, lakini kama ndani yako
huoni hivyo ni wazi huwezi kufanikiwa, pia hata dunia nzima iseme kwamba wewe
ni wa kushindwa, lakini ikiwa ndani yako unajiona wewe ni mtu wa mafanikio,
utafanikiwa.
Kiti kikubwa hapa, jifunze kutokulaumu hali yoyote
ile, inayotokea nje katika maisha yako kwamba ndio imekukwamisha. Anayejizuia
na kujikwamisha sio mwingine bali ni wewe mwenyewe na hali hasi nyingi ulizozibeba.
Kuanzia leo amua kujenga hali bora ndani mwako itakayokupa mafanikio makubwa.
5. Kuna wakati unaweza ukajikuta unaumia sana
kwenye maisha yako, hiyo yote kwa sababu ya maoni hasi ya watu wanayokutolea
wewe. Sasa ili usiendelea kuumia kwa jambo hilo, kumbuka hivi, hicho ambacho
kinaongelewa juu yako ni kwa mujibu wa maoni yao wao wenyewe. Uhalisia wa wewe
jinsi ulivyo unaujua wewe.
Hivyo, acha kuchukua maoni ya watu na ukaamua
kuyatumia kuendesha maisha yako. Alooo! Ukifanya hivyo utamuia sana na utaiona
dunia chungu. Ishi wewe kama wewe kwa kufata kile ambacho moyo wako unakutuma
na hiyo itakufanya uishi maisha ya ushindi na mafanikio makubwa.
6. Kitu pekee kitakacho kufanikisha si wingi wa
maarifa ya mafanikio unayoyapata kila siku. Mafanikio yako utayapata kwa wewe
kuamua kuyatumia maarifa hayo tena kwa uhakika.
Jiulize leo hivi, tokea uanze kujifunza juu ya
mafanikio, umechukua hatua kiasi gani? Au umebakia kuwa ni mtu wa kushangilia
na kuwaacha wengine wachukue hatua za kimafanikio?
Kama makala hii
imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI
KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)