Dec 13, 2016
Siri 6 Za Kuishi Maisha Ya Ushindi.
Kwa
kawaida zipo siri na mbinu nyingi sana za kukusaidia kuishi maisha ya ushindi
wakati wote. Hakuna haja ya kulaumu au kulalamika maisha ni magumu, zipo siri za kukusaidia
kukabiliana na changamoto zako.
Leo
kwa kifupi, naomba nikushirikishe mbinu au siri chache za mafanikio ambazo
zitakusaidia kukupa hamasa na nguvu ya kuishi kwa ushindi na mafanikio makubwa
sana.
1. Kila wakati, pambana na mambo magumu, wakati
mambo hayo bado ni rahisi. Pambana na changamoto zako, wakati changamoto hizo
bado ni kidogo. Pambana na kuitunza afya yako, wakati bado umzima. Pambana na
umaskini, wakati bado ukijana mwenye nguvu.
Kila changamoto unayokutana nayo kwenye maisha,
unaweza kuishinda ikiwa utakabiliana nayo mapema. Acha kusubiri mambo
yameharibika ndio uanze kukomaa na changamoto yako. Acha kusubiri nyumba
imeungua ndio utafute maji ya kuzimia moto.
Jifunze kutokuishi maisha ya zima moto. Ishi kwa mipango
sahihi, ambayo mipango hiyo mwisho wa siku itakuongoza wewe kuweza kufikia
katika mafanikio yako makubwa. Wengi wanashindwa katika maisha kwa sababu ya
kuchelewa kuthibiti mambo ambayo walitakiwa wayathibiti mwanzoni.
Jiulize ni mara ngapi umekwama, kwa sababu ya
kushindwa kuithibiti hali fulani ambayo ulitakiwa kuithibiti mapema? Acha
kuendelea kuharibu maisha yako kwa kusubiri eti mpaka mambo yameharibika ndio
utafute dawa yake. Changamka sasa na anza kutekeleza majukumu yako mapema.
7
Tunza na kuilea ndoto yako kwa uangalifu, ili ikupe mafanikio. |
2. Siku zote katika safari ya mafanikio, kuwa
makini sana na jinsi unavyoitunza na kuilea ndoto yako. Kama ndoto yako
unaitunza na kuilea katika hali ya hofu na mashaka sana basi, utavuna magugu na
hautaweza kufanikiwa.
Na pia kama ndoto yako unatitunza na kuilea katika
matumaini makubwa ya kufanikiwa, imani ya mafanikio na kujiamini, uwe na
uhakika ni lazima utafanikiwa. Wapo wengi wanaoshindwa kufikia ndoto zao kwa
sababu ya kuzielea ndoto zao katika mazingira mabovu.
Kama ulivyo mmea ili ukue ni lazima umwagaliwe maji
safi, halikadhalika ndoto yako iko hivyo
hivyo. Ni lazima ndoto yako ituzwe kwa matumaini na imani ya mafanikio na sio
kuitunza katika hofu na woga ambapo mwisho wa siku ni lazima utakwama.
Najua hapo ulipo una ndoto ya iaina fulani, jiulize
unailea ndoto yako katika mazingira yapi? Je, unajiamini utafanikisha? Au au upo
kwenye mazingira ya mashaka na hofu? Mazingira yoyote yale unayoyatumia
kuilelea ndoto yako yanakupa jibu kama utafanikiwa au hautafanikiwa
kuifanikisha ndoto yako.
3. Ili kufikia mafanikio zaidi ya hapo ulipo, ipo
haja na ulazima wa wewe kujituma na kufanya kazi kwa bidii sana nje ya yale
mazoea uliyojiwekea. Kwa mfano, kama umezoea kufanya kazi kwa saa 8, ongeza masaa
mengine manne ya ziada. Kama umezoea kuamka sa 12, anza kuamka saa 11 alfajiri.
Fanya kitu ambacho kitakutoa nje ya mazoea yako yaani ‘comfort zone’. Kwa chochote kile unachokifanya, fanya nje ya mazoea
yako. Hiyo itakusaidia sana kujenga misuri mikubwa ya kukuwezesha kufika mabali
kimafanikio.
4. Kwa hali yoyote ile ambayo inatokea nje ya
wewe haina mchango mkubwa sana wa kuweza kukukwamisha au kukufanya ushindwe
kufikia mafanikio yako. Kitu ambacho kitakufanya ushindwe kufanikiwa ni ile
hali inayotokea ndani mwako tu.
Hali hiyo inayotokea ndani mwako, ndiyo ina nguvu
kubwa sana ya kubadillisha maisha yako na kuwa ya mafanikio kabisa. Hebu
jiulize kila unapowaza mafanikio, ndani mwako unajionaje? Unajiona ni kwamba
utafanikiwa au utashindwa? Kipi unachokiona ndani mwako?
Haijalishi watu wanasemaje au watasema nini juu
yako, hata watu dunia nzima waseme kwamba utafanikiwa, lakini kama ndani yako
huoni hivyo ni wazi huwezi kufanikiwa, pia hata dunia nzima iseme kwamba wewe
ni wa kushindwa, lakini ikiwa ndani yako unajiona wewe ni mtu wa mafanikio,
utafanikiwa.
Kiti kikubwa hapa, jifunze kutokulaumu hali yoyote
ile, inayotokea nje katika maisha yako kwamba ndio imekukwamisha. Anayejizuia
na kujikwamisha sio mwingine bali ni wewe mwenyewe na hali hasi nyingi ulizozibeba.
Kuanzia leo amua kujenga hali bora ndani mwako itakayokupa mafanikio makubwa.
5. Kuna wakati unaweza ukajikuta unaumia sana
kwenye maisha yako, hiyo yote kwa sababu ya maoni hasi ya watu wanayokutolea
wewe. Sasa ili usiendelea kuumia kwa jambo hilo, kumbuka hivi, hicho ambacho
kinaongelewa juu yako ni kwa mujibu wa maoni yao wao wenyewe. Uhalisia wa wewe
jinsi ulivyo unaujua wewe.
Hivyo, acha kuchukua maoni ya watu na ukaamua
kuyatumia kuendesha maisha yako. Alooo! Ukifanya hivyo utamuia sana na utaiona
dunia chungu. Ishi wewe kama wewe kwa kufata kile ambacho moyo wako unakutuma
na hiyo itakufanya uishi maisha ya ushindi na mafanikio makubwa.
6. Kitu pekee kitakacho kufanikisha si wingi wa
maarifa ya mafanikio unayoyapata kila siku. Mafanikio yako utayapata kwa wewe
kuamua kuyatumia maarifa hayo tena kwa uhakika.
Jiulize leo hivi, tokea uanze kujifunza juu ya
mafanikio, umechukua hatua kiasi gani? Au umebakia kuwa ni mtu wa kushangilia
na kuwaacha wengine wachukue hatua za kimafanikio?
Kama makala hii
imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI
KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.