Nov 2, 2016
Namna Bora Ya Kuendelea Kuishi Hata Ukiwa Umekufa.
Pamoja na malengo
mengi uliyonayo katika miasha yako, lipo kusudi na lengo moja kubwa sana katika
maisha ambalo hutakiwi kulisahau kabisa. Lengo hilo ni kufanya maisha ya wengine
kuwa ya maana na furaha.
Siku zote katika
maisha yako, jitahidi sana kufanya maisha ya wengine kuwa ya maana, bora na furaha
kwa sababu yako wewe. Uwezo wa kutekeleza hilo najua unao na hakuna cha
kukuzuia.
Kwa chochote kile unachofanya
iwe kwa kusema au kwa kutenda, hakikisha unafanya maisha ya wengine kuendelea
kuwa bora. Epuka kabisa kuumiza watu katika maisha yako kwa jinsi yoyote ile.
Ifanye dunia iwe na
furaha kwa sababu yako wewe, wafanye watu wale wanaokuzunguka wawe pia na
furaha na mafanikio kwa sababu yako wewe, ukifanya hivyo unajitengenezea njia
bora ya kuishi hata ukiwa umekufa.
Katika maisha kitakachokufanya
ukumbukwe siku ukifa si kwa sababu ya pesa ulizonazo au umeishi miaka mingi
sana duniani, bali ni kwa namna gani jinsi ulivyogusa maisha ya watu ikiwa ni
pamoja na kuwapa furaha.
Unapofanya maisha ya
wengine kuwa ya furaha, bora na yenye maana unakuwa unajenga kumbukumbu kubwa
sana mioyoni mwao ambayo sio rahisi kusahaulika, na inakuwa ni njia bora kwako
ya kuishi mara mbili wakati upo hai na hata ukiwa umekufa.
Naamini unawajua
watu vizuri ambao majina yao hayaachwi kutajwa pamoja na kwamba kwa sasa
hatunao katika hii dunia. Kilichowafanya wawe hivyo ni kwa sababu ya kufanya
maisha ya watu wengine kuwa ya maana na furaha.
Bila shaka
tunakubaliana hakuna asiyewajua watu kama Nelson
Mandela, Nkwame Nkruma, Samora Machel na wengineo wengi ambao walipigania
ukombozi wa nchi zao.
Siri kubwa ya watu
hwa kuweza kukumbukwa kama nilivyosema ni ile kufanya maisha ya watu wengine
kujengwa katika msingi wa furaha, amani, matumaini na mafanikio makubwa.
Suala la kufanya
maisha ya wengine yawe ya furaha na ya maana, lifanye kama kuwa jukumu lako.
Anzia hapo ulipo ulipo kufanya maisha ya wengine kuwa na furaha na yenye maana
kubwa.
Acha kujiuliza sana
utafanikishaje hili au utaanzaje? hutakiwi kuwa na wasiwasi sana kwani ni jambo
ambalo halihitaji pesa, bali ni uamuzi
wako wewe mwenyewe wa kuanza.
Yapo mambo ya
msingi ambayo unatakiwa uyazingatie ii kufanye maisha ya wengine yawe na maana
na furaha. Mambo hayo ni kama haya hapa yafuatayo.
Kwa kile unachokisema,
sema kwa maneno ya kutia moyo na sio kuumiza hapo utakuwa umefanya maisha ya wengine
yawe ya furaha na maana kubwa sana duniani.
kwa kile
unachoandika, jitahidi sana kuandika mambo ambayo yatatoa tumaini na nuru kubwa
kwa maisha ya wengine leo na hata miaka mitano, kumi au hata miaka mia moja
ijayo.
Kwa mitazamo
uliyonayo, hakikisha unakuwa na mitazamo ambayo inakusaidia wewe na wengine
kuwajengea faraja na matumaini makubwa ya mafanikio yao.
Pia hata nguvu na
juhudi zako za kusaidia jamii ni lazima ziweze kuonekana za maana sana ambazo
zinalenga si kukusaidia wewe tu, bali hata na kuwasaidia na wengine kufikia
malengo yao.
Kila wakati ishi
maisha ya kutoa maana kwa maisha ya watu wengine. Unapoishi maisha ya kutoa
maana kwa watu wengine na kuepuka ubinafsi wa kila aina hapo unakuwa unajitengenezea
njia ya ukika ya kufikia mafanikio makubwa.
Tunakutakia kila la
kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Endelea kujifunza
kupitia dirayamafikio.blogspot.com kila siku.
Napenda pia
kukaribisha wewe rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na jina
lako kwenda 0713 048035 ili
uanganishwe. Hakuna gharama na karibu sana.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.