Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, March 2, 2018

Acha Kusubiri Hali Ya Hatari, Badili Maisha Yako Sasa.

No comments :
Antony Burges alikuwa na umri wa miaka 40, kipindi ambacho daktari wake alimwambia hawezi kupona tena ugonjwa wa kansa uliokuwa unamsumbua. Taarifa hiyo ya daktari  ilisisitiza kwamba ni lazima Antony afe tena ndani ya muda wa mwaka mmoja.
Kwa Antony ilikuwa ni habari mbaya sana kwake na tena iliyomshtua. Kilichokuwa kikimsikitisha Antony si kwa sababu anakwenda kufa, bali alisikitishwa na ujio wa kifo chake huku akiwa hajatimiza kabisa ndoto zake.
Alichokuwa akiwaza kila wakati inakuwaje anakwenda kufa wakati ndoto zake hazijatimia? Kutokana na maswali hayo ndiyo yalimfanya arudi tena kwa daktari kuumuliza ni kweli hawezi kabisa kupona ugonjwa huo wa kansa?
Lakini katika hali ya kusikitisha Antony alipewa jibu lile lile na kuambiwa isingewezekana kupona, ni lazima angekufa. Juhudi za madaktari bingwa ili kuokoa maisha yake wakati akiumwa zilikuwa zimefika ukomo, ilikuwa ni lazima afe.
Antony alirudi nyumbani kwa masikitiko mkubwa na akiwaza kwamba sasa anakwenda kufa kifo cha aibu. Anakwenda kufa akiwa maskini ambaye hajaweka historia yoyote, hicho ndicho kilichomkera.

Acha kusubiri hali ya hatari, fanya kitu cha kubadili maisha yako kila siku.
Akiwa kwenye chumba chake anachoishi huku akiwa katika hali ya kukosa matumaini ya kuishi,   alikumbuka kitu na kuapa asingeweza kufa bila kuacha kitu chochote cha kukumbukwa duniani.
Hapo ndipo alipokumbuka kwamba anakipaji cha kuandika. Aliapa ni lazima afanye kitu hata kama muda wa kuishi umekwisha. Ilikuwa ni lazima aandike ‘novel’ ambazo zitasomwa wakati akiwa amekufa. Hicho ndicho kilichotokea.
Katika kipindi cha mwaka mmoja akiwa anasubiri kifo chake, Antony Burges aliweza kuandika ‘novel’ tano, ambapo kitu hichohicho alishindwa kukifanya katika maisha yake yote mpaka pale alipopigiwa kengele ya kifo.
Ilikuwa sio rahisi kukamilisha kazi hiyo kwa kipindi cha muda mfupi, lakini iliwezekana. Unajua ni kwa nini? ni kwa sababu kifo kilikuwa kinamsubiri, na ilikuwa ni lazima akamilishe malengo yake kabla hajafa.
Hata hivyo lakini, zikiwa zimebaki siku chache ili kipindi cha mwaka mmoja kikamilike na afe kama daktari alivyodai alirudi hospital tena. Daktari aliyemkuta, alimfanyia vipimo upya na alimwambia uwezekano wa kufa katika kipindi hicho cha mwaka mmoja haupo tena.
Kwa taafrifa hiyo mpya kutoka kwa daktari ilimpa Antony nguvu mpya, nuru mpya na tumaini jipya la maisha. Antony kwa hasira za mafanikio aliamua sasa kuandika vitabu vingine vingi kwa nguvu zaidi. Aliweza kuandika vitabu vingine zaidi ya 70, mara baada ya kupona kutoka kifo chake.
Aligundua swala la kusubiri mpaka itokee hali ya hatari ndio ufanye kitu katika maisha yako ni baya sana. Utakuta wengi wanashindwa kufanikiwa kwenye maisha yao kwa sababu ya kufanya mambo yao mpaka wasubiri taa nyekundu.
Wengi wetu ukichunguza katika maisha bado tupo kama Antony wa zamani, ni watu ambao utakuta tumeficha vipaji na uwezo mkubwa ndani yetu bila kuutumia. Utakuta tunakutakuja kuutumia uwezo huo mpaka pale kengele ya hatari igonge vichwani mwetu.
Jiulize ni mara ngapi hutaki kufanya mambo yako kwa wakati mpaka usukumwe? Kama unaishi maisha ya kusukumwa sukumwa hadi hali mbaya zikutokee mafanikio yanakuwa magumu sana kuonekana kwako.
Yapo mambo kadhaa ambayo tunaweza kujifunza kupitia Antony Burges, miongoni mwa hayo ni:-
Kwanza, jifunze kutumia uwezo wako wote ulionao unapokwa hai. Acha kusubiri hali ya hatari ndio uanze kutumia uwwezo wako kukufanikisha. Acha kusubiri watoto wamefukuzwa shule ndio uanze harakati za kutafuta ada.
Kwa muda na rasilimali yoyote uliyonyo itumie vizuri kwa wakati ili ikusaide kukupa mfanikio unayoyataka kwenye maisha yako. Unao uwezo mkubwa sana, utumie wakati wote kuleta mabadiliko katika maisha yako na ya wengine.
Pili, hata siku moja usikatishwe tamaa na kitu chochote hata kama ni kifo. Katika mazingira magumu ambayo Antony alikuwa ameshaambiwa ni lazima atakufa, lakini aliweza kufanya kazi bila kufikiria hilo na kufanikisha ndoto yake.
Alichokuwa akitaka kuona ni ndoto zake zinatimia ilikuwa haijalishi mazingira anayopita ni ya aina gani. Alikuwa anajua kabisa siku zake za kuishi ni chache, lakini ilikuwa ni lazima apigane mpaka mwisho.
Tatu, wakati wote ukitaka kuwa mshindi katika kila eneo acha kusubiri hali ya hatari, fanya sasa kutimiza ndoto zako. Pigania ndoto zako wako bado ukijana. Pigania ndoto zako wakati bado una afya na nguvu za kutosha. Pigania ndoto zako mpaka tone la mwisho.
Inapotokea mazingira ya kukatisha tamaa, usikubali mazingira hayo yawe ndio eti sababu ya wewe kushindwa. Ukisubiri kama Antony kutokufanya kitu utatakuwa unajichelewesha mwenyewe kufikia mafanikio yako.
Kila wakati kumbuka mafanikio yako yanawezekana, badili masiha yako kwa kuwa na fikra sahihi.
Nikutakie siku njema na anasante sana kwa kutembelea  DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza. Washirishi na wengine waweze kupata maarifa haya bora.
Pia napenda kukukaribisha rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 04 80 35 ili uanganishwe.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,


No comments :

Post a Comment