Dec 12, 2016
Maadili Yakufuata Ili Kufikia UTAJIRI.
Kila
kitu katika maisha ili uweze kukipata kina misingi na maadili yake. Hakuna kitu
au mafanikio ambayo unaweza ukayapata kiholela, ni muhimu kwako kufuata maadili
yake tena ikiwezekana kila siku ili uweze kufanikiwa.
Kwa
mfano, yapo maadili ya msingi ya kufuata kwa mwanamichezo, mwanafunzi, mfanyabiashara
au daktari hadi kufanikiwa. Ukiangalia kila eneo la maisha hadi lilete
mafanikio linahitaji maadili ya aina fulani hivi.
Hata
linapokuja suala la kutafuta mafanikio na utajiri kwa ujumla yapo maadili ya
msingi ambayo ni lazima uyafuate ili ufanikiwe. Haya ndiyo maadili ambayo
karibu kila mtu ambaye ni tajiri anayatumia.
Je,
unataka kujua ni maadili yapi ya msingi ambayo unatakiwa kuyafuata ili uweze
kufanikiwa na kuwa tajiri? Hilo lisikupe shida, fuatana nami katika makala haya
na tujifunze pamoja.
1.
Kufanya kazi kwa bidii.
Kati
ya kitu muhimu ambacho kinauwezo wa kukutoa kwenye umaskini na kukufanya ukawa tajiri
ni kufanya kazi kwa bidii zote. Hakuna ubishi katika hili, ikiwa utajitoa
kufanya kazi kwa bidii ni lazima utafanikiwa tu.
Unaweza
leo hii ukawa maskini wa kutupwa lakini kesho utakuwa tajiri kama utajitoa
kufanya kazi kwa bidii sana. Haya ni maadili ya msingi sana kuyafuata kila siku hasa kwa mtu yeyote anayetaka
kufanikiwa na kuwa tajiri.
Jiwekee nidhamu binafsi, itakayokusaidia kutengeneza utajiri. |
2.
Ung’ang’anizi.
Ili ufanikiwe na kuwa tajiri, moja ya maadili ambayo unatakiwa kuwa nayo ni kwa
wewe kukubali kuwa king’ang’anizi. Huwezi ukafanikiwa ikiwa hautakuwa king’angazi
hasa kwa yale mambo unayoyafanya.
Ukiangalia
sifa na maadili yaliyowafanya matajiri kupata utajiri wao ni kule kung’ang’ania
kwao. Waliposhindwa jambo fulani, hawakuona kwamba hicho ndicho kikwazo bali
waling’ang’ania hadi kufanikiwa.
3.
Nidhamu binafsi.
Hutaweza
kufanikiwa na kuwa tajiri katika maisha yako kama huna nidhamu binafsi. Maisha yako
ya mafanikio yanajengwa hasa kwa wewe kujitengenezea nidhamu binafsi katika
kila eneo.
Kwa
mfano, unatakiwa kuwa na nidhamu binafsi kwenye kazi unayoifanya, matumizi yako yako ya
pesa na hata nidhamu binafsi kwenye malengo uliyojiwekea. Utafanikiwa na kujenga mafanikio makubwa kama
una nidhamu binafsi.
4.
Kujiamini.
Maadili
mengine ya msingi ambayo unatakiwa kuwa nayo ni kujiamini kwako. kila wakati ni
muhimu kujiamini ili ufanikiwe. Mara nyingi watu wanaojiamini ndio
wanaofanikiwa sana.
Unapokuwa
unajiamini inakusaidia sana hata katika changamoto nyingi uweze kukabiliana
nazo na kuzishinda. Ikiwa nia yako ni kufikia utajiri mkubwa, hebu anza kwa
kujiamini kwanza.
5.
Kufanya kazi kwa mwendelezo.
Kile
kitu ambacho umekichagua kukifanya ni muhimu sana kukifanya kwa mwendelezo kila
siku. Hata kama ni kwa kidogo lakini kitu hicho ni lazima ufanye kila siku ili
kikupe nguvu ya kukufanikisha.
Wanaofanikiwa
si kwamba wanauwezo mkubwa sana kama unavyofikiri, bali mambo yao huyafanya
kila siku. Weka nguvu zako kwa kile unachokifanya kila siku, ni lazima utapata
matokeo ya kukusaidia kufanikiwa.
6.
Simamia maamuzi yako.
Lazima
uwe na maamuzi ambayo hayabadiliki badiliki. Ukisema mwaka huu nakwenda kufanya
jambo hili ni vyema ukatekeleza jambo hilo na sio kuwa mtu wa kuacha acha.
Kwa
jinsi unavyozidi kuwa na maamuzi imara ni msaada kwako wa kuweza kukusaidia
kufikia malengo ya aina fulani ambayo unakuwa umejiwekea tena kwa wakati
mwafaka.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.