google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 24, 2015

Faida 7 Za kufanya Mazoezi Ya mwili.

No comments :
Kuwa na afya bora ni msingi wa mafanikio yote. Hata uwe na mipango na malengo mazuri vipi lakini kama afya yako ni mbovu huwezi kuyafikia mafanikio hayo unayoyataka. Unapokuwa na afya bora inakuwa inakupa nguvu ya kuishi maisha bora wakati wote na kufanya mambo mengi bila kuteteleka.
Kama ambavyo waswahili wanasema ‘mwili haujengwi kwa matofali’ ndivyo hivyo afya hii tunayaoizungumzia haiji kwa bahati mbaya tu. Mara nyingi vyakula tunavyokula na aina ya maisha tunayoyaishi karibu kila siku ndiyo inayotuamulia afya zetu ziweje kwa sasa na baadae
Kama unaishi maisha ya kulakula hovyo tu bila utaratibu kamwe usitegemee ikawa rahisi kujenga afya bora ni lazima itakusumbua. Vilevile hata kama hujihusishi na mazoezi nayo pia itakuwa ni tatizo kwa afya yako. Ili ufanikiwe ni muhimu kutambua kitu cha kwanza kukilinda ni afya kuliko kitu chochote kile.
Kwa hiyo utakuja kuona kuwa chakula bora chenye virutubisho vyote muhimu, ni kitu cha lazima na msingi sana kwa afya zetu. Lakini mbali vyakula hivyo pia tunaona hata mazoezi yanahusika pia katika kutupa afya zetu kwa kiasi kikubwa kuliko wengi tunavyofikiri.
Wengi huwa tunaona mazoezi ya mwili yanafanyika lakini huwa hatujui yanafanya kazi gani hasa kwenye hii miili yetu. Mara nyingi zipo faida nyingi za kufanya mazoezi ambazo siyo rahisi kuzitambua ikiwa hujafanya uchunguzi hata kidogo. Faida hizo ni kama hizi zifuatazo:-

1. Mazoezi ya mwili husaidia kulirekebisha shinikizo la damu.
2. Mazoezi ya mwili huiruhusu damu nyingi zaidi kuzifikia sehemu zote za mwili na kuifanya mikono na miguu ipate joto.
3. Mazoezi ya mwili yanaondoa mambo yote mawili. Yaani mkazo wa mwili na mfadhaiko wa moyo, na kukusiadia wewe kujisikia vizuri zaidi katika maisha yako. Mazoezi ya mwili kwa kawaida ni tiba bora kabisa ya wasiwasi na msongo (stress).
4. Mazoezi ya mwili hutupatia nguvu ya umeme kwa ajili ya ubongo wetu pamoja na seli za neva. Yanaongeza afya kwa kuuamsha mfumo wa kinga mwilini (immune system). Mwili unapowekwa katika hali ya afya kwa kufanya mazoezi yanayofaa. Ubongo unakuwa na uwezo wa kufikiri kwa ubunifu na ufanisi zaidi.
5. Yanaweza kukusaidia kuiweka vizuri rangi ya uso wako na kukuweka katika hali nzuri kabisa kimwili. 
6. Mazoezi ya mwili hukufanya uwe na nguvu nyingi zaidi, hivyo kuchelewesha kupatwa na uchovu kimwili na kimawazo 
7. Yanausaidia ubongo wako kutengeneza dawa inayokupa wewe hali ya kujisikia vizuri na kukuongezea uwezo wa kustahimili maumivu.
Endapo wewe ulikuwa hufanyi mazoezi, basi anza taratibu (polepole) na kuongeza nguvu yake hatua kwa hatua upatapo uwezo wa kustahimili.
Nakutakia kila la kheri katika maendeleo ya afya na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
 Imani Ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035 kwa ushauri na msaada wa haraka.



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.