Jan 11, 2018
Zijue Kanuni Bora Za Mafanikio Yako Kwa Mwaka 2018.
U hali mpenzi msomaji wetu wa mtando huu wa DIRA YA MAFANIKIO, bila shaka u mzima na unaendela vyema na
majukumu yako ya kila siku.
Kama ulivyo msemo, usemao kizuri kula na wenzako basi nami bila
hiana nakukaribisha jamvini ili tule kwa pamoja chakula kinachoitwa“kanuni za mafanikio kwa mwaka 2018”.
Naomba utambue ni chakula ambacho hakina madhara yeyote katika
afya yako, lakini pili chakula hiki pindi utakapokula kitakupa mwangaza mpya wa
maisha yako. Nimeona nikwambie mapema faida ya chakula hiki ili usije ukasema
umeshiba.
Miongoni mwa kanuni muhimu ambazo unatakiwa kuzifahamu katika
mwaka huu ili uweze kufanikiwa katika maisha yako ni kama ifuatavyo;
1. Elimu.
Kila kitu ambacho unakiona katika dunia hii, ipo misingi mikuu
ya elimu hadi kitu hicho kimeweza kufanikiwa. Hatuzungumzii elimu ya darasani
pekee, la hasha zipo elimu nyingine ambazo hazikuitaji uiingie darasani
bali unaweza kujifunza kutoka sehemu tofauti tofauti mbali na kukaa
darasani.
Elimu hii unaweza kujifunza kwa watu ambao tayari wamekwisha
fanikiwa au katika vyazo mbalimbali vya utoaji elimu kama vile makongamono,
warsha,vitabu na katika mitandao ya kijamii.
Hivyo ili uweze kuwa bora katika maisha yako ya kila siku hasa
katika mwaka huu 2018, ni vyema ukawekeza muda mwingi katika kujifunza katika
jambo hilo. Kwani ukweli ambao upo bayana kwa wote waliofanikiwa ni kwamba watu
hao wamewekeza muda mwingi katika kujifunza, na kujifunza huku hakikisha hakuna
ukomo.
2. Hamasa.
Jambo la pili ili uweze kufanikiwa zaidi katika mwaka huu ni vyema
ukahakiisha ya kwamba unakuwa na hamasa ya kuweza kufanikiwa zaidi, na hamasa
hii itokane na njaa ya kufanikiwa, hivyo kila wakati ni lazima utafute kitu
ambacho kitakupa motisha ya kuweza kufanikiwa ziaidi.
Na miongoni mwa vitu hivyo kwanza hakikisha unazungukwa na
marafiki sahihi lakini pili hakikisha ya kwamba kwa jambo lolote ambalo
unalifanya unakuwa unalipenda.
3. Kutenda jambo hilo.
Mara baada ya kupata elimu, hamasa jambo linalofuata ni kutenda
jambo hilo. Mara nyingi watu wengi huwa wanapata elimu na hamasa tu,
jambo ambalo linafanya watu hao waweze kukomea kwenye hatua hizo mbili tu. Ila
kwa kuwa wewe ni msaka mafanikio na unataka kufanikiwa zaidi ni vyema
ukahakiisha ya kwamba unafika mpaka hatua ya tatu ya kulitenda jambo hilo, na
katika kulitenda jambo hilo ni hakikisha unalitenda kwa juhudi zote ulizonazo.
Mwisho nimalize kwa kusema ya kwamba kanuni ambazo zitakusaidia
wewe uweze kufanikiwa katika maisha yako ni ELIMU+HAMASA+KUTENDA=MAFANIKIO.
Ndimi Afisa Mipango Na
Mafanikio Benson Chonya
07576-909942.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.