Jan 27, 2018
Utengenezaji Wa Chakula Cha Kuku Kwa Kutumia Mchwa.
Rafiki, mchwa na funza
ni chakula bora sana kwa kuku. Chakula hiki kina protini kwa wingi sana
kwa mifugo yetu, ili kuku aweze kukua vizuri na kuwa na uzito mzuri anahitaji
vyakula vyenye protein kwa wingi.
Wadudu jamii ya funza
na mchwa ni jamii ya wadudu ambao wana protin nyingi, iwapo kuku wako utawapa
chakula hiki basi kuku wako watakuwa kwa haraka na watakuwa na uzito mkubwa
ambao itakua ni faida kwako.
Pia chakula hiki cha
mchwa na funza kinapunguza changamoto ya magonjwa kwa kiasi fulani hasa yale
magonjwa yanayotokana na lishe. Mpaka hapo unaona faidaya wazi itokanayo na
chakula hiki cha mchwa na funza.
1. UTENGENEZAJI WA FUNZA.
Ili uweze kutengeneza
funza unahitaji kuwa na vitu vifuatavyo; Nailon, samadi, maji na jembe na eneo
la kutengenezea.
Jinsi ya kutengeneza funza;
Tengeneza tuta.
Weka nailoni katika
tuta lako.
Weka samadi yako
(samadi mbichi ya Ng'ombe)
Weka udongo kwa mbali
kwa juu katika samadi yako.
Mwagia mwagia maji,
ninaposema mwagia mwagia maji namaanisha nyunyuzia maji katika tuta lako kwa
kiasi kidogo.
Funika juu kwa nailoni
katika eneo ambalo umetengeneza tuta lako hakikisha kusiwe na jua kali.
Katika tuta lako
hakikisha kunakuwa na unyevu unyevu.
Baada ya siku kumi
funua nailoni lako utakuta kunafunza wengi waache kuku wako wale hadi
watakapomaliza.
Baada ya kumaliza kula
funika tena na nailoni baada ya siku mbili utakuta tena kuna funza wakutosha
hivyo unatakiwa utengeneze matuta mawili au zaidi kwa ajili ya chakula kwa
mifugo yako,
2. UTENGENEZAJI WA MCHWA.
Ili kutengeneza mchwa
unahitaji kuwa na vitu vifuatavyo;
Samadi ya ng'ombe, maranda
ya mbao au majani makavu au mabua mahindi,
Mabox au chungu.
Jinsi ya kutengeneza mchwa.
Chukua samadi ya ng'ombe
changanya na maranda ya mbao vizuri mwagia maji michanganyiko wako
ulowane vizuri.
Weka kwenye
chungu au box michanganyiko wako.
Chukua chungu/box lako
weka katika njia ya mchwa kwa maana sehemu yenye asili ya mchuguu ambapo mchwa
wanapatikana.
Baada ya siku tatu
utaona box lako linamejaa mchwa chukua ka wape kuku wako wale.
Hapa ndipo mwisho wa
somo letu la leo natumaini umejifunza mengi katika somo la leo nenda kayafanyie
kazi haya uliyojifujifunza ili kuboresha mifugo yako.
MUHIMU;- Chakula hiki kitumike
kama chakula cha ziada.
Nikutakie utekelezaji
mwema na tutaonana wakati ujao, usipange kukosa mfululizo wa makala hizi.
NI MIMI RAFIKI YAKO,
FRANK MAPUNDA,
0758918243/0656918243.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.