Jan 8, 2018
Misingi Ya Maisha Na Mafanikio Kutoka Kwenye Kitabu Cha The Top 200 Secrets Of Success And The Pillars Of Self-Mastery.
Hiki ni kitabu
kilichoandikwa na mwandishi Robin Sharma kwa malengo ya kuonyesha sheria na kanuni
mbalimbali za maisha ambazo inatakiwa kuzisimamia na kuzifanyia kazi kila siku kwenye
maisha yako kwa kiasi kikubwa sana.
Ni kitabu kifupi ambacho
ukikazana kukisoma ni rahisi tu kukimaliza kwa siku moja, kwani ni kitabu ambacho
hakina maelezo marefu sana na yapo mambo mengi ya kujifunza lakini, yafuatayo
ni baadhi ya machache yake.
1.
Tenga jumapili moja kila wiki, halafu tafuta muda ambapo kila jioni unakuwa
unakaa angalau saa moja na kuanza kutafakari juu ya maisha yako wapi unapotoka
na wapi unapokwenda na kisha kupanga mipango ya wiki linalofuata. Tabia hii
ukiisimamia kiuhakika, itakufanya upige hatua sana.
2.
Kaa karibu na watu ambao utaamua kujifunza vitu kutoka kwao. Usikae na watu
ambao wanaweza kukuzamisha kimaisha, watu hao ni hatari sana kwenye maisha yako
kimafanikio na ni rahisi kukurudisha nyuma.
3.
Usiende kitandani kulala ukiwa na kazi yoyote ya kufanya au kuna jambo la kina
la kulifikiria. Kitandani pako pafanye iwe ndio sehemu ya wewe kwenda kupumzika,
ukienda kulala, na ulale kweli kama mtoto mdogo mdogo.
4.
Usijaribu kula masaa matatu kabla hujalala. Kiafya, inashauriwa kula masaa
zaidi ya matatu kwa sababu hiyo inakuwa inapelekea mwili wako unafanya
mmeng’enyo bora wa chakula, kinyume na ukila ndani ya saa tatu na ukalala,
unaharibu afya yako.
5.
Kila siku fanya mambo makubwa mawili ambayo kikawaida hupendi kuyafanya. Kwa
kufanya mambo hayo mawili, inakusaidia kujenga sfa za ushupavu wa kufanya mambo
mengine tena zaidi na zaidi yatakayokuweka kwenye ngazi kubwa ya mafanikio.
6.
Furaha ya kweli ndani yako inakuja, mara baada ya wewe kuweza kutimiza malengo
yako. Ukishatimiza malengo yako ile furaha ya kweli inajengeka ndani yako kwa
kiasi kikubwa sana, haijalishi yawe malengo yako binafsi au malengo mengine ya
kawaida.
7.
Kila siku unapochagua kufanya kitu au unapochagua kufanya jambo la aina fulani,
unatakiwa kwenda hatua ya ziada. Usijjichangamnye ukafanye na ukaishia pale tu,
nenda hatua ya ziada na hapo utakuwa unatengeneza mafanikio makubwa sana kwa
upande wako wakati wote.
8.
Lala kidogo kwa wastani, tumia kidogo matumizi yako na fanya kazi kwa nguvu
sana, na mafanikio utayaona kwa upande wako.
9.
Usiruhusu kujadili mipango ya maendeleo yako binafsi na watu wengine.
Unachotakiwa kufanya ni kuwaacha watu hao waone MATOKEO na si MCHAHAKATO wa
kila hatua unayopitia. Kujadili mipango
ya maendeleo yako binafsi na watu wengine, huko ni kujianika sana na kujiruhusu
ujulikane kwa uwazi bila sababu.
10. Vitu
vinagunduliwa kwa namna mbili tu. Kwanza, kwenye akili yako na pia ni nje
katika umbo la kawaida. Kwa mfano; nyumba inaanza kujengwa kwenye karatasi
kwanza, halafu unakuja kuiona nje ikiwa nyumba halisi ikionekana.
Chukua
hatua kila siku kujifunza haya muhimu uliyojifunza.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.