Jan 9, 2018
Mambo Matatu Ya Kukusaidia Kuboresha Kipato Chako Kwa Uhakika.
Msingi
wa kujenga kipato kikubwa na hatimae kuwa huru kifedha huwa haupatikani kwa
bahati mbaya. Msingi huo zaidi unapatikana kwa wewe kujua zaidi mambo ya msingi
yatakayoweza kukusaidia kuboresha kipato chako kila iitwapo leo.
Kwa kawaida
kuna mambo ambayo ukiyajua yana msaada mkubwa sana katika kukusaidia kuweza
kuboresha kipato chako. Mambo haya wengi tunayajua ila kwa sababu sisi ni
binadamu tunakuwa tuna yasahau sana.
Kupitia
makala haya nataka nikuonyeshe mambo ya msingi matatu, ambayo ukiyazingatia
yatakusaidia sana kuweza kuboresha kipato chako karibu kila siku na maisha yako
yakawa bora zaidi. Mambo hayo ni yapi? Karibu tujifunze.
Jambo la kwanza; angalia matumizi yako.
Ni wazi
kabisa matumizi uliyonayo yanaweza kukusaidia kuboresha kipato chako au
yakakiharibu kabisa. Kama matumizi yako ni mabaya kipato chako hakiwezi kuwa bora
pia hata iweje, lazima utakuwa una kipato kibovu tu ambacho hakitakusaidia.
Hapa
unaona, eneo mojawapo la kushughlika nalo sana kama unataka kuboresha kipato
chako ni juu ya matumizi uliyonayo. Matumizi uliyonayo ukiweza kuyapangili a
vizuri, itakusaidai kuweza kupiga hatua ya kukusaidia kuboresha kipato chako kwa
kiasi kikubwa.
Jambo la pili; angalia uwekaji wako wa
akiba.
Je,
una weka akiba vya kutosha au unaweka akiba kama matone ya mvua kwa kurasha rasha
au huweki akiba kabisa? naamini majibu hapa unayo wewe mwenyewe kipi ambacho
unakifanya kwenye swala zima la uwekaji wa akiba.
Ukiweza
kuboresha juu ya uwekeji wako wa akiba vizuri uwe na uhakika hata matumizi yako
yatakuwa vizuri sana kiasi cha kwamba kuweza kuboresha kipato chako na
kukusaidia hata kuweza kuwekeza kwenye miradi mingine.
Jambo la tatu; angalia jinsi
unavyowekeza.
Najua
unaweza ukawa kweli matumizi yako sasa yako sawa, na umeamua kuweka akiba je,
kitu kingine unawekeza? Kama huwekezi unategemea kipato kimoja na pia hapo hapo
ukategemea kipato ulichonacho kibadilike naomba hapo usahau.
Mafanikio makubwa ya kuweza kufikia ngazi ya kuongeza kipato chako na wewe hadi kufikia
uhuru wa kifedha yanapatikana kutokana na wewe kuweza kuwekeza. Usipowekeza sahau
mafanikio hayo.
Ni muhimu
na msingi sana kuzingatia matumizi yako ya pesa, uwekaji wako wa akiba na
kuwekeza pale unaotafuta kuboresha kipato chako kwenye maisha. Unapozingatia mambo
hayo uwe na uhakika kipato chako lazima kitakuwa bora hata kama kwa sasa mambo
yanaonekana mabaya.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.