Jan 21, 2018
HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Anayetaka Usawa Sana Mwisho Wake Hugeuka Mchawi.
Karibu rafiki na mpenzi
msomaji wa mtandao wako wa DIRA YA
MAFANIKIO, sina shaka kwa wakati huu ni mzima wa afya na upo tayari katika
siku ya leo kuweza kujifunza hekima za maisha na mafanikio kama ilivyo kawaida
yetu. Naamini unaendelea kujifunza kupitia hapa jamvini na unapata kitu cha kukusaidia.
Kumbuka kama ninavyokwambia
kila wakati, hekima za maisha na mafanikio zinakupa busara za maisha na
mafanikio, zinakujengea misingi ya kimafanikio na hata uelewa wa kujua mambo
kadhaa wa kadhaa kupitia babu zetu ama unaweza ukawaita wahenga wetu wa zamani,
yote haya unayapata hapa ukiwa DIRA YA
MAFANIKIO kila jumapili.
Sitaki nikuchoshe kwa maneno
mengi sana, nikukaribishe tena jamvini tuweze kujifunza hekima za maisha na
mafanikio za siku hii ya leo.
1. Anayetaka usawa sana mwisho wake hugeuka mchawi.
Katika hekima hii ya maisha
na mafanikio ina maana kwamba, tukiwa
sisi kama binadamu tukubali kuwa binadamu kutofautiana kupo. Siyo kwa sababu fulani
kapata baiskeli ni lazima na wewe upate au fulani kapata nyumba na wewe
unawaza lazima nami nipate kwa njia
yoyote hata isiyo ya halali.
Maneno kama haya mwishowe
humsukuma mtu kutumia hila mbaya au njia zisizo za kawaida kama vile uchawi au
kila aina ya dhuluma aijuae yeye ili kumwezesha kupata mafanikio hayo. Hekima hii hutumika
sana katika kuwaonya wanaopenda
kujikweza na kujiona wao ni wao kwamba kila kitu lazima wapate kama wanavyowaona
wengine.
Watu hao wanasahau kuwa si
kila kitu mnaweza kuwa sawa. kujaribu kuwa sawa na watu wengine kwa kila kitu
huko ni sawa na kutafuta kwako wewe kuweza kujiumiza. Kwa kuliona hili, hekima
za maisha na mafanikio zimeweka wazi, ukitaka usawa mwisho wake hugeuka kuwa
uchawi na huo ndio ukweli halisi hata kama unauma.
2. Mwenda
usiku amesifiwa kulipokucha.
Kuna wakati unaweza ukawa
unatenda jambo la aina fulani ambalo jambo hilo watu wengine wanakuwa hawalijui
kabisa. Mtu huyu anayetenda jambo lisiilofamika katika hekima anafananishwa na mtu mwenda usiku au mtu yule anayetembea
usiku asijue ni nini kilichopo mbele yake ilimradi tu anaenda.
Kwa kawaida mtu huyu anayetembea usiku au anayetenda
jambo ambalo kwa wakati ule wengine hawalielewi na inapotokea jambo hilo linapoonyesha
mafanikio ndipo watu wanaanza kumsifu. Hekima hii hutumika sana kwa mtu
anayechekwa na wenziwe juu ya jambo alitendalo iwapo wakati ule wale wamchekao
hawaelewi usahihi wa lile alitendalo.
Si busara na si uungwana kuanza
kumcheka mtu kwa kitu usichokijua hata kidogo na wakati mwenzio anakifanya. Kama
ni kufanya mwache afanye, lakini ukiendelea kucheka yakitoka mafanikio jiandae
kumsifia. Wapo watu ambao wanaonekana mashujaa baada ya kubezwa sana, ndio
maana hekima zinatufundisha mwenda usiku amesifiwa kulipokucha.
Fanyia
kazi hekima hizi na zikusaidie kuchukua hatua na kuhakikisha ndoto zako
zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.