Jan 15, 2018
Kama Utashindwa Kuangalia Matokeo Haya, Huwezi Kunikiwa Hata Kidogo.
Yapo
mambo mengi sana tunatoweza kuyapata kwenye maisha kila siku na tusijue chanzo
chake nini. Kwa mfano, unaweza ukashangaa una maisha ya hovyo sana na hata usijue
sababu yake hasa, basi tu unaishia kusema mimi ndivyo nilivyopangiwa.
Ukiangalia
katika uhalisia wa ndani, ni nani wa
kukupangia maisha yako yakawa ya hovyo au ni kweli kwamba wewe una mikosi kama
ambavyo unasema, kimsingi yote hayo unayoyasema unajidanganya tena mchana
kweupe.
Kiuhalisia
kunakuwa na chanzo, ambacho kinafanya maisha yako yawe hivyo yalivyo iwe mazuri
au mabaya. Na chanzo hicho kwa bahati mbaya au nzuri kinaanzia ndani mwako
wewe, yaani chanzo hicho kinakufanya uwe na maisha hovyo au mazuri.
Naona
unanishangaa sana na kuanza kutafuta sababu za kujitetea kwamba, sasa iweje
mimi nisababishe maisha yangu mwenyewe yakawa ya hovyo? Yaaa, inawezekana tu,
ikiwa utashindwa kuangalia matokeo yanayosababishwa na mawazo na matendo
yako.
Kila
mara utajikuta ni mtu wa kuanguka sana, utakuwa unaanza jambo, lakini kabla
hujafika kule linakotaka kufika ili likupe mafanikio, unashangaa tena
umeshashindwa, unasimama tena kuanza kingine tena unashindwa.
Unapokuja
kuangalia kwa umakini kwa nini wewe uko hivyo unakuja kugundua ni matokeo ya wewe
kushindwa kuwa mwangalifu na matokeo yanayotokana na mawazo na matendo yako ya
kila siku, hapo tu ndipo unapokwama.
Inabidi
tukubaline ili ufanikiwe, Kila kitu unachokwenda kukifanya kwenye maisha yako unapaswa kuangalia matokeo yake kwanza. Uelewe
tu kwamba kila kitu unachokifanya kina matokeo yanaweza yakawa ni matokeo ya
kukufanikisha au kukufanya ushindwe.
Na matokeo
hayo kwa bahati mbaya au nzuri huwa hayatokei sasa hivi, yanakuja kutokea kwa
baadae hata miaka kumi mbeleni, lakini yanakuwa ni matokeo ambayo yanatokana na
mambo fulani hivi uliyoyafanya zamani kwa kipindi cha nyuma.
Matokeo
utakayoyapata yanawezea kutokana na mawazo yako au hata vitendo vyako. Mawazo yako
ya aina fulani hivi, yanaweza kukuzalishia matokeo ambayo unataka au huyataki,
halikadhalika na vitendo vyako hivyo hivyo, vinaweza kukupa matokeo.
Kupata
matokeo hayo yawe mazuri au mabaya, yote hiyo inategemea sana na kesho yako
wewe unataka iweje. Ikiwa unataka kesho yako iwe bora, basi uwe na uhakika
utakuwa makini sana na mawazo na vitendo unavyochukua kwa sasa.
Haitawezekana
hata kidogo uwe na mawazo ya hovyo na vitendo vya hovyo wakati unatengeneza
maisha yako ya kesho. Hapa ni lazima itafika mahali utatuliza sana akili yako
ili kuweza ‘kuatamia’ kile kilichochema
kwako.
Ukiona
mtu mawazo yake yako hovyo hovyo na hajatulia kabisa, unapaswa kujua hata kesho
yake haiwezi kuwa ya mafanikio itakuwa ni ya hovyo pia hivyo hivyo. Mawazo na
hatua zako zinatakiwa kuwa makini sana kila wakati.
Ndio
maana tunakwambia sana ni muhimu sana kuangalia matokeo haya ya kesho kabla
hujatumia mawazo yako na kabla hujachukua hatua. Unatakiwa ujenge utamaduni wa
kujiuliza mara mbil mbili kwamba je, hiki unachokiwaza kipo sahihi au la.
Amua
kila wakati kupata matokeo unayoyataka kwa kuwa mwangalifu sana wa mawazo na
matendo yako. Ukifanya uamuzi huo utakufanya uwe mshindi katika maisha yako
kila wakati, tofauti na ambavyo ungeacha
mambo yaende tu kama yalivyo.
Kesho
yako ya mafanikio makubwa, inajengwa na mawazo yako bora ya sasa, na pia
inajengwa na matendo yako bora ya sasa, kwa namna yoyote ukishindwa kuangalia
vitu hivyo matokeo yako ya kesho yatakuwa mabaya sana.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.