Jan 21, 2018
KIPAJI CHAKO; Wosia Wa Mafanikio Kutoka Kwa Mama.
Ilikuwa
ni majira ya saa tisa kamili usiku ambapo ndege,wanyama na viumbe vyote vyenye
uhai na visivyo vya uhai vilikuwa havipo duniani kwa muda, mida hiyo viumbe
vyote vilikuwa vimelala. Usingizi ndio uliokuwa umetawala nyakati hizo.
Ikumbukwe
nyakati hizo hali ilikuwa ni shwari sana, yenye kuhamasisha sana kila kiumbe
mwenye pumzi kuweza kufanya tafakari ya jinsi gani atapanga siku yake
inayofuata, pia kutafakari mchana wake ulikuwaje kwa siku hiyo.
Mida
hiyo nilikuwa nimeamka kwa ajili ya kujisomea, hii ilikuwa ni ratiba yangu ya
kila siku kuweza kuamka mida hiyo na kuuanza kujisomea masomo mbalimbali kwani
ni muda ambao niliuona na tulivu sana kwangu.
Siku
hiyo nilikuwa nimepaanga kurudia kujisomea somo la kiswahili kwani siku ile
mchana wake, wakati nikiwa shuleni sikumuelewa vizuri mwalimu wangu, hivyo
niliona ni vyema kutumia wasaa huo kuweza kujikumbusha.
Wakati
naendelea kujimoea nilimsikia baba yangu akikohoa kwa kikohozi ambacho hata
mimi binafsi kiukweli kilinistua sana, baba alikohoa kama mara sita mfululizo
hivi pasipo kupumzika. Mara baada ya kukohoa vile nilimsikia baba akiita kwa
sauti ya chinichini.
“mke
wangu amka nakufa mwenzio” nikamsikia
baba akiendelea kuita tena,
,,,,,,,
Mama Ester mke wangu, naomba uamke unisadie nakufa mwenzio,,,,,,,,,,,,,
Sauti
ile ya baba ilinifanya niache kuendelea kusoma, kwani iligopesha sana na
ukizingatia kwa wakati ule nilikuwa bado mdogo hivyo nilikuwa naogopa sana hadithi mbalimbali zilizokuwa zinahusu kifo.
mmmmmmmh!
Nilishusha pumzi ndefu sana huku akili na mawazo yangu, sambamba na akili yangu iliwaza vingi visivyokuwa na
majibu, hivi baba haya maneno ambayo anayesema ana maanisha nini? Niliwaza
mwenyewe.
Mawazo
na akili yangu viliganda kwa muda mithiri ya barafu ya mlima kilimanjaro,
niliwaza pamoja na ugonjwa huu ambao ulikuwa unamsumbua baba hivi akifa
atanisomesha nani? Niliwaza pasipo kupata majibu.
Wakati
huo hali ya mama ilikiwa si nzuri pia,
kwani naye kwa kipindi kile wakati
baba anaumwa mama naye alikuwa ni
mjamzito.
Niliendelea
kutafakakari mambo mbalimbali pasipo kupata majawabu ya kile nilichokuwa
nawaza.
Nilifunika
daftari ambalo nilikuwa nasoma kisha kutega maskio yangu kusikiliza sauti na
kile kilichokuwa kikijiri chumbani kwa baba kwa mama.
Huku
baba angu akiendelea kumwita mama yangu pasipo mafanikio yeyote, ghafla baba
akamua kumuita mama kwa sauti ya ukali kidogo, “mama Ester ina maana hunisiki?
Nakufa mwenzio!
Sauti
ile ya ukali ambayo baba alimuita mama, kwa mbali nilisikia mama akiitaka;
Abeee
mume wangu.........
“Mama
Ester mke wangu kwa kweli mimi hali yangu siku ya leo naona haipo sawa kabisa
hivyo sidhani kama nitapona mke wangu ” sauti ile ya baba yenye kila aina
zote upole na ukarimu zilinifanya
niamini ya kwamba baba alikuwa amezidiwa sana usiku ule.
Nini
kitaendelea, usikose sehemu ya pili ya simulizi hii ya kusimumua ya wosia wa
mama sehemu ya pili…..
0757-909942,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.