Jan 12, 2018
Usiache Siku Yako Ikaisha Bila Kufanya Mambo Haya.
Yambo mambo matatu ambayo hutakiwi kuacha kuyafanya kila siku. Kwa
kifupi, kila siku inapoanza na hadi inapoisha ni lazima uhakikishe mambo hayo
umeyafanya kikamilifu. Mambo hayo yatakusaidia sana kukujenga kwenye maisha
yako kwa jinsi siku zinavyokwenda mbele.
Mambo haya muhimu ambayo nataka wewe rafiki yangu uyajue ni kama
haya yafuatayo;-
1. Kujifunza.
Ni muhimu
sana kuhakikisha umejifunza kitu cha kukusaidia kwenye maisha yako kila siku,
akili yako lazima iweke kitu. Usiache siku yako ikaisha hivi hivi tu, weka kitu
cha kukusaidia akilini mwako.
Kila unapoamka jifunze kitu, na endelea kujifunza kwa siku
nzima. Ukijfunza inakusaidia sana kukukomaza kifikra na kukujengea akili ya
mafanikio maishani mwako kila wakati. Watu wanaojifunza na kufanyia kazi ndio
wanaofanikiwa pia kwenye maisha.
2. Kutoa upendo.
Ni muhimu pia
sana kwako kutoa upendo ulionao na kwa wengine pia kila iitwapo leo. Hutakiwi
kuishi kwa uadui, upendo unahitajika ili kuifanya dunia iwe sehemu salama kwako
na kwa wengine pia.
Kama una ugomvi na watu achana na watu hao. Ishi maisha ya
upendo kwa kuwapenda wengine na hiyo itakusaidia kujenga mahusiaono mazuri sana
ambayo yataweza kudumu kwa muda mrefu na kwa manufaa.
3. Kutoa kila ulichonacho kikamilifu.
Huhitaji hapa
kuuliza, ni lazima utoe kila ulichonacho kwa ukamilifu wote kupitia kazi
unayoifanya. Nini unafanya hapo ulipo, toa uwezo wako woote yaani usibakishe
kitu kama ni juhudi weka zote.
Kama ni maarifa ya aina fulani uliyonayo, hakikisha pia unatoa
yote kwa ukamilifu ili kuwasaidia wengine. Kwa kila ukifanyacho, kitoe kwa
ukamilifu sana ili kiweze kuleta msaada na matokeo bora kwa watu wengine kwenye
maisha yao pia.
Ukifanyia
kazi mambo hayo yatakusaidia sana kuweza kupiga hatua na hata kubadilisha
maisha yako.
Uwe na wakati
mwema na siku njema pia, kila la kheri na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kuweza kujifunza kila
siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.